Kwenye viunga vya wasomi na wanasiasa, wachambuzi na wanaharakati hili jambo linaendelea kujadiliwa sana.
Katika dhamira ya kuleta mabadiliko Rais Magufuli anaonekana kuwa na dhamira lakini amekosa wapi na lipi ashike.
Amekosa mipango ambayo ingeihakikishia Tanzania mabadiliko aliyokusudia kupita kwenye njia nzuri na sasa dhamira hiyo inwakwaza watanzania wengi.
Kilichoko CCM
Si tu kwamba Magufuli ametengeneza CCM mpya ya wakuja na wanaomuunga mkono, hata ilani ya chama na vipaumbele vyake havifuati.
Zipo taarifa za mgawanyiko mkubwa wa siri na tofauti za kimtazamo kuhusu namna anavyoendesha nchi.
Zipo taarifa za kujiamulia mambo ambayo hayapati baraka za chama na zipo taarifa za wazee kumsusa.
Zipo taarifa za kuvigawa vyombo vya kiutawala na kuweka watu wake hata kama wana makandokando ilimradi wanamuunga mkono na wale anaohisi watamsaidia kufika dhamira yake hata kama anavunja taratibu.
Kwa hali hiyo hata CCM kuna kuugulia na kuchukizwa kuhusu mambo yanavyokwenda ndani ya nchi.
Hata huko CCM kuna lawama na kutukuza . Kuna lawama za Kujifanyia mambo kwa mtazamo wa mtu na si wa chama na nchi kwa ujumla.
Kuhusu mageuzi anayotaka Magufuli kuelekea uzalendo na maendeleo chini ya chama kimoja na kuviza demokrasia kuna lawama kwa nini asipitishe mabadiliko katika utaratibu na maelewano na kuamua kutumia nyenzo zilizowekwa kisheria badala yake anaonekana kubaka tu na kuamrisha?
Lawama hizi zinakuja kwa kule kuichafua nchi na kutumia mbinu zinazoweza kuhatarisha amani. Hata CCM watu wamenuna. (Vyanzo vyetu mbalimbali)
Wanasiasa na makundi mengine
Kundi hili nalo linachukizwa, hapa wapo wanasiasa, wanaharakati, asasi za kiraia na kisheria na baadhi ya taasisi za dini. Wakati mwengine hulazimika kutumika Uzalendo tu ili mambo yasiharibike.
Niliwahi kupata taarifa kuhusu maamuzi ambayo yangekwisha kuchukuliwa dhidi ya kudai demokrasia lakini utu na uzalendo unawapa wakati mgumu wanasiasa na wanaharakati kiasi cha kujipa matumaini ya viongozi kujifunza na kutoa muda zaidi wakiamini wazee na wastaafu wataingilia kati.
Kikubwa ni huu Umagufuli na sio UCCM. Kama ni CCM tu hayo mabadiliko yangepitishwa kwenye njia zake kwa maslahi mapana ya Taifa hata kama kungetumika mbinu ovu lakini zilizokwenda shule.
Magufuli anafeli si tu kwa mbinu lakini kuwachukulia wapinzani kuwa si watu muhimu kwenye nchi na hatima yake anaidhoofisha kwanza nchi mbele ya ulimwwengu na CCM mbele ya uso wa dunia.
Ieleweke kwamba njia za mabadiliko ya kimfumo huulizwa wananchi jambo ambalo Magufuli hajalifanya.
Mifano inayotolewa ni kuja kwa vyama vingi na kuondowa mfumo wa chama kimoja wananchi waliulizwa na likawa jambo la kitaifa. Hata kama wachache walitaka mabadiliko lakini mfumo wa mabadiliko ulifuatwa kwa kiasi chake.
Leo Magufuli anauwa demokrasia na vyama vingi kinyemela ambayo ni njia isiyo salama kwa afya ya nchi. Hatima yake kunajitokeza chuki, visasi, na kuvunja umoja wetu.
UMAGUFULI v/s UTARATIBU
Bahati mbaya Rais anapotoshwa na baadhi ya wateule na viongozi wenye maslahi binafsi.
Kwani kuna ubaya gani kama Rais angeleta mjadala mezani wa kufanya mabadiliko ya kimfumo na kuwachukuwa wanasiasa wote kwenye mjadala wa kitaifa ili kutengeneza strong politics zenye vionjo vya uzalendo kwa kuandaliwa mfumo, ambapo watu wote muhimu wakiwemo wanasiasa kuhakikishiwa vipawa vyao na mitazamo yao ingeheshimiwa kwenye mabadiliko hayo?
Kwa nini kusingeanza na Ajenda ya Kitaifa ya Mjadala wa mabadiliko na kupelekwa kwa wasomi kisha ndio kukatazamwa uungwaji mkono.
Baadae zingetumika njia za kidemokrasia Bungeni kuamua kwa wengi wape ili jambo likapata Baraka za wananchi na uwakilishi?
Kwa nini Magufuli kaamua kufanya kinyemela na kufuata mtazamo wake na si mtazamo wa wananchi walio wengi?
Kuwa na nia nzuri ni jambo moja na kuwa na mikakati mizuri ni jambo la pili. Magufuli ana nia nzuri lakini ana mipango mibovu.
Kwa Tanzania ilipofika katika demokrasia mabadiliko yoyote yasiyopata Baraka za makundi muhimu ni kuhatarisha umoja wetu na ustawi wa Tanzania.
USHAURI
Rais Magufuli tumia fursa iliyobaki ya kutuliza hali ili ukiondoka tukupe tuzo ya kitaifa bila kujali vyama. Anzia mwanzo na usianzie mwisho katika njia ya kutaka kuleta mabadiliko.
Itisha mjadala wa kitaifa na ukubali kukosolewa ili upate kupenyeza fikra zako. Watanzania ni waelewa na ni rahisi kusamehe.
Naamini watakusamehe na watakuwa nawe kwenye safari ya kweli ya mabadiliko. Nenda pale UDSM na kwenye vigoda upate ushauri hutojuta.
Walete wanasiasa pamoja na wewe uwe mlenzi wa maridhiano, sikiliza kilio chao, fuata ushauri mzuri utakaotolewa jenga gurudumu moja tu utaeleweka na sio kubaguwa na kuwaweka wanaokupinga kwenye kapu la wasio wazalendo.
Fikiria Katiba mpya hii ni kete iliyobaki kwa haya mambo ya kuchukiza na kutukuza ambayo ndani ya miaka 4 yamejitokeza.
Tanzania ni yetu sote.
Kishada.