Kuacha kazi kumbe kazi!!

Kuacha kazi kumbe kazi!!

Siku utapofagia nyumba yako usione hata sh mia, mkeo atapokuacha kwa vile huwezi mtunza, watoto watakapokosa chakula n.k ndipo utapogundua kuwa hiyo ajira yako ilikuwa kitu cha thamani kuliko vitu vyote. Usithubutu kuacha kazi kabla channel zako nyingine hazijatiki.
Ni ushauri Mzuri wenye woga ndani yake , maana woga huo nimeshaushinda, nataman maisha hayo ya kusota, nisipumbazike na check no., nahitaj kukanyaga chupa nifikie trophy boss
 
True, si kazi ya kunibana sana, but I want to work to myself 24/7 najua kufeli kupo, kusipokuwepo hakuna success
Huna mkopo wa serikali? Usije fungwa bure,fanya yote ualimu sidhani ni kazi ambayo ipo busy sana kiasi cha kutoweza kufanya mambo yako mengine vinginevyo mazingira yawe sio rafiki kwa mipango yako
 
Mkuu unawazo zuri tena sana. Chamsingi ujitathimini upo kwenye kundi gani kati ya haya, RISK TAKER, RISK AVERSE au RISK NEUTRAL. Kama ni risk taker chukua maamuzi mapema ili utimize kiu yako.
 
Jenga mirija ya fedha yenye uwezo wa kukuweka busy zaidi mpaka ukakosa muda wa kufanya ajira yako. Then acha ajira focus kwenye biashara yako.

Siku zote fanya calculated risks, usiache kazi kwa mihemko ya motivational books. Kwanza ukishaona bado upo kwenye kiu kalii ya kusoma motivational books, ujue bado hujagusa kwenye kuujua ujasiriamali halisi. Mjasiriamali hana hizo motivational books anaona ni kupoteza muda kwa kuwa yeye yuko busy na namna ya kutatua tatizo fulani. Anasaka suluhisho.

Ushauri jenga plan kwanza ( chora pavements A-Z ) na unachoplan hakikisha uwezekano wa kufanikiwa ni zaidi ya 60% then wekeza nguvu hapo, na hakikisha isiwe ni biashara zilizozoeleka kama banda la chipsi, duka, baa, grocery, kulima tikiti, daladala etc

Hope it helps !


Mkuu taja mfano wa biashara sizizo zoeleka kwanza.
 
Huwezi kuacha kazi bila plans.
Kama unampango wa kufanya biashara uwe umeshaianza
Kama ni kilimo na ufugaji uwe na shamba angalau na mbuzi wanne
Shamba una kibanda chenye vyumba angalau viwili sebule jiko na choo
Uhakika wa maji
Mengine yatafuata.
Wanasema "acha Kazi uone ilivyo kazi kupata kazi "
 
Kwa kipindi fulani Inabidi ushike mawili, japo hupendi. Amua nini unataka kufanya mbadala wa kufundisha, na uanze kulifanyia kazi ilhali ungali mwalimu, ili ujue muelekeo, je kuna tija, utamudu? Kutokana na matokeo, utaamua kama uache kazi, ufanye jaribio la suala jingine au uendelee na ualimu. Usiache kazi kabla ya kupata uhakika wa shughuli mbadala.
 
Wakuu heshima yenu. Katika kipindi cha miezi 9 mfululizo nimekua Dilemma kwa kile ninachokiita kushindwa KUACHA kazi. Nakua katika stress, hasa nikianza kuwasikia wazazi wakirap nikigusia suala hilo. Nimeajiriwa serikalini kama mwalimu. Sina shida yoyote kazini, ila nahisi kama muda wangu Wa kuitumikia serikali umetosha na ninatamani sasa kuishi maisha magumu yenye Uhuru ambapo naamini nitauona ubunifu wangu Wa fursa, sipendi kuwa average man, nataka kufikia malengo yangu mengine ambayo hayahusiani na taaluma.

Sikujua kama KUACHA kazi Nako ni kazi. Marafiki, waajiri, wazazi, ndugu, wamekua kikwazi kwa kunipa woga Wa hali ya juu, basi mim hata sina hofu, napenda kuishi hayo maisha wanayoyahofu. Huwa najisikia vibaya sana nikionywa kutoacha kazi, kazi yenyewe sasa nashindwa kuitekeleza vema kwa kuwa nimesha loose interest nayo, sitaki kufukuzwa nataka kuacha, Nimefanya kazi kwa miaka takribani 6, nahisi Nina call nyingine, huwa napenda sana Uhuru, ubunifu na kuthubutu.

Note:
Ukiwa mtumishi unakuwa secured kwa bima ya afya nk, hili ndilo wanalonitisha hasa, ukichanganya na wimbi la vijana mitaani walokosa ajira.

Nina familia, Je, inaweza kuwa kikwazo kwa mipango yangu?

Japo ninasoma sana vitabu, hasa motivational books, pia Business Books ila napima na mazingira halisi niliyopo,
Sio vitabu vinavyonichichea, ila call ndo inanichochea kusoma vitabu hivyo ili kugain more knowledge with confidence.

Nadhani GT watakuwa wananielewa zaidi ya nifikiriavyo.

Lengo langu sitaki kushika mawili. Na nimaamini katika kile nikipendacho kwa sasa.

Long story short, nisaidieni kimawazo.

Angalizi: We teachers and other servants are too coward with inferiority ya future challenge. Msinitishe nipeni strong thoughts.

Samahani kama kuna lugha Kali.
Maswali, ushauri,critics, mapendekezo ya maandiko, videos, quotes, welcome.
Asanteni.

TZ1
Jilipue tu Mwalimu wangu, Mazingira kama ya Dodoma hayo mfano hata kilimo ni shida,
Tafta chimbo ulime au ufuge kuku.
Ila kama hujawai jaribu miradi kama hii ni mtihani kwani unaweza poteza kila kitu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom