Kova: Kutekwa kwa Kibanda si tukio la kihalifu!

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleimani Kova, amedai kuwa kutekwa na kuumizwa vibaya kwa Mwandishi nguli na Mhariri wa New Habari,Absalom Kibanda, si tukio la kihalifu. Kamanda Kova amedai kuwa tukio hilo limetokana na chuki na kulipiziana visasi.

Hii ni kwasababu waliomteka na kumshambulia Kibanda hawakuchukua kitu chochote toka kwake. Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoa taarifa za uchunguzi wa awali wa jeshi la polisi juu ya tukiohilo lililotokea jana,

Kwahiyo kutekwa na kushambuliwa si uhalifu? Nani anaweza kumwamini Kova aliyewahi 'kuwasha' sinema ya Dr.Ulimboka na anayeshindwa kuizima hadi sasa?
Kwa statement hiyo aliyotoa kamanda Kova, yapo maswali mengi, wananchi tunapaswa kumuuliza.

Swali la kwanza, akiwa Polisi wa ngazi za juu kabisa, anawezaje kukiita kitendo cha unyama wa kutisha aliofanyiwa Kibanda kuwa si cha kihalifu, wakati Kibanda ameumizwa sana na watu waliomshambulia, na Kibanda mwenyewe anaeleza kuwa alimsikia mmoja wa hao watu, akiuliza, afande vipi tumshuti ili tummalizie?

Swali la pili, akiwa Polisi wa ngazi za juu kabisa, anawezaje kuhitimisha, kwa kusema kuwa kitendo alichofanyiwa Kibanda ni cha chuki na cha kulipizana kisasi,wakati hata uchunguzi wenyewe haujaanza?!

Hivi kwa mazingira hayo, serikali hii inategemea kweli tuliamini Jeshi letu la Polisi, ambao jukumu lao kubwa ni kulinda Raia na mali zao, wakati kuna matukio ya nyuma, kama lile la kutekwa na kuteswa,alikofanyiwa Dr Ulimboka na kuuawa kwa mwandishi Mwangosi, Jeshi hilo halionyeshi juhudi zozote za kuwatia mbaroni, vinara wa vitendo hivyo vya kihalifu?!

Kwa mazingira ya nchi hii yanavyokwenda kwa sasa, hayana tofauti sana na vitendo vilivyokuwa vinafanywa na Idi Amin, ambaye kazi yake kubwa ilikuwa kumnyamazisha kwa kumdhuru yeyote yule anayepinga serikaliyake!!
 
Kumbe kosa limeshajulikana ni lakulipiza kisasi sasa tume ya kazi gani kuchunguza ni kwenda kukamatwa huyo aliewekeana kisasi maana anajulikana na kamanda kova.
 
Hivi ni kikundi gani kingine kinapractice na koleo za kung'olea meno zaidi ya uwt? Naona vifaa na style iliyotumika inashabihiana na iliyotumika kwa ulimboka. Anataka kusema watz wameshaiga nao wanatumia hivyo ving'olea meno?
Kung'oa meno na kucha ni staili ya UWT.
 
Kamanda Kova amedai kuwa tukio hilo limetokana na chuki na kulipiziana visasi.
Hii ni kwasababu waliomteka na kumshambulia Kibanda hawakuchukua kitu chochote toka kwake.
Naona DCP Kova anatoa sababu za 'layman' hapa, kwa kuwa hawakuchukua chochote basi ni chuki na ulipizaji kisasi .Watesaji nao walitaka Polisi waamini vivyo hivyo.. Naye anataka umma uamini vivyo hivyo.. Idara ya Upelelezi - Kanda Maalum nayo itaamini vivyo hivyo kwa kuwa mkubwa wao kesha sema hivyo.. Halafu sinema inamalizika.Kitakachoendelea ni sawa na kurusha mawe gizani..
 
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleimani Kova, amedai kuwa kutekwa na kuumizwa vibaya kwa Mwandishi nguli na Mhariri wa New Habari,Absalom Kibanda, si tukio la kihalifu. Kamanda Kova amedai kuwa tukio hilo limetokana na chuki na kulipiziana visasi.

Hii ni kwasababu waliomteka na kumshambulia Kibanda hawakuchukua kitu chochote toka kwake. Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoa taarifa za uchunguzi wa awali wa jeshi la polisi juu ya tukiohilo lililotokea jana,

Kwahiyo kutekwa na kushambuliwa si uhalifu? Nani anaweza kumwamini Kova aliyewahi 'kuwasha' sinema ya Dr.Ulimboka na anayeshindwa kuizima hadi sasa?

mtikila.jpg

Matukio ya Mwangosi na sasa Kibanda yananikumbusha mbali mwanaharakati na mwanasiasa mashuhuri nchini kutoa kashfa nzito dhidi ya Mkulu. Mtikila baada ya tuhuma hizo nzito kuzimwaga hadharani serikali ilimburuza mahakamani na kuishia kutoka kidede/kifua mbele huku akiimba "Hallelluya! Bwana asifiwe." Tuhuma zile zilikuwa nzito na kabisa kuelekezwa kwa mkuu wa nchi. Nini nyuma ya pazia, nini kilifanya kesi iishe kiulaini? Kwa maneno mengine Mtikila alikuwa sahihi vinginevyo kushinda kesi kama ile ilikuwa vigumu.

Rais Kikwete hajaonja uchungu wala kuonyesha kusikitikia tukio la Kuuawa Mwangosi na sasa Kibanda. The time will tell.
 
mh. kova naomba ushauri tuanze kuangalia muvi ipi...... mbona unazitoa kwa kasi sana; kuna ndugu yako mmoja nilisoma nae yeye ni meja wa jeshi siku moja pale upana r. house ilikuwa mwaka mpya aliniambia kichwa chako ni kibovu sana sasa nimeanza kuamini.....
 
hivi hawa polisi wa TZ wakoje?hiv kumteka mtu na kumjeruhi vibaya sio tukio la kiualifu?kwahiyo ualifu lazima uhusishe mali,mi nadhani ulinzi wa raia wetu tujaribu kuwapa wanajeshi hawa polisi wameshashindwa kazi.sina imani nao kabisa.
 
Mbona uchunguzi huu umekamilika mapema hivi, mbona zile za Ulimboka, Mwandosi na nyingine nyingi tume bado hazijaleta majibu......Kweli Tanzania ni Tz. This is another wonder of Tz
 
Ili kupindish ukweli, tume aliyounda wakati wa Ulimboka hivi bado haijamaliza kazi!?? kama vipi awaunganishie na hili

Walio husika wakati huu lazima watakuwa raia wa Uganda na ungamo litakuwa kwa Mzee wa Upako Ubungo...Ngoja tusubiri Movie yenyewe hili trela bado halieleweki.
 
Naona DCP Kova anatoa sababu za 'layman' hapa, kwa kuwa hawakuchukua chochote basi ni chuki na ulipizaji kisasi.

Watesaji nao walitaka Polisi waamini vivyo hivyo.. Naye anataka umma uamini vivyo hivyo.. Idara ya Upelelezi - Kanda Maalum nayo itaamini vivyo hivyo kwa kuwa mkubwa wao kesha sema hivyo.. Halafu sinema inamalizika.Kitakachoendelea ni sawa na kurusha mawe gizani..

.......

Hivi wakati wa Ulimboka kuna kitu walichukua? Huyu mzee aache janjawire hata sisi tuna Mungu.
 
hilo sio tukio la kihalifu bana, acheni kumzodoa kamanda wetu manyota.
mtikila.jpg

Matukio ya Mwangosi na sasa Kibanda yananikumbusha mbali mwanaharakati na mwanasiasa mashuhuri nchini kutoa kashfa nzito dhidi ya Mkulu. Mtikila baada ya tuhuma hizo nzito kuzimwaga hadharani serikali ilimburuza mahakamani na kuishia kutoka kidede/kifua mbele huku akiimba "Hallelluya! Bwana asifiwe." Tuhuma zile zilikuwa nzito na kabisa kuelekezwa kwa mkuu wa nchi. Nini nyuma ya pazia, nini kilifanya kesi iishe kiulaini? Kwa maneno mengine Mtikila alikuwa sahihi vinginevyo kushinda kesi kama ile ilikuwa vigumu.

Rais Kikwete hajaonja uchungu wala kuonyesha kusikitikia tukio la Kuuawa Mwangosi na sasa Kibanda. The time will tell.
 
mtikila.jpg

Matukio ya Mwangosi na sasa Kibanda yananikumbusha mbali mwanaharakati na mwanasiasa mashuhuri nchini kutoa kashfa nzito dhidi ya Mkulu. Mtikila baada ya tuhuma hizo nzito kuzimwaga hadharani serikali ilimburuza mahakamani na kuishia kutoka kidede/kifua mbele huku akiimba "Hallelluya! Bwana asifiwe." Tuhuma zile zilikuwa nzito na kabisa kuelekezwa kwa mkuu wa nchi. Nini nyuma ya pazia, nini kilifanya kesi iishe kiulaini? Kwa maneno mengine Mtikila alikuwa sahihi vinginevyo kushinda kesi kama ile ilikuwa vigumu.

Rais Kikwete hajaonja uchungu wala kuonyesha kusikitikia tukio la Kuuawa Mwangosi na sasa Kibanda. The time will tell.
tena kwa kuongezea tu,
hili tukio la Kibanda lingemtokea msanii mwenzake (kama diamond)
JK angekuwa wa kwanza kwenda kumjulia hali hospitalini.
 
Duh!!!Another movie from Kova....mtitu distributors jiandae kusambaza movie hii mpya kutoka kwa bwana kova,safari steling aliyemteka kibanda sijui atakuwa mnyarwanda????
 
Back
Top Bottom