TLS: Tukio la kutekwa na kutoweka kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji

Oct 15, 2018
17
153
TAMKO KWA VYOMBO VYA HABARI

KUHUSU TUKIO LA KUTEKWA NA KUTOWEKA KWA MFANYABIASHARA MOHAMED DEWJI


Ikiwa ni siku ya saba (7) tangu kutekwa na kutoweka kwa mfanyabiashara ambae pia ni mbunge wa zamani wa Singida Mjini ndugu yetu Mohamed Dewji maarufu kama Mo;

Chama cha Mawakili wa Kujitegemea Tanganyika, Tanganyika Law Society (TLS) kinaungana na watanzania wote kulaani kitendo cha kutekwa na kutoweka kwa ndugu zetu miongoni mwao akiwemo Ben Saanane, Azory Gwanda, Ibrahim Musa alias Roma Mkatoliki, Awadh Mtezo alias Moni Central zone, na Simon Kanguye, Samson Josiah, Beuty Yolanda, Idrisa Ally, Rehema Juma, Mfanyabiashara na mmiliki wa mabasi ya kampuni ya Super Sami ndugu Samsoni Josiah na Mo Dewji. Miongoni mwa majina tajwa hapo juu walipatikana na kukiri kuteswa na watekaji baada ya kuachiwa huru na wengine hawajapatikana mpaka leo na taarifa zao hakuna.

TLS inaungana na familia za ndugu zetu hao na watanzania wote na tunachukua fursa hii kuikumbusha jamii, Serikali yetu na vyombo vyetu vya usalama kwamba Tanzania ni nchi huru kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 kama ilivyorekebishwa. Ibara ya 14 ya Katiba inatambua haki yetu kama wananchi ya kuishi na kupata hifadhi ya maisha yetu. Aidha ibara ya 15 inatambua umuhimu wa kuwa na uhuru wa kwenda mahali popote bila kizuizi chochote. Tunapotafakari kutekwa na kutoweka kwa ndugu zetu hao tuliowataja bila ya kuwasahau wengine, tunaangalia hivi vitendo kama uvunjwaji mkubwa wa haki za msingi za ndugu zetu.

Matukio ya utekaji yanayoripotiwa mara kwa mara ni kielelezo kwamba usalama wa raia nchini si wa kuridhisha.

Hivyo basi TLS tunatoa wito kwa vyombo vya usalama kuendeleza jitihada za kuwatafuta ndugu zetu hao waliotekwa na wengine kutoweka hadi sasa. Pia tunaomba vyombo vinavyohusika na ulinzi na usalama wa raia vihakikishe watekaji wametiwa nguvuni na wafikishwe mahakamani haraka iwezekanavyo.

Tunaitaka Serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama kuimarisha ulinzi wa raia wake kwa ustawi bora wa taifa lenye amani.

Wakili: FatmaKarume
Rais-Tanganyika Law Society




IMG-20181018-WA0043.jpg
 
Hilo tamko linalingana kabisa na aliyosema Godbless Lema kwa kila kitu.Ni tamko ambalo linaonekana wazi limeandaliwa na CHADEMA likapelekwa TLS ili Fatuma Karume atie sahihi na kulipeleka vypmbo vya habari

Walitekwa niwalewale, waliopatikana niwalewale, wasio patikana ni walewale, vyombo vinavyohusika kishughulikia tatizo hili ni vilevile. Labda kunawalio jiteka kwenye list
 
Ooh ! Inasikitisha sanaa. Eeeeeh Mola sikia vilio vyetu hivi. Tuokoe na Fariji watu wako. Mioyo yetu inakulilia Mungu mwenye uwezo Mkubwa kuliko wao watekao na watesao.
 
tls wanaandika kwa kikwetu Kiswahili, kweli mabadiliko siyo kama yule mkurya Tundu Lisu aliyepita alikuwa anajifanya ni Kiingereza tu wakati kiingereza chenyewe hakijui, grammatic errors kibao!

Hongereni tls kwa kuandika kikwetu!
 
Mbona wamekopi aliyo yasema Lema? hili ni tawi la chadema?
Haijalishi ila angalau wamekemea, Mbona Chama Cha Mauaji hakijatoa tamko lolote....Naona bado wanatafakari ni jinsi gani watazichukua Mali za Mo, Na mtakunya mwaka huu, Misaada hakuna , mikopo ndo mmekopa paka hamkopesheki tena, sasa mmeamua kuanza kudhulumu mali za wananchi kwa nguvu.

Za mlianza na manji, mkaenda kwa wengine , sasa mmekuja kwa mo.

Kila kukicha mnabuni mbinu za kukwarua hela za wananchi, mmeanzisha chanzo kipya cha mapato cha faini za barabarani ambapo mnawabambika wananchi makosa ya uongo ili tu mpate hela.

Pesa za wakulima wa korosho mmechukua, paka rambirambi za wafiwa mnachukua hata haya hamuoni.

Na bado, naona namba mnaisoma wenyewe.

Pumbavu zenu.
 
Back
Top Bottom