Kuacha kazi kumbe kazi!!

Kuacha kazi kumbe kazi!!

Kama unafamilia usikurupuke kuacha tu ghafla, jijenge, weka miradi kadhaa ambayo itakusukuma kukupatia chochote kwa ajili ya familia yako na hakikisha umesimama vyema ndio uache

Mtaani ni kugum hasa ukiwa huna kazi au chochote cha kukuingizia pesa mkuu na wewe una familia usijeitesa bure familia yako jipange ukiacha unakua umechange tu direction hata hiyo miradi aweza simamia mkeo kw auangalizi wako ukaendelea na hiko unachokitaka kukifanya kwa uhuru.
Sikurupuki Mkuu, nilipewa mawazo ya kujipanga hapa jf nadhani mwaka jana, nikafanya hivyo, sasa kutekeleza kuacha kazi ndo kaz mkuu
 
Mtoa Mada
Una Wazo jema.
Kuajiriwa ni utumwa.

Nakushauri tafuta mradi ukiwa kazini
Ukisimama kiasi then ACHA KAZI YA UALIMU.

Kuna kipindi nimekiona TBC majuzi wiki hii cha SHAMBANI kilimwonyesha MAMA mmoja aliacha kazi Serikalini na kujikita kwenye KILIMO CHA MBOGA MBOGA kisichotumia Udongo

Baada ya maelezo yake yote ali niispire SANA

Analima mboga mboga nyingi kwa eneo dogo kwa gharama nafuu
Anauza kwenye supermarket na sehem mbalimbali hadi anazidiwa na order za wateja.

Nakushauri tafuta mradi au MTAJI kwanza
Pili shirikisha family kwa maana ya Mke na watoto wako.

Ndugu wengine watakupoteza
Asante mkuu, naendlea kuwasikiliza..
 
Wakuu heshima yenu. Katika kipindi cha miezi 9 mfululizo nimekua Dilemma kwa kile ninachokiita kushindwa KUACHA kazi. Nakua katika stress, hasa nikianza kuwasikia wazazi wakirap nikigusia suala hilo. Nimeajiriwa serikalini kama mwalimu. Sina shida yoyote kazini, ila nahisi kama muda wangu Wa kuitumikia serikali umetosha na ninatamani sasa kuishi maisha magumu yenye Uhuru ambapo naamini nitauona ubunifu wangu Wa fursa, sipendi kuwa average man, nataka kufikia malengo yangu mengine ambayo hayahusiani na taaluma. Sikujua kama KUACHA kazi Nako ni kazi. Marafiki, waajiri, wazazi, ndugu, wamekua kikwazi kwa kunipa woga Wa hali ya juu, basi mim hata sina hofu, napenda kuishi hayo maisha wanayoyahofu. Huwa najisikia vibaya sana nikionywa kutoacha kazi, kazi yenyewe sasa nashindwa kuitekeleza vema kwa kuwa nimesha loose interest nayo, sitaki kufukuzwa nataka kuacha, Nimefanya kazi kwa miaka takribani 6, nahisi Nina call nyingine, huwa napenda sana Uhuru, ubunifu na kuthubutu.

Note:
Ukiwa mtumishi unakuwa secured kwa bima ya afya nk, hili ndilo wanalonitisha hasa, ukichanganya na wimbi la vijana mitaani walokosa ajira.

Nina familia, Je, inaweza kuwa kikwazo kwa mipango yangu?

Japo ninasoma sana vitabu, hasa motivational books, pia Business Books ila napima na mazingira halisi niliyopo,
Sio vitabu vinavyonichichea, ila call ndo inanichochea kusoma vitabu hivyo ili kugain more knowledge with confidence.

Nadhani GT watakuwa wananielewa zaidi ya nifikiriavyo.

Lengo langu sitaki kushika mawili. Na nimaamini katika kile nikipendacho kwa sasa.

Long story short, nisaidieni kimawazo.

Angalizi: We teachers and other servants are too coward with inferiority ya future challenge. Msinitishe nipeni strong thoughts.

Samahani kama kuna lugha Kali.
Maswali, ushauri,critics, mapendekezo ya maandiko, videos, quotes, welcome.
Asanteni.

TZ1
Usithubutu Kuacha kazi for the fun of it....It will not be once you are done but PM if you realy want to
 
Jenga mirija ya fedha yenye uwezo wa kukuweka busy zaidi mpaka ukakosa muda wa kufanya ajira yako. Then acha ajira focus kwenye biashara yako.

Siku zote fanya calculated risks, usiache kazi kwa mihemko ya motivational books. Kwanza ukishaona bado upo kwenye kiu kalii ya kusoma motivational books, ujue bado hujagusa kwenye kuujua ujasiriamali halisi. Mjasiriamali hana hizo motivational books anaona ni kupoteza muda kwa kuwa yeye yuko busy na namna ya kutatua tatizo fulani. Anasaka suluhisho.

Ushauri jenga plan kwanza ( chora pavements A-Z ) na unachoplan hakikisha uwezekano wa kufanikiwa ni zaidi ya 60% then wekeza nguvu hapo, na hakikisha isiwe ni biashara zilizozoeleka kama banda la chipsi, duka, baa, grocery, kulima tikiti, daladala etc

Hope it helps !
Msaada mkubwa sana Mkuu, kuhusu motivational books nimsomaji, ila nimesema naangalia na mazingira halisi, na Hamna kitu nakwepa ka mihemko, ni miezi Tisa sasa nipo kwenye mizani yangu kuyapima mambo, c jambo dogo,, asante,
 
Jenga mirija ya fedha yenye uwezo wa kukuweka busy zaidi mpaka ukakosa muda wa kufanya ajira yako. Then acha ajira focus kwenye biashara yako.

Siku zote fanya calculated risks, usiache kazi kwa mihemko ya motivational books. Kwanza ukishaona bado upo kwenye kiu kalii ya kusoma motivational books, ujue bado hujagusa kwenye kuujua ujasiriamali halisi. Mjasiriamali hana hizo motivational books anaona ni kupoteza muda kwa kuwa yeye yuko busy na namna ya kutatua tatizo fulani. Anasaka suluhisho.

Ushauri jenga plan kwanza ( chora pavements A-Z ) na unachoplan hakikisha uwezekano wa kufanikiwa ni zaidi ya 60% then wekeza nguvu hapo, na hakikisha isiwe ni biashara zilizozoeleka kama banda la chipsi, duka, baa, grocery, kulima tikiti, daladala etc

Hope it helps !
Brother ushauri wako nimeukubali,mtoa mada zingatia hili.
 
Sikurupuki Mkuu, nilipewa mawazo ya kujipanga hapa jf nadhani mwaka jana, nikafanya hivyo, sasa kutekeleza kuacha kazi ndo kaz mkuu
kama umejipanga then go ahead kuna muda unatakiwa kusimamia unachoamini na kuupa moyo furaha
 
Siku utapofagia nyumba yako usione hata sh mia, mkeo atapokuacha kwa vile huwezi mtunza, watoto watakapokosa chakula n.k ndipo utapogundua kuwa hiyo ajira yako ilikuwa kitu cha thamani kuliko vitu vyote. Usithubutu kuacha kazi kabla channel zako nyingine hazijatiki.
 
Huna mkopo wa serikali? Usije fungwa bure,fanya yote ualimu sidhani ni kazi ambayo ipo busy sana kiasi cha kutoweza kufanya mambo yako mengine vinginevyo mazingira yawe sio rafiki kwa mipango yako
 
Kuna maamuzi hutakiwi kumshirikisha hata mwenzi wako maana tuna maono tofauti.Unajipanga halafu unaacha.

Ukifungua mdomo wako tu ndo mwanzo wa kuletewa hadithi za kalumakenge halafu wanakufuatilia.
Hapa nimejifunza kitu Mkuu, asante.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom