Kosa ni la msaliti?

Kosa ni la msaliti?

Kwa mtazamo wangu makosa yapo kwa wote, in short katika dunia ya hivi sasa iliyojaa ulaghai na utapeli kumwamini mtu kupitiliza awe mpenzi au rafiki ni kosa la kimkakati, watu wengi siku hizi wamekuwa wabinafsi kupitiliza wenye kujijali wao binafsi, utu umepotea, ukiwa katika mahusiano na mtu inabidi kukaa kimachale, kosa la huyo dada ni kumwamini jamaa kupitiliza na kosa la jamaa ni kutumia udhaifu huo kufanya alilofanya itoshe kusema mahusiano (ndoa ikiwemo) hivi sasa yamekaa kimtego mno, ni vyema kuishi kwa akili sana na kuchukua tahadhari zote, wanaume na wanawake wanaotapeliwa kwenye mahusiano ni wengi, matapeli kotekote
 
Kosa la Mwanamke Anapopenda Ni Nini?

Kuna mtoa mada juzi kasema kwamba dada yake alikuwa in love na mshikaji fulani na mwisho wa siku yule jamaa akamtapeli ikiwemo kadi yake ya bank, na kumuacha akiwa mjamzito

Nikaona baadhi ya comments wakisema kwamba wanawake huwa tunapenda sana bila kuchunguza au kutumia akili

Sasa najiuliza, kosa la huyo dada ni nini hasa?

Kumpenda huyo mwanaume na kumwamini hilo ndiyo kosa?

Kwa nini tusimlaumu kwanza mwanaume kwa kuwa msaliti na tapeli wa mapenzi?

In short ameaminiwa ila amefanya hiyana wakulaumiwa hapa ni huyu binadamu aliekosa utu na kuongozwa na tamaa

Ajabu ni kwamba mwanamke akipenda sana utasikia:
Utasikia 👇

Wanawake wakipenda wanapenda vibaya, hawatumii akili
ooh 👇
Mwanamke akitiwa vizuri hasikii wala haoni

Hapo mwanamke kaonekana amependa vibaya sio kupongezwa kwa kua na upendo usiopimika

Sasa ikitokea mwanamke kaamua kua bandidu
unasikia👇

Wanawake ni majambazi, tusiwaamini, ni watu wabaya, hawana mapenzi..🙄

Na bla bla kibao
Hata hapa jamvini tunaona hizi shutuma

Sasa mimi nashangazwa...

Mwanamke akipenda kwa moyo, akaamini na kujitoa kwa mtu, mwisho wa siku akapigwa matukio na kudhalilishwa, tunaishia kusema:

Alitumia hisia badala ya akili
Na kuacha kulaumu mharibifu

Akiamua kuwa bandidu, kujilinda na kutoweka moyo wake kirahisi, unaambiwa:👇

Huyu sio wife material

Sasa mwanamke afanye nini? 😅

Tukipenda sana, tunatumia akili vibaya
Tukijilinda, hatuna upendo
Tukiamini, tumejitoa bila kuchunguza
Tukikataa kuamini kirahisi, tunaambiwa tuna attitude

Basi kosa la mwanamke linakuwa nini hasa?

Nyinyi wanaume, nawaambieni kitu...

Mwanamke anapojitolea kukupenda kwa moyo bila kuwa na kasumba nyingi, wewe ambaye unapendwa appreciate hiyo nafasi

Usigeuze upendo wa mwenzako kuwa fimbo ya kumchapia
Usitumie udhaifu wa mtu anayekupenda kama silaha dhidi yake

Na kama unaona kwamba upendo unaopewa unakuzidi, au unaona huwezi kuurudisha kwa kiwango anachokupa, ni bora kuwa muwazi kwenye mapenzi kuliko kuendelea kumshikilia mtu huku ukijua humthamini na wala huna haja nae

Mwambie ukweli
Mwambie unachoweza na usichoweza kumpa ajue kabisa ananyoa au anasuka

Na hii hata kwa mwanamke pia ni vivyo hivyo ukiona hujamuelewa mshikaji be open mapema MUDA NI MALI!

Maana wakati mwingine kinachomuumiza mtu si kwamba hapendwi, bali ni kupewa matumaini na mtu ambaye tayari anajua hawezi kumpenda

Na mwisho wa siku, moyo wenye upendo si ule unaopenda tu

Moyo wenye upendo ni ule ambao haumuumizi mwingine kwa makusudi(labda bahati mbaya)

Swali la mjadala 👇
Kosa ni la anaependa sana na kujitolea?
Au kosa ni la anaeumiza mwingine
Kwa kumjeruhi kihisia au hata kiuchumi?

ShesRise_1 ✋️
Ninachofahamu utapeli na ujinga wa mapenzi uko pande zote mbili ili kwa wanawake vitu vyote viwili vimezidi zaidi
 
Kwa mtazamo wangu makosa yapo kwa wote, in short katika dunia ya hivi sasa iliyojaa ulaghai na utapeli kumwamini mtu kupitiliza awe mpenzi au rafiki ni kosa la kimkakati, watu wengi siku hizi wamekuwa wabinafsi kupitiliza wenye kujijali wao binafsi, utu umepotea, ukiwa katika mahusiano na mtu inabidi kukaa kimachale, kosa la huyo dada ni kumwamini jamaa kupitiliza na kosa la jamaa ni kutumia udhaifu huo kufanya alilofanya itoshe kusema mahusiano (ndoa ikiwemo) hivi sasa yamekaa kimtego mno, ni vyema kuishi kwa akili sana na kuchukua tahadhari zote, wanaume na wanawake wanaotapeliwa kwenye mahusiano ni wengi, matapeli kotekote
Aisee hiki ni nini?
Watu tumeifanya dunia kua shagala bagala 🙌
Hakuna kuaminiana tena
 
Nyasi zinaliwa na pundamilia na simba anakula pundamilia, nyasi zinaona simba ni mlinzi wake hazijui kuwa simba ni katili kiasi gani. Pundamilia nao wanaona nyasi ni mwokozi wao kwa chakula hawajui zinawachukia kiasi gani, laiti nyasi zingejua ukweli au basi mwenye buku anikopeshe ☺️
Umeandika falsafa kubwa sana, i hope ushapata buku lako.
 
Back
Top Bottom