Kuacha kazi kumbe kazi!!

Kuacha kazi kumbe kazi!!

Bado hujafanya maamuzi,Kwa Jinsi ulivyoandika hapa Bandiko lako Usithubutu kuacha kazi Utaangukia pua.
 
Usidhubutu kuacha KAZI ndugu zingatia hili utakayokutana nayo duniani hutaamini kama ulitumia akili zako kuaza kuacha kazi
 
Wakuu heshima yenu. Katika kipindi cha miezi 9 mfululizo nimekua Dilemma kwa kile ninachokiita kushindwa KUACHA kazi. Nakua katika stress, hasa nikianza kuwasikia wazazi wakirap nikigusia suala hilo. Nimeajiriwa serikalini kama mwalimu. Sina shida yoyote kazini, ila nahisi kama muda wangu Wa kuitumikia serikali umetosha na ninatamani sasa kuishi maisha magumu yenye Uhuru ambapo naamini nitauona ubunifu wangu Wa fursa, sipendi kuwa average man, nataka kufikia malengo yangu mengine ambayo hayahusiani na taaluma.

Sikujua kama KUACHA kazi Nako ni kazi. Marafiki, waajiri, wazazi, ndugu, wamekua kikwazi kwa kunipa woga Wa hali ya juu, basi mim hata sina hofu, napenda kuishi hayo maisha wanayoyahofu. Huwa najisikia vibaya sana nikionywa kutoacha kazi, kazi yenyewe sasa nashindwa kuitekeleza vema kwa kuwa nimesha loose interest nayo, sitaki kufukuzwa nataka kuacha, Nimefanya kazi kwa miaka takribani 6, nahisi Nina call nyingine, huwa napenda sana Uhuru, ubunifu na kuthubutu.

Note:
Ukiwa mtumishi unakuwa secured kwa bima ya afya nk, hili ndilo wanalonitisha hasa, ukichanganya na wimbi la vijana mitaani walokosa ajira.

Nina familia, Je, inaweza kuwa kikwazo kwa mipango yangu?

Japo ninasoma sana vitabu, hasa motivational books, pia Business Books ila napima na mazingira halisi niliyopo,
Sio vitabu vinavyonichichea, ila call ndo inanichochea kusoma vitabu hivyo ili kugain more knowledge with confidence.

Nadhani GT watakuwa wananielewa zaidi ya nifikiriavyo.

Lengo langu sitaki kushika mawili. Na nimaamini katika kile nikipendacho kwa sasa.

Long story short, nisaidieni kimawazo.

Angalizi: We teachers and other servants are too coward with inferiority ya future challenge. Msinitishe nipeni strong thoughts.

Samahani kama kuna lugha Kali.
Maswali, ushauri,critics, mapendekezo ya maandiko, videos, quotes, welcome.
Asanteni.

TZ1
Namshukuru Mungu niko hatua za mwisho kabisa na mimi kuacha ya serikakini. Ulicho kiandika kina ukweli kwa 100%!! Vitisho ni vingi sana kutoka kwa wazazi, wana familia, work mates! Nina miaka 15 sasa kazini, lakini niko hoi! Nimechoka mpaka nimepitiliza.

Ila naamini kinachotakiwa ni kufanya tu maamuzi magumu na ambayo hutokuja kuyajutia. Kiukweli kazi ya kuajiriwa inachosha sana. Muda mwingi unatumikishwa, kwa malipo kiduchu mwisho wa mwezi! Unatishwa, unaendeshwa kama gari bovu! Halafu unajiona kama una uwezo vile wa kufanya mambo makubwa zaidi nje ya mfumo wa ajira!

Binafsi naona kujiajiri ni bora zaidi ya kuajiriwa. Tuwaachie wale wenzangu na mimi (waoga) ambao siku zote huamini hakuna maisha nje ya ajira.

NB: Muhimu ni maandalizi tu. Ukikurupuka kuacha pasipo kujiandaa, umekwisha.
 
Bado hujafanya maamuzi,Kwa Jinsi ulivyoandika hapa Bandiko lako Usithubutu kuacha kazi Utaangukia pua.
Urudi utujibu bas
Kwa niaba yake, naomba mnitafute mwezi wa 12 mwaka huu ili niwape mrejesho. Nimeamua kuacha baada ya kuona ninazeeka kabla ya wakati.

Nina biashara ina mwaka 1 na nusu sasa. Inaendelea vizuri. Ni bora niwekeze nguvu huko, kuliko kwenye ajira iliyojaa stress na majungu.

Ahueni familia, jamaa na marafiki wamenielewa baada ya miezi kadhaa ya msuguano. Mungu yupo, naamini nitavuka salama kwenye kipindi cha mpito. Haya maamuzi yametoka moyoni!

Siku zote uoga wako, ndiyo umaskini wako. Siyo lazima wote tuajiriwe. Munvu na atubariki woye wenye mawazo ya aina hii ya kujilipua. No way out. Maisha lazima yaendelee.
 
Hakika mwenyewe nataka kujilipua mkuu
 
Hakika mwenyewe nataka kujilipua mkuu
Mimi kiukweli siyo mshabiki wa Magufuli. Ila kwa ile miaka ya utawala wake, aliniongezea sana ujasiri. Maana niliishi kwa mshahara mdogo mpaka basi.

Imagine nilikuwa na mkopo benki! Ilipofika 2016 makato ya Bodi ya mikopo yakaongezeka mara dufu! Hapo hakuna cha kupanda daraja, wala kuongezewa mshahara!

Hakika zile stress zilinitoa kabisa katika mstari. Mungu yupo. Tutashinda tu. Wenye moyo waendelee kulitumikia Taifa kwa uadilifu na uaminifu mkubwa. Na sisi wenye mioyo myepesi, wacha tukalipambanie Taifa letu, kwa namna nyingine.
 
Mimi kiukweli siyo mshabiki wa Magufuli. Ila kwa ile miaka ya utawala wake, aliniongezea sana ujasiri. Maana nikiishi kwa mshahara mdogo mpaka basi.

Imagine nilikuwa na mkopo benki! Ilipofika 2016 kamato ya Bodi ya mikopo yakaongezeka mara dufu! Hapo hakuna cha kupanda daraja, wala kuongezewa mshahara!

Hakika zile stress zilinitoa kabisa katika mstari. Mungu yupo. Tutashinda tu. Wenye moyo waendelee kulitumikia Taifa kwa uadilifu na uaminifu mkubwa. Na sisi wenye mioyo myepesi, wacha tukalipambanie Taifa letu, kwa namna nyingine.
Yap..no way out ni kukomaa tu
 
Me too nimeanza huo mpango ila mimi nimejikita kwenye ufugaji aise mambo yanakwenda vizuri kibanda nacho , hii ajira ya gvt nimeplan nikifunga 10yrs kwaheri sasa na 7yrs bado mitatu nipige mkopo mrefu nisepe zangu nikatanue zaidi miradi yangu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom