Tukio la kutekwa kwa Mo Dewji: Maelezo ya shuhuda (dereva wa Uber) na kamanda Mambosasa mbona kama yanatofautiana?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema waliomteka mfanyabiashara maarufu nchini Mohamed Dewji ‘Mo’ ni Wazungu wawili.

Akizungumza nje ya Hoteli ya Colosseum leo Alhamisi Oktoba 11, 2018 amesema watu watatu wanashikiliwa kuhusika kwa tukio hilo kwa ajili ya mahojiano zaidi.

"Asubuhi ya leo Wazungu wawili walikuwa na gari aina ya Surf. Kulikuwa na magari mawili, moja lilikuwa ndani na lingine nje, gari la ndani liliwasha taa ghafla na lile lililokuwa nje likaingia na kwenda kupaki karibu na gari la MO Dewji lililokuwa limepaki.”

“Na MO akiwa ndani ya gari hilo Wazungu wawili wakatoka na kumbana MO Dewji baada ya kutoka ndani ya gari lake na kisha kumpakia katika gari lao aina ya Surf kisha wakaondoka naye kusikojulikana," amesema Mambosasa.

Hata hivyo, dereva wa Uber amesimulia tukio la kutekwa kwa Mo Dewji akisema alikuwa anakwenda kumshusha abiria katika hoteli hiyo saa 11 asubuhi ndipo alipokutana na tukio hilo.

“Tulikuwa tunakaribia eneo hilo, mara mbele yetu tukaona watu wanne wameshuka kwenye gari dogo wakiwa wamejifunika usoni, wakapiga risasi moja juu, wale askari wa hoteli kila mmoja akakimbia,” anasimulia.

“Waliingia ndani ya hoteli na kutoka na mtu, ambaye nilimjua kuwa ni Mo,” amesimulia dereva huyo ambaye anadai muda mwingi alikuwa amejiinamia kwenye gari kwa hofu.

Inadaiwa waliingia sehemu ya kufanyia mazoezi ‘gym’ na kumkuta hapo huku wakiwaacha watu wengine waliokuwa hapo.

Anasema baada ya watu hao kumchukua mwekezaji huyo wa klabu ya Simba waliondoka na gari kwa kasi kuelekea maeneo ya Masaki.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema polisi wanafuatilia taarifa za madai ya kutekwa kwa mfanyabiashara huyo.

Chanzo:Mwananchi online.

Naona Mfanyakazi WA MBOWE leo UMESHINDA HAPA JF kwa kazi maalumu tu...ya kuwaaminisha watanzania ya kuwa ni serikali ya MAGUFULI ndio inahusika na hiki kilicho mtokea MO....UMESAHAU KABSA KUZUNGUMZIA SUALA LA MBUNGE WENU KUWAKIMBIA....inawezekana kabsa CHADEMA KWA SASA HUU UMAFIA NDIO PLAN B YENU YA KUPAMBANA NA MAGUFULI mkishirikiana na hao MABALOZI WA WA EU wanaowapatia misaada
 
Hawa Moderators akili zao mara nyingine zinapishana sana. MImi nilianzisha hii thread wakaihamishia wapi sijui. Wanaudhi sana mara nyingine.

Huwa mara nyingi sana nayatilia shaka maelezo ya Polisi kuhusu matukio mbalimbali ya uhalifu nchini, hasa yale ambayo polisi huwa wanahusika, kwa mfano kuuwawa kwa watuhumiwa. Siku zote nimeamini kwamba Polisi wanaweka chumvi nyingi sana katika kusimulia hayo matokio, na hata mara nyingine kupindisha ukweli kimakusudi kwa faida au maslahi ya serikali au ya polisi wenyewe.

Sasa katika kile ambacho kinaonekana ni muendelezo wa Polisi kusimulia mambo tofauti na tukio, ni hili la utekwaji wa MO. Huwezi kuamini kwamba wanasimulia juu ya tukio lilelile. Dereva wa Uba ambaye alikuwapo wakati wa tukio la utekaji anaeleza ifuatavyo;

View attachment 894219
Sasa, tofauti na hayo maelezo ya dereva wa Uba ambaye alikuwapo, Mambosasa ambaye hakuwapo kwenye tukio anaeleza yafuatyo;

View attachment 894221
Sasa wana JF, hebu niambieni, tuamini maelezo yepi; ya dereva wa Uba aliyekuwapo wakati tukio likitokea, au Mambosasa ambaye anaweza akawa na ajenda nyingine kwenye kutoa haya maelezo kama ilivyo kawaida ya Polisi?

Ukweli ni kwamba binafsi naona kama Mambosasa anatoa maelezo kwa namna ya kupotosha ukweli fulani. Utafikiri ana wasiwasi hawa watu wasiojulikana ni wale wanaojulikana na anajaribu kufanya watu wasidhani kwamba watekaji ni watu wasiojulikana wanaojulikana ili serikali isilaumike.

Lakini jumuisho la yote ni kwamba tunafurahi kusikia MO ameshapatikana.
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema waliomteka mfanyabiashara maarufu nchini Mohamed Dewji ‘Mo’ ni Wazungu wawili.

Akizungumza nje ya Hoteli ya Colosseum leo Alhamisi Oktoba 11, 2018 amesema watu watatu wanashikiliwa kuhusika kwa tukio hilo kwa ajili ya mahojiano zaidi.

"Asubuhi ya leo Wazungu wawili walikuwa na gari aina ya Surf. Kulikuwa na magari mawili, moja lilikuwa ndani na lingine nje, gari la ndani liliwasha taa ghafla na lile lililokuwa nje likaingia na kwenda kupaki karibu na gari la MO Dewji lililokuwa limepaki.”

“Na MO akiwa ndani ya gari hilo Wazungu wawili wakatoka na kumbana MO Dewji baada ya kutoka ndani ya gari lake na kisha kumpakia katika gari lao aina ya Surf kisha wakaondoka naye kusikojulikana," amesema Mambosasa.

Hata hivyo, dereva wa Uber amesimulia tukio la kutekwa kwa Mo Dewji akisema alikuwa anakwenda kumshusha abiria katika hoteli hiyo saa 11 asubuhi ndipo alipokutana na tukio hilo.

“Tulikuwa tunakaribia eneo hilo, mara mbele yetu tukaona watu wanne wameshuka kwenye gari dogo wakiwa wamejifunika usoni, wakapiga risasi moja juu, wale askari wa hoteli kila mmoja akakimbia,” anasimulia.

“Waliingia ndani ya hoteli na kutoka na mtu, ambaye nilimjua kuwa ni Mo,” amesimulia dereva huyo ambaye anadai muda mwingi alikuwa amejiinamia kwenye gari kwa hofu.

Inadaiwa waliingia sehemu ya kufanyia mazoezi ‘gym’ na kumkuta hapo huku wakiwaacha watu wengine waliokuwa hapo.

Chanzo:Mwananchi.
Kiukweli mimi mwenyewe nimejiuliza sana tofauti ya kauli hizi, pia kilichonishtua zaid ni ile kuambiwa kuwa hata cctv hazikunasa tukio. Ukiangalia maelezo hayo mawili, kama kweli alivosimulia dereva ni kweli, basi mambosasa anajua kila kitu kuhusu utekaji huu ila anajaribu kudivert attention ya watu.
Maana haiwezekan tukio litokee camera zisinase ila uje kuconclude kuwa ni wazungu. Umejuaje, kama ni ngoz nyeus na maana umewapa nafasi hao watu kukimbia wakat ukiwa busy kumtafuta huyo mzungu.
Hapa sasa nakumbuka lile tukio la mwanafunzi aliyepigwa risas jinsi risasi za zilipogeuka na kuwa zilitokea upande wa viongoz. Hivi nan alitoa kauli vile? Tuwe serious na kaz zetu jaman wengine wanaushi na kujenga kupitia mo. Je kwa uzembe huo mnahatarisha milo ya watu 28000. Kumbuken wengine ni wakwe zenu
 
1539266750987.png
 
Hawa Moderators akili zao mara nyingine zinapishana sana. MImi nilianzisha hii thread wakaihamishia wapi sijui. Wanaudhi sana mara nyingine.

Huwa mara nyingi sana nayatilia shaka maelezo ya Polisi kuhusu matukio mbalimbali ya uhalifu nchini, hasa yale ambayo polisi huwa wanahusika, kwa mfano kuuwawa kwa watuhumiwa. Siku zote nimeamini kwamba Polisi wanaweka chumvi nyingi sana katika kusimulia hayo matokio, na hata mara nyingine kupindisha ukweli kimakusudi kwa faida au maslahi ya serikali au ya polisi wenyewe.

Sasa katika kile ambacho kinaonekana ni muendelezo wa Polisi kusimulia mambo tofauti na tukio, ni hili la utekwaji wa MO. Huwezi kuamini kwamba wanasimulia juu ya tukio lilelile. Dereva wa Uba ambaye alikuwapo wakati wa tukio la utekaji anaeleza ifuatavyo;

View attachment 894219
Sasa, tofauti na hayo maelezo ya dereva wa Uba ambaye alikuwapo, Mambosasa ambaye hakuwapo kwenye tukio anaeleza yafuatyo;

View attachment 894221
Sasa wana JF, hebu niambieni, tuamini maelezo yepi; ya dereva wa Uba aliyekuwapo wakati tukio likitokea, au Mambosasa ambaye anaweza akawa na ajenda nyingine kwenye kutoa haya maelezo kama ilivyo kawaida ya Polisi?

Ukweli ni kwamba binafsi naona kama Mambosasa anatoa maelezo kwa namna ya kupotosha ukweli fulani. Utafikiri ana wasiwasi hawa watu wasiojulikana ni wale wanaojulikana na anajaribu kufanya watu wasidhani kwamba watekaji ni watu wasiojulikana wanaojulikana ili serikali isilaumike.

Lakini jumuisho la yote ni kwamba tunafurahi kusikia MO ameshapatikana.
Hata mim nimeanzisha hii kitu wakahamisha. Ili kuweza fanikisha ni kuacha watu watiririke wanavyoona mnaweza pata hints za kuanzia
 
Naona Mfanyakazi WA MBOWE leo UMESHINDA HAPA JF kwa kazi maalumu tu...ya kuwaaminisha watanzania ya kuwa ni serikali ya MAGUFULI ndio inahusika na hiki kilicho mtokea MO....UMESAHAU KABSA KUZUNGUMZIA SUALA LA MBUNGE WENU KUWAKIMBIA....inawezekana kabsa CHADEMA KWA SASA HUU UMAFIA NDIO PLAN B YENU YA KUPAMBANA NA MAGUFULI mkishirikiana na hao MABALOZI WA WA EU wanaowapatia misaada

Hata Mimi naweza amini hivyo kabisa.
 
Back
Top Bottom