Kova: Kutekwa kwa Kibanda si tukio la kihalifu!

Waandishi wa habari wanatakiwa kutusaidia kwa kuwabana hawa viongozi na kauli zao za ajabu. Maana ya ualifu ni nini Kama kutekwa, kusulibiwa au kuchukua sheria mkononi si ualifu! Pia waandishi kila siku wanakubali kuigwa na kuelezwa uundwaji wa kamati au timu za upelelezi na maneno makali kila litokeapo tukio lakini matokeo ya uchunguzi hawaitwi kuelezwa. Kwa nini wasimuulize?

Vipi mkuu hujui kabla ya kuwageuka waandishi hawa hawa walinunuliwa? Waandishi wenyewe wamegawanyika na makanjanja ndio wameshika hatamu. Subiri uone. Wengi wao wamehasiwa akili zao. Kama uongo waone wale wanaokula na kulala kwa kodi zetu.

Dhambi hii haiwabakizi ngo
 
Hivi hawa wahariri huwa hawachukui hata mafunzo ya ujasusi walau kidogo tu?

Unaandika uoza wa magaidi wa CCM wakati machale ya Willy Gamba hata robo huna?
 
Subhanaallah! Huyu Nae alienda kufanya nini MACCA na MADINA....Kutalii au kuhiji? ipo siku waliopewa nyadhifa watakapo oneshwa na Mola wao yale waliyokua wakiyafanya na apo ndipo watakapojuta kua VYEO ni DHAMANA
 
Kova anaongea km 'layman' wa mambo ya usalama wa raia, nina hofu na taaluma yake.
 
Naona Kova anajiandaa kutoa movie nyingine sasa. Huu ni upuuzi sana, intelejensia ya polisi wetu ni weak sana.
 
Kova anaongea km 'layman' wa mambo ya usalama wa raia, nina hofu na taaluma yake.

Je alijkuwa amelewa' au amevuta bangi? Hususani klupita kiasi. Hata maana ya 'uhalifu' akaisahau.
Yote kwa yote, Kova ni kiungo kikuu dhidi ya unyang'anyi na udhalimu mkuu.
 
Yan mpaka huyu ------ aondoke pale Magogoni tutaona na kusikia kila la kustaajabisha, kuogofya na kusononesha..
 
Wasimkamate wa msumbiji... heri wamkamate mmalawi harafu waseme ilikuwa ni mambo ya lake malawi.... aka nyasa
 
Kova naye sasa nadhani anazeeka vibaya,mtu ameumizwa yeye anasema huo siyo uhalifu(siyo tukio la kihalifu).Kwani uhalifu ni nini? mtu akilipiza kisasi na kusababisha majeraha kwa mtu mwengine huo siyo uhalifu? kama siyo uhalifu,mbona jeshi la polisi limechukua hatua?,hebu kova atupe fasili ya uhalifu.:-*







Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleimani Kova, amedai kuwa kutekwa na kuumizwa vibaya kwa Mwandishi nguli na Mhariri wa New Habari,Absalom Kibanda, si tukio la kihalifu. Kamanda Kova amedai kuwa tukio hilo limetokana na chuki na kulipiziana visasi.

Hii ni kwasababu waliomteka na kumshambulia Kibanda hawakuchukua kitu chochote toka kwake. Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoa taarifa za uchunguzi wa awali wa jeshi la polisi juu ya tukiohilo lililotokea jana,

Kwahiyo kutekwa na kushambuliwa si uhalifu? Nani anaweza kumwamini Kova aliyewahi 'kuwasha' sinema ya Dr.Ulimboka na anayeshindwa kuizima hadi sasa?
 
Kamanda Kova, wapi yule mtuhumiwa wa Ulimboka, ulimtangaza kwa mbwe mbwe nyiiingi. Haya sasa tuletee mwingine. Tatizo jamaa anapenda kufanya kazi mbele ya Camera.
 
Kwa hiyo ina maana watu wakimdhuru mtu kwa silaha kwa nia ya kulipiza kisasi si uhalifu!

Hii Kali kweli, Au Polisi hawajui sheria!
 
Machademu wauaji hahaha mbinu zenu kwisha gundulika ngoja KIBANDA aje amuanike Dj aliyezungusha form 4
 
Mh! Kwa hiyo kulipiza kisasi sii uhalifu? Kuchukua sheria mkononi ni sawa? Mungu tunusuru!
 
Ila kwa kauli hii inaonekana Polisi wameshakamilisha uchunguzi kwa hiyo Afande atatuambia kina nani wamelipiza kisasi na kwa mizengwe ipi iliyopelekea alipiziwe kisasi
 
Tena Kibanda mwenyewe anaeleza kuwa alimsikia mmojawao akiuliza, vipi afande tumshuti? Ukweli huyo jamaa, ni Mungu aliyemuokoa kimuujiza,kwa kuwa huyo jamaa alipojaribu kufyatua trigger,ikagoma!

Hili tukio halina tofauti kabisa na tukio la Ulimboka,kwa hiyo upo uwezekano mkubwa kuwa State organs, zinahusika kikamilifu na tukio hili, kwa hiyo isingekuwa busara hata kidogo, kwa Jeshi hilo la polisi ndiyo liunde Tume, wakati mazingira yanaonyesha, wao ni miongoni ya watuhumiwa wakuu wa tukio hilo!

State Organs nazo ni dhaifu kiasi ktk matukio mawili bado wameshindwa kuteeleza azma yao so kama wananchi tukiamua hawa hakuna kitu kbisa hawamalizi hata 24hrs..si umeona lindi...si uliona mbeya?
 
Ajabu kakimbilia media na majibu haraka haraka. Anaficha nini? Kusema si uhalifu maana yake nini? Hata kama ni visasi ndiyo ni halali kumfanya mtu hivyo? Kama sivyo kumbe anajua waliomlipiza kisasi Kibanda. Kakamata wangapi hadi sasa?
 
Back
Top Bottom