Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,162
Kwa statement hiyo aliyotoa kamanda Kova, yapo maswali mengi, wananchi tunapaswa kumuuliza.Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleimani Kova, amedai kuwa kutekwa na kuumizwa vibaya kwa Mwandishi nguli na Mhariri wa New Habari,Absalom Kibanda, si tukio la kihalifu. Kamanda Kova amedai kuwa tukio hilo limetokana na chuki na kulipiziana visasi.
Hii ni kwasababu waliomteka na kumshambulia Kibanda hawakuchukua kitu chochote toka kwake. Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoa taarifa za uchunguzi wa awali wa jeshi la polisi juu ya tukiohilo lililotokea jana,
Kwahiyo kutekwa na kushambuliwa si uhalifu? Nani anaweza kumwamini Kova aliyewahi 'kuwasha' sinema ya Dr.Ulimboka na anayeshindwa kuizima hadi sasa?
Swali la kwanza, akiwa Polisi wa ngazi za juu kabisa, anawezaje kukiita kitendo cha unyama wa kutisha aliofanyiwa Kibanda kuwa si cha kihalifu, wakati Kibanda ameumizwa sana na watu waliomshambulia, na Kibanda mwenyewe anaeleza kuwa alimsikia mmoja wa hao watu, akiuliza, afande vipi tumshuti ili tummalizie?
Swali la pili, akiwa Polisi wa ngazi za juu kabisa, anawezaje kuhitimisha, kwa kusema kuwa kitendo alichofanyiwa Kibanda ni cha chuki na cha kulipizana kisasi,wakati hata uchunguzi wenyewe haujaanza?!
Hivi kwa mazingira hayo, serikali hii inategemea kweli tuliamini Jeshi letu la Polisi, ambao jukumu lao kubwa ni kulinda Raia na mali zao, wakati kuna matukio ya nyuma, kama lile la kutekwa na kuteswa,alikofanyiwa Dr Ulimboka na kuuawa kwa mwandishi Mwangosi, Jeshi hilo halionyeshi juhudi zozote za kuwatia mbaroni, vinara wa vitendo hivyo vya kihalifu?!
Kwa mazingira ya nchi hii yanavyokwenda kwa sasa, hayana tofauti sana na vitendo vilivyokuwa vinafanywa na Idi Amin, ambaye kazi yake kubwa ilikuwa kumnyamazisha kwa kumdhuru yeyote yule anayepinga serikaliyake!!