Kuanguka kwa Demokrasia Tanzania: U-Magufuli na mabadiliko yasiyo na baraka za Watanzania

Tanzania Tunafuata Tanzanian Democracy model ambayo ni part of African Democracy.

Swali la msingi ni Watanzania wanataka nini kati ya demokrasia na maendeleo?. Watanzania wanataka maendeleo, na maendeleo hayana chama, hivyo rais Magufuli analeta maendeleo kupitia mwelekeo wa chama kimoja, kazi imeanza leo kwenye huu uchaguzi wa serikali za mitaa na kukamilika mwakani katika uchaguzi Mkuu kwa Tanzania kurejea kuwa nchi ya chama kimoja, tukiisha pata maendeleo ndipo tutaigeukia demokrasia.

P
Hong Kong panamaendeleo tayari ,unaonaje yanayotokea n.k,hivyo sikweli tuamini ktk uchuro huo kwamba baada ya vitu ndipo tudai.nadhan hapa inayolindwa ni ccm sio RAIA wema tz
 
Usilazimishe upuuzi wako kila mtu uauunge mkono, kati ya baba wa taifa na huyu jiwe ni nani anapaswa kufuatwa zaidi, yaani JK aanzishe utaratibu wa vyama vingi kwa maslah ya kujenga selikari inayokosolewa arafu atokee mtu/kikundi cha watu wavunje utaratibu kwa maslah yao binafsi..huu sio uungwana hata kidogo.
Usiseme kikundi cha watu,sema Wasukuma!
 
Tanzania Tunafuata Tanzanian Democracy model ambayo ni part of African Democracy.

Swali la msingi ni Watanzania wanataka nini kati ya demokrasia na maendeleo?. Watanzania wanataka maendeleo, na maendeleo hayana chama, hivyo rais Magufuli analeta maendeleo kupitia mwelekeo wa chama kimoja, kazi imeanza leo kwenye huu uchaguzi wa serikali za mitaa na kukamilika mwakani katika uchaguzi Mkuu kwa Tanzania kurejea kuwa nchi ya chama kimoja, tukiisha pata maendeleo ndipo tutaigeukia demokrasia.

P
P,
Watanzania wanataka demokrasia na maendeleo pamoja. Na ndiyo maana hata watu wa CCM hawawezi kusema wazi kwamba Watanzania hawaitaji vyama vingi na kukiweka kura leo itakuwa zaidi ya 70% ya Watanzania wanataka demokrasia. Sababu kubwa ni utamaduni wetu tofauti na nchi nyingine Watanzania wanaishi maisha ambayo hayafanani kuna Massai mfano na watu wa Pwani hawa ni watu tofauti kwenye kila kitu lakini tuko nchi mmoja sasa bila demokrasia ni tabu hapo. Vilevile sababu kubwa ya Magu kupinga vyama ni za kiuchumi lakini naomba ulifanyie kazi hili kwa research zangu nimegundua sababu kubwa ni gharama na rushwa kubwa iliyokuwepo ndani ya CCM.
Magu alivyoingia madarakani akagundua kuna rushwa sana ndani ya CCM ili kupata pesa za kampeni na kuendesha chama ambacho kilikuwa kinaenda kwa hasara. Kulikuwa kuna hongo na wizara za wakina kigoda waliweka wafanyabiashara kama njia ya kutoa na kuiba pesa serikalini EPA mfano pesa nyingi ilikuwa iende chamani. Share za Voda ambazo Rostam alikuja kuziuza wakati wa Magu ni zile za Chama na alifanya makusudi ili aweze kuweka ukaribu na riasi ajae maana zilikuwa kwenye jina lake angeweza kizizika ni zaidi ya tsh 200B. Vilevile pesa za majengo zilikuwa zinaenda kwa vigogo n.k.
Sasa Magu ameona strategically akizuia wapinzani ndiyo njia pekee ya kuzuia CCM kutumia pesa za chaguzi pesa ambazo yeye anaina kama ni upotevu wa pesa bure. Hivyo Magu sababu za kuua upinzani ni kiuchumi lakini ni kwasababu ya matatizo ya CCM na sio upinzani. Hivyo kwa ufupi kubana matumizi ni kubana Upinzania ili CCM isiombe pesa kinyemela za serikali kwa chaguzi. Na kwa uoga bado hana nguvu ya kuziia hizo catel za ndani ya chama ambazo zinataka pesa na vigogo ambao hawako productive. Tatizo hapa ni mfumo ndani ya CCM wa kupata pesa.

Kusema upinzani hausaidii nchi si kweli.
 
Kwenye viunga vya wasomi na wanasiasa, wachambuzi na wanaharakati hili jambo linaendelea kujadiliwa sana.

Katika dhamira ya kuleta mabadiliko Rais Magufuli anaonekana kuwa na dhamira lakini amekosa wapi na lipi ashike.

Amekosa mipango ambayo ingeihakikishia Tanzania mabadiliko aliyokusudia kupita kwenye njia nzuri na sasa dhamira hiyo inwakwaza watanzania wengi.

Kilichoko CCM
Si tu kwamba Magufuli ametengeneza CCM mpya ya wakuja na wanaomuunga mkono, hata ilani ya chama na vipaumbele vyake havifuati.

Zipo taarifa za mgawanyiko mkubwa wa siri na tofauti za kimtazamo kuhusu namna anavyoendesha nchi.

Zipo taarifa za kujiamulia mambo ambayo hayapati baraka za chama na zipo taarifa za wazee kumsusa.

Zipo taarifa za kuvigawa vyombo vya kiutawala na kuweka watu wake hata kama wana makandokando ilimradi wanamuunga mkono na wale anaohisi watamsaidia kufika dhamira yake hata kama anavunja taratibu.

Kwa hali hiyo hata CCM kuna kuugulia na kuchukizwa kuhusu mambo yanavyokwenda ndani ya nchi.

Hata huko CCM kuna lawama na kutukuza . Kuna lawama za Kujifanyia mambo kwa mtazamo wa mtu na si wa chama na nchi kwa ujumla.

Kuhusu mageuzi anayotaka Magufuli kuelekea uzalendo na maendeleo chini ya chama kimoja na kuviza demokrasia kuna lawama kwa nini asipitishe mabadiliko katika utaratibu na maelewano na kuamua kutumia nyenzo zilizowekwa kisheria badala yake anaonekana kubaka tu na kuamrisha?

Lawama hizi zinakuja kwa kule kuichafua nchi na kutumia mbinu zinazoweza kuhatarisha amani. Hata CCM watu wamenuna. (Vyanzo vyetu mbalimbali)

Wanasiasa na makundi mengine
Kundi hili nalo linachukizwa, hapa wapo wanasiasa, wanaharakati, asasi za kiraia na kisheria na baadhi ya taasisi za dini. Wakati mwengine hulazimika kutumika Uzalendo tu ili mambo yasiharibike.

Niliwahi kupata taarifa kuhusu maamuzi ambayo yangekwisha kuchukuliwa dhidi ya kudai demokrasia lakini utu na uzalendo unawapa wakati mgumu wanasiasa na wanaharakati kiasi cha kujipa matumaini ya viongozi kujifunza na kutoa muda zaidi wakiamini wazee na wastaafu wataingilia kati.

Kikubwa ni huu Umagufuli na sio UCCM. Kama ni CCM tu hayo mabadiliko yangepitishwa kwenye njia zake kwa maslahi mapana ya Taifa hata kama kungetumika mbinu ovu lakini zilizokwenda shule.

Magufuli anafeli si tu kwa mbinu lakini kuwachukulia wapinzani kuwa si watu muhimu kwenye nchi na hatima yake anaidhoofisha kwanza nchi mbele ya ulimwwengu na CCM mbele ya uso wa dunia.

Ieleweke kwamba njia za mabadiliko ya kimfumo huulizwa wananchi jambo ambalo Magufuli hajalifanya.

Mifano inayotolewa ni kuja kwa vyama vingi na kuondowa mfumo wa chama kimoja wananchi waliulizwa na likawa jambo la kitaifa. Hata kama wachache walitaka mabadiliko lakini mfumo wa mabadiliko ulifuatwa kwa kiasi chake.

Leo Magufuli anauwa demokrasia na vyama vingi kinyemela ambayo ni njia isiyo salama kwa afya ya nchi. Hatima yake kunajitokeza chuki, visasi, na kuvunja umoja wetu.

UMAGUFULI v/s UTARATIBU
Bahati mbaya Rais anapotoshwa na baadhi ya wateule na viongozi wenye maslahi binafsi.

Kwani kuna ubaya gani kama Rais angeleta mjadala mezani wa kufanya mabadiliko ya kimfumo na kuwachukuwa wanasiasa wote kwenye mjadala wa kitaifa ili kutengeneza strong politics zenye vionjo vya uzalendo kwa kuandaliwa mfumo, ambapo watu wote muhimu wakiwemo wanasiasa kuhakikishiwa vipawa vyao na mitazamo yao ingeheshimiwa kwenye mabadiliko hayo?

Kwa nini kusingeanza na Ajenda ya Kitaifa ya Mjadala wa mabadiliko na kupelekwa kwa wasomi kisha ndio kukatazamwa uungwaji mkono.

Baadae zingetumika njia za kidemokrasia Bungeni kuamua kwa wengi wape ili jambo likapata Baraka za wananchi na uwakilishi?

Kwa nini Magufuli kaamua kufanya kinyemela na kufuata mtazamo wake na si mtazamo wa wananchi walio wengi?

Kuwa na nia nzuri ni jambo moja na kuwa na mikakati mizuri ni jambo la pili. Magufuli ana nia nzuri lakini ana mipango mibovu.

Kwa Tanzania ilipofika katika demokrasia mabadiliko yoyote yasiyopata Baraka za makundi muhimu ni kuhatarisha umoja wetu na ustawi wa Tanzania.

USHAURI
Rais Magufuli tumia fursa iliyobaki ya kutuliza hali ili ukiondoka tukupe tuzo ya kitaifa bila kujali vyama. Anzia mwanzo na usianzie mwisho katika njia ya kutaka kuleta mabadiliko.

Itisha mjadala wa kitaifa na ukubali kukosolewa ili upate kupenyeza fikra zako. Watanzania ni waelewa na ni rahisi kusamehe.

Naamini watakusamehe na watakuwa nawe kwenye safari ya kweli ya mabadiliko. Nenda pale UDSM na kwenye vigoda upate ushauri hutojuta.

Walete wanasiasa pamoja na wewe uwe mlenzi wa maridhiano, sikiliza kilio chao, fuata ushauri mzuri utakaotolewa jenga gurudumu moja tu utaeleweka na sio kubaguwa na kuwaweka wanaokupinga kwenye kapu la wasio wazalendo.

Fikiria Katiba mpya hii ni kete iliyobaki kwa haya mambo ya kuchukiza na kutukuza ambayo ndani ya miaka 4 yamejitokeza.

Tanzania ni yetu sote.

Kishada.

Kishada,
Hakika huu ni ushauri mujarab kwa mtu yeyote makini mwenye kuchukulia mambo in a broad perspective.
Tatizo la huyu Mkuu wetu wa kaya alishasema..''HATAKI USHAURI WA MTU YEYOTE MAANA YEYE NDIYE RAIS''.
Kwa maneno yake mwenyewe ukimshauri ndiyo UNAPOTEZA KABISA...Hizi ni lugha za kujimwambafy.

Juzi amezindua kitabu cha Rais mstahafu Mzee Ben Mkapa na katika kitabu hicho kuna mambo ya msingi sana ambayo huyu Rais angeliyachukua na kuya-implement angelonekana ni BONGE LA RAIS...!!Mkapa kazungumzia Katiba, Demokrasia na Utawala wa Sheria mambo ambayo kwenye Utawala wa Magufuli yanaleta shida..!!

Pengine tatizo ni Mzee Mkapa kutumia lugha ya ENGLISH katika kitabu chake cha.''My Life, My Purpose''! Yawezekana Magufuli lugha inampa shida. Kwa mtu mnyenyekevu alipaswa kutafuta MKALIMANI lakini pia hata kumwita Mzee Mkapa Ikulu na kuongea nae ana kwa ana ili ampe hayo madini......tunajua Mkapa ndiyo mentor wa JPM....kama anabisha ajifanye kama anajikuna.....!!
 
Hakuna haja ya kuwaumiza ndugu zetu , kuharibu mali zao na kupandikiza chuki kisa kurejesha chama kimoja kwa njia ovu. Ndio tukasema kufuatwe butaratibu tu na nyenzo zipo.

Kuna majitu ya CCM yamejaa hofu na woga...!!!Wanajua Magufuli akipigwa chini au kupunguziwa makali hawaijui kesho yao!!!All in all mabadiliko lazima yatakuja tu maana lazima JPM atamaliza muhula wake!
Taratibu za kufuata na nyenzo mbona zipo tele? Bunge lipo, Katiba ipo na Wananchi wapo....Kinachotakiwa ni kuanzisha mchakato wa referendum ya Katiba mpya ili mambo yaende..!!!Tatizo la Magufulication hataki kusikia hiyo Katiba mpya maana itamnyang'anya Udikteta na Umwambafy vitu anavovipenda sana huyu Rais!!
 
We una chuki tu. Umejaa chuki moyoni mwako.

I am very sorry sikubaliani na ww hata kidogo, ushauri wako una chembe chembe za uchadema, unaposema umagufuli in English is Magulification sasa hebu google upate majibu yako kutoka kwa mmoja wa wasomi bora kabisa Africa. Acha mimi nikushauri ondoa uchadema kichwani mwako na ukubaliane na mimi this country or any country in Africa wanahitaji umagufuli you hate it or like it but Magufuli is the best president this country has ever had.

Ni Rais anaethubutu na amefanya makubwa mengi and of course ana mapungufu yake but mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Sasa hebu turudi kwa the so called demokrasia. Hivi ww unaielewaje demokrasia? Hivi vyama vya upinzani kila siku wanapiga kelele demokrasia inabakwa lakini wanasahau wabakaji wakubwa ni wao.

Hakuna demokrasia yoyote vyama vya upinzani kuna udikteta wa hali ya juu but you don’t see that, Leo kuna kesi ya mkulima kuhusu ukomo wa urais antaka katiba itafsiriwe lakini ACT pamoja na TLS (chama kipya cha upinzani) wamejiunga all they want is to make sure mahakama haiondoi ukomo wa rais but at the same time upinzani wao ruksa kukalia viti vyao for as long as they want. My question to you now hivi kweli unaamini kuna demokrasia ya kweli upinzani especially ACT and chadema???

If your answer is yes then you don’t know what does democracy mean. Tatizo kubwa upinzani ni ubinafsi na wanafanya mambo mengi yasyostahili kama udikteta wa wazi kabisa lakini bahati mbaya mazwazwa kama wewe hamuoni, leo hii magufuli akitaka kufanya mchakato wa kuondoa ukomo wa urais OMG Hiyo kelele itasikika dunia nzima, so please upinzani nendeni shule demokrasia sio maandamano, demokrasia ya kweli ni lazima iwe na ukomo wa uongozi sasa hivi bongo unfortunately hatuna vyama vya upinzani bali tuna makampuni binafsi yanayojiita opposition’s kumbe ni mafisadi. La mwisho watanzania tuwe na shukurani kwa JPM kafanya mengi makubwa na sikatai ana mapungufu yake kama binadamu wengine but i do know mazwazwa wengi kazi kuwaelimisha but we won’t give up.
[/QUOT
 
Tanzania Tunafuata Tanzanian Democracy model ambayo ni part of African Democracy.

Swali la msingi ni Watanzania wanataka nini kati ya demokrasia na maendeleo?. Watanzania wanataka maendeleo, na maendeleo hayana chama, hivyo rais Magufuli analeta maendeleo kupitia mwelekeo wa chama kimoja, kazi imeanza leo kwenye huu uchaguzi wa serikali za mitaa na kukamilika mwakani katika uchaguzi Mkuu kwa Tanzania kurejea kuwa nchi ya chama kimoja, tukiisha pata maendeleo ndipo tutaigeukia demokrasia.

P
Pascal, je miaka 1 (5) iliyobaki inatosha au ndo itabidi tumuongeze ili atimize hayo anayotaka atimize?
 
"Bila CCM madhubuti nchi itayumba" J.K.Nyerere
Hii CCM sio madhubuti na nchi imeshayumba tayari.CCM haijawahi kujiandaa kumdhibiti raisi ambaye ataendesha nchi kinyume na misingi yake.
Nani wa kumfunga paka kengele?Hakuna!
 
Tanzania Tunafuata Tanzanian Democracy model ambayo ni part of African Democracy.

Swali la msingi ni Watanzania wanataka nini kati ya demokrasia na maendeleo?. Watanzania wanataka maendeleo, na maendeleo hayana chama, hivyo rais Magufuli analeta maendeleo kupitia mwelekeo wa chama kimoja, kazi imeanza leo kwenye huu uchaguzi wa serikali za mitaa na kukamilika mwakani katika uchaguzi Mkuu kwa Tanzania kurejea kuwa nchi ya chama kimoja, tukiisha pata maendeleo ndipo tutaigeukia demokrasia.

P
Bwana Pasco kama ni suala la maendeleo hayo unayodai bila utu wala demokrasia, kina Nyerere hawakuwa na sababu ya kusaidia nchi za kusini mwa Afrika kumfurumusha kaburu.Kila mtu ni shahidi jinsi makaburu walivyoiletea maendeleo South Africa.Swali linakuja je waafrika wanahitaji maendeleo pasipo utu, usawa,ukabila na ubaguzi sababu za itikadi?Uko wapi umoja wa kitaifa?
 
Pascal, je miaka 1 (5) iliyobaki inatosha au ndo itabidi tumuongeze ili atimize hayo anayotaka atimize?
Subiri tukiufikia mto ile 2025, tutaangalia kina cha maji ndipo tujadili namna ya kuvuka mto, na tukiona maji ni mengi sana na kasi ni kubwa, then ni busara kusubiria kwa kumpa muda wa kutosha kasi ya maji ipungue na kina cha maji kipungue ili tuvuke salama.
P
 
Tanzania Tunafuata Tanzanian Democracy model ambayo ni part of African Democracy.

Swali la msingi ni Watanzania wanataka nini kati ya demokrasia na maendeleo?. Watanzania wanataka maendeleo, na maendeleo hayana chama, hivyo rais Magufuli analeta maendeleo kupitia mwelekeo wa chama kimoja, kazi imeanza leo kwenye huu uchaguzi wa serikali za mitaa na kukamilika mwakani katika uchaguzi Mkuu kwa Tanzania kurejea kuwa nchi ya chama kimoja, tukiisha pata maendeleo ndipo tutaigeukia demokrasia.

P
Kwahiyo kwa kuwa amepata ushindi mitaa na vijiji vyote sasa tutegemea maendeleo maji, umeme, hospitali barabara za lami kila mtaa na kijiji maana wapinzani walikuwa wanamkwamisha? Pascal Mungu anakuona.
 
Tanzania Tunafuata Tanzanian Democracy model ambayo ni part of African Democracy.

Swali la msingi ni Watanzania wanataka nini kati ya demokrasia na maendeleo?. Watanzania wanataka maendeleo, na maendeleo hayana chama, hivyo rais Magufuli analeta maendeleo kupitia mwelekeo wa chama kimoja, kazi imeanza leo kwenye huu uchaguzi wa serikali za mitaa na kukamilika mwakani katika uchaguzi Mkuu kwa Tanzania kurejea kuwa nchi ya chama kimoja, tukiisha pata maendeleo ndipo tutaigeukia demokrasia.

P
Ficha ujinga wako pasko demokrasia na maendeleo ni inseparable
 
Tanzania Tunafuata Tanzanian Democracy model ambayo ni part of African Democracy.

Swali la msingi ni Watanzania wanataka nini kati ya demokrasia na maendeleo?. Watanzania wanataka maendeleo, na maendeleo hayana chama, hivyo rais Magufuli analeta maendeleo kupitia mwelekeo wa chama kimoja, kazi imeanza leo kwenye huu uchaguzi wa serikali za mitaa na kukamilika mwakani katika uchaguzi Mkuu kwa Tanzania kurejea kuwa nchi ya chama kimoja, tukiisha pata maendeleo ndipo tutaigeukia demokrasia.

P

Pascal, ivi kweli unatuambia tunaweza pata maendeleo bila kuwa na demokrasia? Nitajie nchi moja duniani ambayo haina demokrasia lakini inamaendeleo.
 
Pascal, ivi kweli unatuambia tunaweza pata maendeleo bila kuwa na demokrasia? Nitajie nchi moja duniani ambayo haina demokrasia lakini inamaendeleo.
Nimezitaja hapa

P
 
Tanzania Tunafuata Tanzanian Democracy model ambayo ni part of African Democracy.

Swali la msingi ni Watanzania wanataka nini kati ya demokrasia na maendeleo?. Watanzania wanataka maendeleo, na maendeleo hayana chama, hivyo rais Magufuli analeta maendeleo kupitia mwelekeo wa chama kimoja, kazi imeanza leo kwenye huu uchaguzi wa serikali za mitaa na kukamilika mwakani katika uchaguzi Mkuu kwa Tanzania kurejea kuwa nchi ya chama kimoja, tukiisha pata maendeleo ndipo tutaigeukia demokrasia.

P

Wewe una akili nyingi kuliko Baba wa Taifa ambaye uzoefu wake wa chama kimoja ulimtaka aunge mkono vyama vingi?
 
Duh.. yetu macho..
Tanzania Tunafuata Tanzanian Democracy model ambayo ni part of African Democracy.

Swali la msingi ni Watanzania wanataka nini kati ya demokrasia na maendeleo?. Watanzania wanataka maendeleo, na maendeleo hayana chama, hivyo rais Magufuli analeta maendeleo kupitia mwelekeo wa chama kimoja, kazi imeanza leo kwenye huu uchaguzi wa serikali za mitaa na kukamilika mwakani katika uchaguzi Mkuu kwa Tanzania kurejea kuwa nchi ya chama kimoja, tukiisha pata maendeleo ndipo tutaigeukia demokrasia.

P
 
Tanzania Tunafuata Tanzanian Democracy model ambayo ni part of African Democracy.

Swali la msingi ni Watanzania wanataka nini kati ya demokrasia na maendeleo?. Watanzania wanataka maendeleo, na maendeleo hayana chama, hivyo rais Magufuli analeta maendeleo kupitia mwelekeo wa chama kimoja, kazi imeanza leo kwenye huu uchaguzi wa serikali za mitaa na kukamilika mwakani katika uchaguzi Mkuu kwa Tanzania kurejea kuwa nchi ya chama kimoja, tukiisha pata maendeleo ndipo tutaigeukia demokrasia.

P
Kiukweli yawezekana tuliruka stage moja kabla ya kuingia tuliopo.
Maendeleo kwanza Demokrasia baadae,ingawa hii ni tofauti na ile ya Soviet 1990.
 
Back
Top Bottom