Kova: Kutekwa kwa Kibanda si tukio la kihalifu!

Hii ya afande mshuti inaonekana kama bosi alikuwa anapokea amri ya mtu wa chini yake. Very confusing.
 
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleimani Kova, amedai kuwa kutekwa na kuumizwa vibaya kwa Mwandishi nguli na Mhariri wa New Habari,Absalom Kibanda, si tukio la kihalifu. Kamanda Kova amedai kuwa tukio hilo limetokana na chuki na kulipiziana visasi.

Hii ni kwasababu waliomteka na kumshambulia Kibanda hawakuchukua kitu chochote toka kwake. Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoa taarifa za uchunguzi wa awali wa jeshi la polisi juu ya tukiohilo lililotokea jana,

Kwahiyo kutekwa na kushambuliwa si uhalifu? Nani anaweza kumwamini Kova aliyewahi 'kuwasha' sinema ya Dr.Ulimboka na anayeshindwa kuizima hadi sasa?

.......

Sawa..ilikuwa ni maombezi!!!
 
Hawa watu wanafikiri wapo Maisha hapo, Mungu atawalipizia 2015, watalia na Kusaga meno, Raila yamemkuta, sasa zamu yao!
 
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleimani Kova, amedai kuwa kutekwa na kuumizwa vibaya kwa Mwandishi nguli na Mhariri wa New Habari,Absalom Kibanda, si tukio la kihalifu. Kamanda Kova amedai kuwa tukio hilo limetokana na chuki na kulipiziana visasi.

Hii ni kwasababu waliomteka na kumshambulia Kibanda hawakuchukua kitu chochote toka kwake. Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoa taarifa za uchunguzi wa awali wa jeshi la polisi juu ya tukiohilo lililotokea jana,

Kwahiyo kutekwa na kushambuliwa si uhalifu? Nani anaweza kumwamini Kova aliyewahi 'kuwasha' sinema ya Dr.Ulimboka na anayeshindwa kuizima hadi sasa?
Kwa maelezo aliyotoa kamanda Kova kuwa kitendo cha kushambuliwa Kibanda kuwa si cha kihalifu, bali ni kitendo cha chuki binafsi na kulipizana kisasi, ni lazima kwa maelezo hayo, kwa kuzingatia sheria ya ushahidi, Kova anapaswa, awe mtu wa kwanza kutoa maelezo hayo, kwa hiyo Tume aliyoiunda, ili atoe clues za kupatikana wahalifu hao, kwa kuwa inaonekana anawafahamu!

Kwa kuwa tayari anajua kuwa kitendo hicho si cha ujambazi, kabla hiyo Tume aliyoiteua haijaanza kazi, maana yake hata hao watu aliodai wamelipiza kisasi kwa Kibanda, mosi, atakuwa anawajua, pili, atakuwa anajua watu hao, kama kweli walikuwa wanalipiza kisasi, walikuwa wamelipiza kisasi kwa kisa gani.

Kama Tume hiyo itashindwa 'kumng'ang'ania' afande Kova na kuanza kumhoji, tutajua Tume hiyo si lolote wala chochote, bali ni usanii mwingine kama Tume nyingine za kipolisi ambazo hadi leo hazijawahi kutoa majibu kwa wananchi.

Nitazitaja baadhi ya Tume hizo za kisanii. Tume iliyoundwa kuchunguza wale askari waliojisevia shilingi milioni 150, mwishoni mwa mwaka jana, katika tukio lililotokea Kariakoo. No. 2, Tume iliyoundwa kuchunguza kisa cha kutekwa kwa Dr Ulimboka. No. 3. Tume iliyoundwa ya kuchunguza tukio la kuuawa kwa mwandishi Mwangosi, ambapo Tume hiyo ilidai kuwa chanzo cha kifo hicho hakijulikani, wakati picha za mauaji ya Mwangosi, zilionyesha waziwazi jinsi wale Polisi waliomzunguka walivyokuwa wanamsulubu kwa kipigo na hatimaye, mmojawao, ndipo akamfyatulia bomu, ambapo ndiye yeye pekee, ambaye Polisi wamelazimika kumfikisha mahakamani kwa shinikizo kubwa la wananchi, hata hivyo Polisi hao wanafanya kila wawezalo ili kumnusuru huyo Polisi mwenzao, kwa kuwa wanajua wazi kuwa, huyo jamaa ametolewa kafara tuu, kwa kuwa alipokuwa analifyatua lile bomu, alikuwa anatekeleza amri aliyokuwa amepewa na bosi wake, kamanda Kamuhanda!!
 
Hivi hawa bongo movie hawahaona kova anafaa kuwa msanii mwenzao eti?

886625_223569727783297_686400968_o.jpg
 
Huyu Kova bila shaka Anaujua Mchezo mzima , na kiukweli Kova atatusaidia sana mahakamani huko mbele ya safari , namtakia maisha marefu sana , Ni shahidi muhimu sana .
 
"Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleimani Kova, amedai kuwa kutekwa na kuumizwa vibaya kwa Mwandishi nguli na Mhariri wa New Habari,Absalom Kibanda, si tukio la kihalifu. Kamanda Kova amedai kuwa tukio hilo limetokana na chuki na kulipiziana visasi".

Kova umefanya uchunguzi au ni hisia ndiyo zinakuongoza?
 
Tuanze kuchambua maana ya uhalifu, uhalifu ni tendo lolote ambalo ni uvunjaji wa sheria. Anaposema kutekwa na kuumizwa kwa Absalom Kibanda si tukio la kihalifu nadhani amekosea ulimini, alitakiwa si tukio la kijambazi. Jambazi huwa analengo la kupora lakini kwa tukio hili haikuwa hivyo. Kwa maana hii tukio linakuwa na definition nyingine lakini ni UHALIFU TU.

Hivi wajameni Kova kasoma mpaka wapi? Make Kova ni taaabu kweli hebu nisaidieni elimu yake kwanza ndipo nitachangia zaidi
 
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleimani Kova, amedai kuwa kutekwa na kuumizwa vibaya kwa Mwandishi nguli na Mhariri wa New Habari,Absalom Kibanda, si tukio la kihalifu. Kamanda Kova amedai kuwa tukio hilo limetokana na chuki na kulipiziana visasi.

Hii ni kwasababu waliomteka na kumshambulia Kibanda hawakuchukua kitu chochote toka kwake. Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoa taarifa za uchunguzi wa awali wa jeshi la polisi juu ya tukiohilo lililotokea jana,

Kwahiyo kutekwa na kushambuliwa si uhalifu? Nani anaweza kumwamini Kova aliyewahi 'kuwasha' sinema ya Dr.Ulimboka na anayeshindwa kuizima hadi sasa?

Tunakumbuka hadi leo video iliyowekwa hewani na kova mwenyewe, ila kwa vile hakuizima na ameona watanzania waliipenda basi ameamua kuwasha PART TWO ya vieo hiyo ya kisa na mkasa wa aina ile ile. Ilikuwa mara kichaa, mara mwehu, mara Mkenya ndo anayehusika.

Hii ni dhahiri ya Serikali halisi tuliyokuwa nayo madarakani. Ninaamini mwonekano wa baba ndo mwonekano wa familia. Uasi, uovu, utekaji, unyanyasaji, udini, visasi, mateso ni sura halisi ya utawala na watawala wa sasa na hakuna haja ya kutofautisha na wao kwa matukio halisi yanayojili.

Inasikitisha na kukera sana mabo ya ajabu haya kutokea.
 
Kova aanze kuwachunguza maafande wake. Mgonjwa amesema alisikia wakiitana 'afande'!!!
 
Sura yake ina makunyazi ya damu za watu wasio na hatia.......wanamlilia Mungu kwa udhalimu wa wapenda vyeo!
 
Back
Top Bottom