KP - mchokozi...ha ha haa



Huu ni utani wa nguvu. Naona mzee kajitahidi kapata herufi mbili, ila hii ya tatu inamsubua sana. Nadhani hizi mbili alizipanga mwanzoni mwa uongozi wake, ila hii ya tatu anaipanga mwishoni wakati anaelekea kwenye uchaguzi. Mwanzoni wana ccm walikuwa pamoja ila sasa naona wameanza kusambaratika kwa sababu ya ufisadi, ndo maana inakuwa vigumu kuunganisha herufi ya mwisho. Aombe msaada.
 
Na pia yawezekana baadhi ya vipande anavyohitaji kumalizia kuunganisha herufi ya mwisho vimepotea; mfano kupendwa kwake na wana CCM alipoingia madarakani na hivi sasa haviko kwenye level moja!
 
Pia inawezekana yeye kaikuta puzzle imeshapangwa vizuri mezani akaivuruga sasa anahaha kuirudisha kabla hajagundulika (kama mtoto vile!!!!)

Leo kuna mtu ataitwa ofisini kwa Tido Mhando. Na hivi kuna mkakati wakuzuia wafanyakazi wa serikali wasiwe na shughuli za pembeni!! (rejea thread ya Madaktari kuzuiwa kufanya kazi Private)
 
KP yuko matawi ya viponzo vyake vyafurahisha sana pia ni lishe ya kufikiri,kwa hakika KP namfananisha na Mtanzania tena wa kabila langu aliyeikimbia Tanzania na kuamua kuwa Mkikuyu ndugu Gaddo wa Daily Nation pale kwa Kibaki,bravo bro KP
 
Ila JK anamchora vizuuri sijui kwanini, angekuwa Sitta au Mkapa yangechorwa madumbwana maaakuuubwa ya ajabu!!! sijui bwana labda ni hisia zangu tu.....ila nahisi anamapenzi nae sana....
 
Inawezekana hizo mbili kapatia maana hiyo ya mwisho.......je "M"au "J"???Je kama ccj wameishachukua baadhi yavipande je hiyo M itakamilika????Hapatoshi big up KP!
 
J would fit better on that gap than M:A S tongue:

J won't fit at all. CC stands for we[sisi]. M stands for Mtandao. How can he dare to work with mtandao while he is the chairperson of CCM and have already descrimate the rest by forming Sisi ( baba,mama, watoto plus friends and their sons/daughter)? If he puts Mtandao instead of Mapinduzi, the party is not secure at all. Can he put M and claiming to stand for mapinduzi?

Then, he is thinking......
 
Na pia yawezekana baadhi ya vipande anavyohitaji kumalizia kuunganisha herufi ya mwisho vimepotea; mfano kupendwa kwake na wana CCM alipoingia madarakani na hivi sasa haviko kwenye level moja!
..Kweli kabisa maana ukiangalia hata hivyo vipande vilivyobaki hawezi kukamilisha herufi ya mwisho...Ni kamtihani kwa muungwana!! I like this!!:A S-eek:
 
Ila JK anamchora vizuuri sijui kwanini, angekuwa Sitta au Mkapa yangechorwa madumbwana maaakuuubwa ya ajabu!!! sijui bwana labda ni hisia zangu tu.....ila nahisi anamapenzi nae sana....
...MI huwa ananimaliza anampomchora BM kazi inakuwa kwenye miguu eeh! Jamaa juu mkubwa kama nyumba chini vimiguu vidogooo utadhani penseli....
 
Kazi kweli kweli! Kunvunja ni rahisi kuliko kujenga. Ila kufanya ukarabati ni vigumu zaidi kama mtu siyo mjanja!
 
Kuna Huyu mheshimiwa anaitwa Sammy alikua akichorea majira enzi za 90..naona usanii wao unafanana..
Ni bora kufundishana kuvua samaki...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom