Kuanguka kwa Demokrasia Tanzania: U-Magufuli na mabadiliko yasiyo na baraka za Watanzania

Pascal nani kakuambia watanzania wanataka maendeleo hawataki demokrasia? Vyama vingi vyenye demokrasia ya kujadili mambo ndiyo vinatakiwa na Watanzania ili kujiletea maendeleo.
Ona baada ya Mwalimu kukabidhi madaraka kwa Mwinyi na kuruhusu vyama vingi njia ya kupingana kwa namna ile ya kuzalisha vijana kama Macghee, Kaptein Komando, Kaptein Hanspope au wazee kama Kamaliza, Bibi Titi, Kambona nk imepotea imekuwa ya kutangaza Sera, kupinga na hata ikibidi kukebehi na kushangilia majanga ya mwenzako (mfano kukamatiwa ndege, kunyimwa msaada) nk
 
Unapimaje kukubalika chama na jeshi, usalama na wananchi? Kwa hiyo jeshi, usalama na wananchi ndio wanakubaliana na huu mwenendo wa kunajisi box la kura?
Wewe Mwanao akija na mchumba unayafahamu kuwa ni mvuta bangi na mlevi Ila Mwanao hafahamu hutanajisi penzi Lao? Ni hivi kama inawezekana kushawishi wananchi watoe kura, inashindikana vipi kushawishi majeshi ya ulinzi na usalama mlindwe msiibiwe kura? We unadhani wananchi wakikukubali tu ww tindo utapewa nchi hata kama jeshi na usalama wanajua hufai? Usiende kwa wananchi kama unajua jeshi na usalama hawatakupa sapoti na kukulinda. Kila mwaka Tumeibiwa, Tumeibiwa, inachosha sasa.
 
Kwa hiyo jeshi ndio linaloratibu wizi wa kura, kwanini wasijitokeze wakaongoza kabisa nchi? Acha nikachekee mbali, sikujua haya yanaondelea kwenye uchaguzi ya kupita bila kupingwa ni utashi wa jeshi na vyombo vya usalama.
 
Tanzania Tunafuata Tanzanian Democracy model ambayo ni part of African Democracy.

Swali la msingi ni Watanzania wanataka nini kati ya demokrasia na maendeleo?. Watanzania wanataka maendeleo, na maendeleo hayana chama, hivyo rais Magufuli analeta maendeleo kupitia mwelekeo wa chama kimoja, kazi imeanza leo kwenye huu uchaguzi wa serikali za mitaa na kukamilika mwakani katika uchaguzi Mkuu kwa Tanzania kurejea kuwa nchi ya chama kimoja, tukiisha pata maendeleo ndipo tutaigeukia demokrasia.

P
wewe mzee wewe😂😂😂😂😂
 
Wale watukuzaji wanasahau haraka. Mwalimu Nyerere kama muasisi wa Taifa hili. Miaka zaidi ya 25 ya Utawala alitupa fundisho moja kubwa.

huyu Mwalimu alikuwa Mzalendo na kwa zidi ya miaka 25 alitunmia mamlaka yake kuweka misingi ya Utaifa hadi kuzaliwa azimio la Arusha.

Kumbukeni nchi ilivyopita. Alilazimika kuleta Vyama vingi , alijifunza makosa aliyofanya ya kutosikiliza mawazi kinzani. Alijifunza kufuata siasa zenye kuungwa mkono na Ulimwengu.

Well pengine tumeona vyama vingi havitufai lkn na Chama kimoja kilishaproof wrong kitambo. Sasa jee kama kuna haja ya kubadilisha mwelekeo kwa nini taratibu zisifuatwe?

Kwa nini kusiwe na ushirikishwaji.

Tujifunze kupitia kwa huyo huyo Mwalimu. Hapo ndipo Magufuli anapokosea.
 
Kwa hiyo jeshi ndio linaloratibu wizi wa kura, kwanini wasijitokeze wakaongoza kabisa nchi? Acha nikachekee mbali, sikujua haya yanaondelea kwenye uchaguzi ya kupita bila kupingwa ni utashi wa jeshi na vyombo vya usalama.
Ww Ndo unayesema kuna unajisi wa box la kura, na mm nikakwambia kama unajisi upo na majeshi yapo na wanakuangalia tu unavyonajisiwa na ww huna ushawishi wa kuwafanya wakulinde basi shida unayo wewe. 95 tumeibiwa, 2000 waliiba, 2005 wameiba, 2010' tumeibiwa, 2015 ni wizi tu, tumeshinda. Kweli nenda kachekee mbali.
 
Article moja matata sana! This is JF
Kwenye viunga vya wasomi na wanasiasa, wachambuzi na wanaharakati hili jambo linaendelea kujadiliwa sana.

Katika dhamira ya kuleta mabadiliko Rais Magufuli anaonekana kuwa na dhamira lakini amekosa wapi na lipi ashike.

Amekosa mipango ambayo ingeihakikishia Tanzania mabadiliko aliyokusudia kupita kwenye njia nzuri na sasa dhamira hiyo inwakwaza watanzania wengi.

Kilichoko CCM
Si tu kwamba Magufuli ametengeneza CCM mpya ya wakuja na wanaomuunga mkono, hata ilani ya chama na vipaumbele vyake havifuati.

Zipo taarifa za mgawanyiko mkubwa wa siri na tofauti za kimtazamo kuhusu namna anavyoendesha nchi.

Zipo taarifa za kujiamulia mambo ambayo hayapati baraka za chama na zipo taarifa za wazee kumsusa.

Zipo taarifa za kuvigawa vyombo vya kiutawala na kuweka watu wake hata kama wana makandokando ilimradi wanamuunga mkono na wale anaohisi watamsaidia kufika dhamira yake hata kama anavunja taratibu.

Kwa hali hiyo hata CCM kuna kuugulia na kuchukizwa kuhusu mambo yanavyokwenda ndani ya nchi.

Hata huko CCM kuna lawama na kutukuza . Kuna lawama za Kujifanyia mambo kwa mtazamo wa mtu na si wa chama na nchi kwa ujumla.

Kuhusu mageuzi anayotaka Magufuli kuelekea uzalendo na maendeleo chini ya chama kimoja na kuviza demokrasia kuna lawama kwa nini asipitishe mabadiliko katika utaratibu na maelewano na kuamua kutumia nyenzo zilizowekwa kisheria badala yake anaonekana kubaka tu na kuamrisha?

Lawama hizi zinakuja kwa kule kuichafua nchi na kutumia mbinu zinazoweza kuhatarisha amani. Hata CCM watu wamenuna. (Vyanzo vyetu mbalimbali)

Wanasiasa na makundi mengine
Kundi hili nalo linachukizwa, hapa wapo wanasiasa, wanaharakati, asasi za kiraia na kisheria na baadhi ya taasisi za dini. Wakati mwengine hulazimika kutumika Uzalendo tu ili mambo yasiharibike.

Niliwahi kupata taarifa kuhusu maamuzi ambayo yangekwisha kuchukuliwa dhidi ya kudai demokrasia lakini utu na uzalendo unawapa wakati mgumu wanasiasa na wanaharakati kiasi cha kujipa matumaini ya viongozi kujifunza na kutoa muda zaidi wakiamini wazee na wastaafu wataingilia kati.

Kikubwa ni huu Umagufuli na sio UCCM. Kama ni CCM tu hayo mabadiliko yangepitishwa kwenye njia zake kwa maslahi mapana ya Taifa hata kama kungetumika mbinu ovu lakini zilizokwenda shule.

Magufuli anafeli si tu kwa mbinu lakini kuwachukulia wapinzani kuwa si watu muhimu kwenye nchi na hatima yake anaidhoofisha kwanza nchi mbele ya ulimwwengu na CCM mbele ya uso wa dunia.

Ieleweke kwamba njia za mabadiliko ya kimfumo huulizwa wananchi jambo ambalo Magufuli hajalifanya.

Mifano inayotolewa ni kuja kwa vyama vingi na kuondowa mfumo wa chama kimoja wananchi waliulizwa na likawa jambo la kitaifa. Hata kama wachache walitaka mabadiliko lakini mfumo wa mabadiliko ulifuatwa kwa kiasi chake.

Leo Magufuli anauwa demokrasia na vyama vingi kinyemela ambayo ni njia isiyo salama kwa afya ya nchi. Hatima yake kunajitokeza chuki, visasi, na kuvunja umoja wetu.

UMAGUFULI v/s UTARATIBU
Bahati mbaya Rais anapotoshwa na baadhi ya wateule na viongozi wenye maslahi binafsi.

Kwani kuna ubaya gani kama Rais angeleta mjadala mezani wa kufanya mabadiliko ya kimfumo na kuwachukuwa wanasiasa wote kwenye mjadala wa kitaifa ili kutengeneza strong politics zenye vionjo vya uzalendo kwa kuandaliwa mfumo, ambapo watu wote muhimu wakiwemo wanasiasa kuhakikishiwa vipawa vyao na mitazamo yao ingeheshimiwa kwenye mabadiliko hayo?

Kwa nini kusingeanza na Ajenda ya Kitaifa ya Mjadala wa mabadiliko na kupelekwa kwa wasomi kisha ndio kukatazamwa uungwaji mkono.

Baadae zingetumika njia za kidemokrasia Bungeni kuamua kwa wengi wape ili jambo likapata Baraka za wananchi na uwakilishi?

Kwa nini Magufuli kaamua kufanya kinyemela na kufuata mtazamo wake na si mtazamo wa wananchi walio wengi?

Kuwa na nia nzuri ni jambo moja na kuwa na mikakati mizuri ni jambo la pili. Magufuli ana nia nzuri lakini ana mipango mibovu.

Kwa Tanzania ilipofika katika demokrasia mabadiliko yoyote yasiyopata Baraka za makundi muhimu ni kuhatarisha umoja wetu na ustawi wa Tanzania.

USHAURI
Rais Magufuli tumia fursa iliyobaki ya kutuliza hali ili ukiondoka tukupe tuzo ya kitaifa bila kujali vyama. Anzia mwanzo na usianzie mwisho katika njia ya kutaka kuleta mabadiliko.

Itisha mjadala wa kitaifa na ukubali kukosolewa ili upate kupenyeza fikra zako. Watanzania ni waelewa na ni rahisi kusamehe.

Naamini watakusamehe na watakuwa nawe kwenye safari ya kweli ya mabadiliko. Nenda pale UDSM na kwenye vigoda upate ushauri hutojuta.

Walete wanasiasa pamoja na wewe uwe mlenzi wa maridhiano, sikiliza kilio chao, fuata ushauri mzuri utakaotolewa jenga gurudumu moja tu utaeleweka na sio kubaguwa na kuwaweka wanaokupinga kwenye kapu la wasio wazalendo.

Fikiria Katiba mpya hii ni kete iliyobaki kwa haya mambo ya kuchukiza na kutukuza ambayo ndani ya miaka 4 yamejitokeza.

Tanzania ni yetu sote.

Kishada.
 
Kwa hiyo jeshi ndio linaloratibu wizi wa kura, kwanini wasijitokeze wakaongoza kabisa nchi? Acha nikachekee mbali, sikujua haya yanaondelea kwenye uchaguzi ya kupita bila kupingwa ni utashi wa jeshi na vyombo vya usalama.
We mkeo umemtafutia kazi halafu kila mwisho wa mwezi anakuja kukulilia bosi kamzulumu mshahara' wewe kwa bosi huendi kuuliza kulikoni, mkeo haachi kazi na ww kazi yako kulalamika kwa marafiki tu bosi anavyomwonea mkeo. Ww upo sawa kweli?
 
Tanzania Tunafuata Tanzanian Democracy model ambayo ni part of African Democracy.

Swali la msingi ni Watanzania wanataka nini kati ya demokrasia na maendeleo?. Watanzania wanataka maendeleo, na maendeleo hayana chama, hivyo rais Magufuli analeta maendeleo kupitia mwelekeo wa chama kimoja, kazi imeanza leo kwenye huu uchaguzi wa serikali za mitaa na kukamilika mwakani katika uchaguzi Mkuu kwa Tanzania kurejea kuwa nchi ya chama kimoja, tukiisha pata maendeleo ndipo tutaigeukia demokrasia.

P
Nilikuwa sijamwelewa Mh.Raisi.
Kumbe anaposema maendeleo hayana chama anamaanisha vyama pinzani havihitajiki?
 
I am very sorry sikubaliani na ww hata kidogo, ushauri wako una chembe chembe za uchadema, unaposema umagufuli in English is Magulification sasa hebu google upate majibu yako kutoka kwa mmoja wa wasomi bora kabisa Africa. Acha mimi nikushauri ondoa uchadema kichwani mwako na ukubaliane na mimi this country or any country in Africa wanahitaji umagufuli you hate it or like it but Magufuli is the best president this country has ever had. Ni Rais anaethubutu na amefanya makubwa mengi and of course ana mapungufu yake but mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Sasa hebu turudi kwa the so called demokrasia. Hivi ww unaielewaje demokrasia? Hivi vyama vya upinzani kila siku wanapiga kelele demokrasia inabakwa lakini wanasahau wabakaji wakubwa ni wao. Hakuna demokrasia yoyote vyama vya upinzani kuna udikteta wa hali ya juu but you don’t see that, Leo kuna kesi ya mkulima kuhusu ukomo wa urais antaka katiba itafsiriwe lakini ACT pamoja na TLS (chama kipya cha upinzani) wamejiunga all they want is to make sure mahakama haiondoi ukomo wa rais but at the same time upinzani wao ruksa kukalia viti vyao for as long as they want. My question to you now hivi kweli unaamini kuna demokrasia ya kweli upinzani especially ACT and chadema??? If your answer is yes then you don’t know what does democracy mean. Tatizo kubwa upinzani ni ubinafsi na wanafanya mambo mengi yasyostahili kama udikteta wa wazi kabisa lakini bahati mbaya mazwazwa kama wewe hamuoni, leo hii magufuli akitaka kufanya mchakato wa kuondoa ukomo wa urais OMG Hiyo kelele itasikika dunia nzima, so please upinzani nendeni shule demokrasia sio maandamano, demokrasia ya kweli ni lazima iwe na ukomo wa uongozi sasa hivi bongo unfortunately hatuna vyama vya upinzani bali tuna makampuni binafsi yanayojiita opposition’s kumbe ni mafisadi. La mwisho watanzania tuwe na shukurani kwa JPM kafanya mengi makubwa na sikatai ana mapungufu yake kama binadamu wengine but i do know mazwazwa wengi kazi kuwaelimisha but we won’t give up.
Na wewe umeandika heka nzima ukionyesha uhusiano wako wote na mcc...rubbish
 
Nilikuwa sijamwelewa Mh.Raisi.
Kumbe anaposema maendeleo hayana chama anamaanisha vyama pinzani havihitajiki?
Kuna kuvunjwa taratibu. Baadhi yetu wanasema ndio African Democracy. Kumbe tumefika huko kwa njia za panya si uletwe mjadala tu tuendelee kupendana.
 
Naona kuna transition inafanyika. Pengine wadau wa nchi wanaelewa. Tatizo ni kupitia njia za Panya na kuvurugana. Lete mjadala kama kuja kwa vyama vingi kulivyofanyika. Hakuna tatizo.
 
Naomba watu wajadili mada. Hapo kuna mambo mengi yanahitaji tafakuri.
 
Hapo nmekusoma vema
Tanzania Tunafuata Tanzanian Democracy model ambayo ni part of African Democracy.

Swali la msingi ni Watanzania wanataka nini kati ya demokrasia na maendeleo?. Watanzania wanataka maendeleo, na maendeleo hayana chama, hivyo rais Magufuli analeta maendeleo kupitia mwelekeo wa chama kimoja, kazi imeanza leo kwenye huu uchaguzi wa serikali za mitaa na kukamilika mwakani katika uchaguzi Mkuu kwa Tanzania kurejea kuwa nchi ya chama kimoja, tukiisha pata maendeleo ndipo tutaigeukia demokrasia.

P
 
Tanzania Tunafuata Tanzanian Democracy model ambayo ni part of African Democracy.

Swali la msingi ni Watanzania wanataka nini kati ya demokrasia na maendeleo?. Watanzania wanataka maendeleo, na maendeleo hayana chama, hivyo rais Magufuli analeta maendeleo kupitia mwelekeo wa chama kimoja, kazi imeanza leo kwenye huu uchaguzi wa serikali za mitaa na kukamilika mwakani katika uchaguzi Mkuu kwa
Tanzania kurejea kuwa nchi ya chama kimoja, tukiisha pata maendeleo ndipo tutaigeukia demokrasia.

P
. sidhani kama Magufuli atafanikiwa kufikia maendeleo ya kweli labda u dikte
ta
 
Tanzania Tunafuata Tanzanian Democracy model ambayo ni part of African Democracy.

Swali la msingi ni Watanzania wanataka nini kati ya demokrasia na maendeleo?. Watanzania wanataka maendeleo, na maendeleo hayana chama, hivyo rais Magufuli analeta maendeleo kupitia mwelekeo wa chama kimoja, kazi imeanza leo kwenye huu uchaguzi wa serikali za mitaa na kukamilika mwakani katika uchaguzi Mkuu kwa Tanzania kurejea kuwa nchi ya chama kimoja, tukiisha pata maendeleo ndipo tutaigeukia demokrasia.

P
Umechanganya demokrasia uendana na,maendeleo,je maendeleo ya vitu yanayofanyika yatawezaleta maendeleo? Oneman show is equal to total failure
 
Siku zaja si mbali japo ngumu kuamini sasa ccm na upinzani wataongea lugha moja wataungana dhidi ya adui wao.
 
. sidhani kama Magufuli atafanikiwa kufikia maendeleo ya kweli labda u dikte
ta
Huwezi endelea bila kushirikiana na mabeberu.Hakuna nchi yeyeto duniani iliyoendelea kwa kupingana na mabeberu,wao ndo wamebeba dhima na ngekewa ya maendeleo
 
Back
Top Bottom