Kosa ni la msaliti?

Kosa ni la msaliti?

Twin kuna watu ni matapeli wa kutupwa anaweza kuigiza hata kwa kipindi kirefu sema tu ukiwa makini unaweza kuona red flags ndogo ndogo

Hapa atalaumiwa huyu dada kama unavyosema lakini huyu tapeli nae asiacwe hii ni tabiya mbaya sana kujinufaisha kwa namna hii

Sawa sawa shukrani twini 😊
Lakini wanawake kawaida wanaangukia kwenye mikono ya matapeli eti wanatafuta bad boys.

Mwanamke ni kawaida kumkataa mwanaume sahihi, akaenda kumchagua mwanaume tapeli, katili.

Ni same tu kwa kijana wa kiume anaweza kumwacha Binti anayejielewa, akaenda kuwachagua sijui wanawahita bad girls.

MAPENZI UPOFU
 
Kosa la Mwanamke Anapopenda Ni Nini?

Kuna mtoa mada juzi kasema kwamba dada yake alikuwa in love na mshikaji fulani na mwisho wa siku yule jamaa akamtapeli ikiwemo kadi yake ya bank, na kumuacha akiwa mjamzito

Nikaona baadhi ya comments wakisema kwamba wanawake huwa tunapenda sana bila kuchunguza au kutumia akili

Sasa najiuliza, kosa la huyo dada ni nini hasa?

Kumpenda huyo mwanaume na kumwamini hilo ndiyo kosa?

Kwa nini tusimlaumu kwanza mwanaume kwa kuwa msaliti na tapeli wa mapenzi?

In short ameaminiwa ila amefanya hiyana wakulaumiwa hapa ni huyu binadamu aliekosa utu na kuongozwa na tamaa

Ajabu ni kwamba mwanamke akipenda sana utasikia:
Utasikia 👇

Wanawake wakipenda wanapenda vibaya, hawatumii akili
ooh 👇
Mwanamke akitiwa vizuri hasikii wala haoni

Hapo mwanamke kaonekana amependa vibaya sio kupongezwa kwa kua na upendo usiopimika

Sasa ikitokea mwanamke kaamua kua bandidu
unasikia👇

Wanawake ni majambazi, tusiwaamini, ni watu wabaya, hawana mapenzi..🙄

Na bla bla kibao
Hata hapa jamvini tunaona hizi shutuma

Sasa mimi nashangazwa...

Mwanamke akipenda kwa moyo, akaamini na kujitoa kwa mtu, mwisho wa siku akapigwa matukio na kudhalilishwa, tunaishia kusema:

Alitumia hisia badala ya akili
Na kuacha kulaumu mharibifu

Akiamua kuwa bandidu, kujilinda na kutoweka moyo wake kirahisi, unaambiwa:👇

Huyu sio wife material

Sasa mwanamke afanye nini? 😅

Tukipenda sana, tunatumia akili vibaya
Tukijilinda, hatuna upendo
Tukiamini, tumejitoa bila kuchunguza
Tukikataa kuamini kirahisi, tunaambiwa tuna attitude

Basi kosa la mwanamke linakuwa nini hasa?

Nyinyi wanaume, nawaambieni kitu...

Mwanamke anapojitolea kukupenda kwa moyo bila kuwa na kasumba nyingi, wewe ambaye unapendwa appreciate hiyo nafasi

Usigeuze upendo wa mwenzako kuwa fimbo ya kumchapia
Usitumie udhaifu wa mtu anayekupenda kama silaha dhidi yake

Na kama unaona kwamba upendo unaopewa unakuzidi, au unaona huwezi kuurudisha kwa kiwango anachokupa, ni bora kuwa muwazi kwenye mapenzi kuliko kuendelea kumshikilia mtu huku ukijua humthamini na wala huna haja nae

Mwambie ukweli
Mwambie unachoweza na usichoweza kumpa ajue kabisa ananyoa au anasuka

Na hii hata kwa mwanamke pia ni vivyo hivyo ukiona hujamuelewa mshikaji be open mapema MUDA NI MALI!

Maana wakati mwingine kinachomuumiza mtu si kwamba hapendwi, bali ni kupewa matumaini na mtu ambaye tayari anajua hawezi kumpenda

Na mwisho wa siku, moyo wenye upendo si ule unaopenda tu

Moyo wenye upendo ni ule ambao haumuumizi mwingine kwa makusudi(labda bahati mbaya)

Swali la mjadala 👇
Kosa ni la anaependa sana na kujitolea?
Au kosa ni la anaeumiza mwingine
Kwa kumjeruhi kihisia au hata kiuchumi?

ShesRise_1 ✋️
Ninachoweza kushauri

Penda kwa moyo.
Chunguza kwa akili.
Jenga kwa muda.
Weka mipaka.
Na usimlazimishe mtu kukupenda.

Kwa sababu moyo wenye upendo sio ule unaopenda tu.

Moyo wenye upendo ni ule unaojua kupenda bila kumuumiza mwingine na pia bila kujiumiza wenyewe kwa makusudi
 
Lakini wanawake kawaida wanaangukia kwenye mikono ya matapeli eti wanatafuta bad boys.

Mwanamke ni kawaida kumkataa mwanaume sahihi, akaenda kumchagua mwanaume tapeli, katili.

Ni same tu kwa kijana wa kiume anaweza kumwacha Binti anayejielewa, akaenda kuwachagua sijui wanawahita bad girls.

MAPENZI UPOFU

Kwanza hakuna watu matapeli kama Wanawake kwa sababu almost maisha yao ni maigizo, pretending, editing n.k

Kuna utapeli zaidi ya kuvaa mawigu na kupaka makeup?
 
mapenzi ni kamari ya kihisia. huwez kucontrol kilichopo akilini kwa mwenza wako, but you can control how much power their choices have over your life.

Don't gamble what you can't afford to lose
Unatema fact tupu leo mwehu ndama safiii 🔥🔥
Huwezi kucontrol kilichopo akilini kwa mwenza wako :hii ni kweli
 
Mimi sizungumzii Mwanamke. Nazungumzia makosa.
Sawa nimeelewa kaka
Mwanamke ni kama mwanaume.

Kumpenda mtu ni kosa kama utampenda mtu asiye sahihi. Elewa hilo.
Nakubali ndiyo
Kumkatili mtu ni jambo jema kama utamkatili mtu sahihi.
Sawa mkuu
So hilo wanalosema wanawake wanapenda kichwakichwa au wale wanaume wanaopigwa za uso kwangu naona wanastahili kwa sababu wangekuwa makini yasingewapata.
Kupenda kicwa kicwa inaweza kua mbaya lakini wewe uliependwa kicwa kicwa na kuaminiwa

Kwanini umtendee maovu huyo mwenza wako kosa lake nini kubwa hata asitahili kutendewa au kulipwa maumivu?
 
Sawa nimeelewa kaka

Nakubali ndiyo

Sawa mkuu

Kupenda kicwa kicwa inaweza kua mbaya lakini wewe uliependwa kicwa kicwa na kuaminiwa

Kwanini umtendee maovu huyo mwenza wako kosa lake nini kubwa hata asitahili kutendewa au kulipwa maumivu?
Unatafuta amani kwenye kambi ya magaidi 😂
 
Ninachoweza kushauri

Penda kwa moyo.
Chunguza kwa akili.
Jenga kwa muda.
Weka mipaka.
Na usimlazimishe mtu kukupenda.

Kwa sababu moyo wenye upendo sio ule unaopenda tu.

Moyo wenye upendo ni ule unaojua kupenda bila kumuumiza mwingine na pia bila kujiumiza wenyewe kwa makusudi
Hakika hakika hakika umenena 👏👏
Lakini pia watu tujiepushe na kua sababu ya maumivu kwa wengine
Hata kama tumependwa sana na waliutupenda wakajiachia kwetu tusiwaumize

Watu hatujafanana maarifa !
 
Sawa nimeelewa kaka

Nakubali ndiyo

Sawa mkuu

Kupenda kicwa kicwa inaweza kua mbaya lakini wewe uliependwa kicwa kicwa na kuaminiwa

Kwanini umtendee maovu huyo mwenza wako kosa lake nini kubwa hata asitahili kutendewa au kulipwa maumivu?

Mimi sijakutendea uovu.
Mimi sio mwaminifu ila uliamua kunipenda hivyohivyo.

Kwa nini hukuchagua waaminifu ili ulipwe uaminifu. Badala yake ukanichagua mimi mhuni.
Ulitegemea ule Ndizi alafu upate ladha ya nanasi Mdogo wangu?

Hii Dunia lazima ujue wapo wema na wabaya. Ukishalijua hilo kazi inabaki kwako. Unaamua unachagua yupi.

Kitendo cha kusema hujui mwema ni yupi na mbaya ni yupi ni kiashiria hujitambui, hujui unataka nini,
Ndio maana kuna muda unatakiwa uchunguze.

Umeingia kwenye biashara ya madini.
Lazima ujue kuna chupa na vioo au mawe yanayofanana na madini lakini sio madini.

So ukiuziwa chupa na mtu akakuambia ni Madini kosa ni lako wewe sio lake. Kwa sababu wewe ulinunua ile chupa kama madini, wakati sio madini
 
Mimi sijakutendea uovu.
Mimi sio mwaminifu ila uliamua kunipenda hivyohivyo.
Hakuna namna nitaeleweka naona kwa sababu nadhani tumetofautia mioyo
Kwa nini hukuchagua waaminifu ili ulipwe uaminifu. Badala yake ukanichagua mimi mhuni.
Ulitegemea ule Ndizi alafu upate ladha ya nanasi Mdogo wangu?
Alikuchagua au mlichaguana
Sawa ni makosa yake kukupenda muhuni lakini haihalalishi huo uhuni wako et una upaka mafuta na kuona ni sawa never ubaya ni ubaya tu
Hii Dunia lazima ujue wapo wema na wabaya. Ukishalijua hilo kazi inabaki kwako. Unaamua unachagua yupi.
Sawa sawa
Kitendo cha kusema hujui mwema ni yupi na mbaya ni yupi ni kiashiria hujitambui, hujui unataka nini,
Ndio maana kuna muda unatakiwa uchunguze.
Unaongea like wewe hujawahi kufanya mistake
Na sisemi hivi kuhalalisha makosa
Naongea kama binadamu ambaye issue ya kuteleza ni jambo lisilo epukika kwa 💯
So kama binadamu hutakiwi kutenda uovu kwa wale watu wanafanya mistake
Jirani yako aache mlango wazi uibe then uone ni haki yako?
Umeingia kwenye biashara ya madini.
Lazima ujue kuna chupa na vioo au mawe yanayofanana na madini lakini sio madini.

So ukiuziwa chupa na mtu akakuambia ni Madini kosa ni lako wewe sio lake. Kwa sababu wewe ulinunua ile chupa kama madini, wakati sio madini
Kosa ni lake na kosa ni lako pia
Ndiyo maana tapeli anaweza kuwajibishwa kwa kujipatia pesa kwa njia ya utapeli
 
Kama walikua wameooana basi mwenye kosa ni mwanaume, kwa sababu mkioana mnakua na lenu moja ila kama walikua hawajaoana ni watu waliopaparukiana tu na kuingizana ndani basi kosa ni la wote wawili. Kwa mwanamke kosa ni kuamini kiasi cha kumpa nyara zake mtu ambaye siye mume wake halali, na kwa mwanaume kosa ni kumsaliti mtu ambaye kamuamini.
 
Haha pole sana.

Mtu akizama kwenye penzi aambiwi chochote kuhusu mpenzi wake. Hata kama mtaa mzima unamjua ye ni tapeli, ye atajifariji nimempenda nitaendana nae hivyohivyo.
Kasheshe aisee lakini kwa nini huyo tapeli anaonekana kana kwamba yupo sahihi
 
Hakika hakika hakika umenena 👏👏
Lakini pia watu tujiepushe na kua sababu ya maumivu kwa wengine
Hata kama tumependwa sana na waliutupenda wakajiachia kwetu tusiwaumize

Watu hatujafanana maarifa !
Kabisa kabisa Na hapo ndipo tunapogusa jambo muhimu sana: kila mtu ana matarajio yake kwenye mahusiano, na watu hatujafanana maarifa, malezi, uzoefu wala namna ya kutafsiri upendo.

Mtu anaweza kukupenda kwa kiwango kikubwa sana na akaona kujitoa kwake ni kawaida, wakati wewe ukaona kiwango hicho ni kikubwa kuliko unavyoweza kurudisha. Hapo si lazima mmoja awe mbaya.

Cha muhimu ni uwazi.

Kama najua matarajio yako kwangu ni makubwa, lakini mimi sina uwezo, nia au utayari wa kukupa unachokitarajia, sitakiwi kutumia upendo wako kama sababu ya kukushikilia.

Na pia wewe kunipenda sana hakunilazimishi nikupende kwa kiwango kilekile. Upendo hauwezi kulazimishwa wala kulipwa kwa deni.

Ndiyo maana communication ni muhimu sana. Tuseme wazi tunataka nini, tunaweza kutoa nini na hatuwezi kutoa nini. Mtu akijua ukweli mapema, ana nafasi ya kuamua kama anaendelea au anaondoka.

Kwa hiyo, tusiumizane kwa makusudi, lakini pia tusichanganye “sitaki kukuumiza” na “lazima nikidhi matarajio yako yote.”

Wakati mwingine kumpenda mtu ni kuwa mkweli kwake hata kama ukweli huo utamuumiza kwa muda

Maana maumivu ya kuambiwa ukweli mapema yanaweza kuwa nafuu kuliko miaka ya kuishi kwenye matumaini ambayo wewe mwenyewe unajua hayatatimia
 
Dunia haipendi victims, Dunia inalaumu victims so don’t be a victim…

Same same nilikuwa namuhadithia mtu kuwa kuna kaka yangu (sio wa kuzaliwa) Alikuwa anampenda mkewe sana, kampa maisha, kamfungulia biashara lakini mwanamke mwisho wa siku akamissuse kila jema alilopewa. Niliyekuwa namuhadithia (ni mwanaume mtu mzima Boss wangu) Alinijibu kaka yako hana akili na alideserve alichofanyiwa….. As naive as i was nilikuwa na sympathize na victim nikashangaa mtu kusema victim hana akili, hana akili kivipi mtu ambaye ana fanya kazi ya akili, anaingiza hela nyingi na he wanted the best for his wife??

Mpaka leo namwangalia Boss wangu kwa macho tofauti….. Make it make sense!!!!
 
Back
Top Bottom