Korosho za kangomba mwaka huu zitaua MTU...

Korosho za kangomba mwaka huu zitaua MTU...

Wewe una akili sana, asilimia kubwa ya korosho itaporwa kwa watu walionunua kwa wakulima, watatishwa na kusingiziwa walanguzi na wahujumu uchumi, hivyo serikali na jeshi itaokoa hela nyingi ilizopaswa kulipa watu wa korosho MUNGU INUSURU HII NCHI..watu watakuwa maskini wa kutupwa na hapo ndio itakuwa furaha ya watawala..Ni rahisi mno kuwatawala watu maskini..
Da, kuna siku jamaa yangu akasema achukue mkopo bank dhamana nyumba kwa akijua mbona pesa zitarudi lakini kila akijaribu alikuwa anaishia njiank, kumbe mambo mengine MWENYEZ MUNGU ANAKUEPUSHA TU, just imagine tayari angechukua 15 million harafu unasikia jambo kama hili ndio kila unapokaa unajijambia tu
 
huu nao ni wizi kama ulivyowizi mwingine isipokuwa umepewa baraka na watu.wanaojiona ni bora kuliko wengine.
 
Ndugu wale wadau wa kangomba chukua hii...
Km ulinunua korosho kuanzia tani3 jiandae kuonyesha shamba lako...
Huu ndio msimamo wa serikali...imegundulika korosho nyingi si za wakulima halisi..
Uhakiki umeanza Jana na majina yatabandikwa
korosho nyingi zitakimbiwa na wenyewe...wale walionunua kwa magumashi bp juu juu.
Kikubwa andaa mipango mapema kaonyeshe shamba mwenyekiti wa mtaa na majirani lazima wathibitishe
Na km ulikodi shamba lazima uonyeshe mkataba wa kukodi shamba.

NB: Mh Rais najua unapita jf komaa pia kuna majina hewa yanaandaliwa na viongozi wa vyama vya ushirika,ukikaza utalipa tani laki1 tu zingine utazitaifisha kwa manufaa ya umma.
Nakukumbusha kuna majina hewa ya malipo...
Kwani ni lazima kuziuza kwa hao wanajeshi?

Unabangua tu unauza kg moja moja.
 
Walitumia pesa halali kununua korosho halali kwa mkulima halali kwa kutumia njia isiyo halali\haramu.
Kwani walanguzi waliiba hizo korosho au walitoa hela zao mfukoni na kununua,
 
Kangomba kama sijakosea ni wale wanaonunua mazao yakiwa shambani kwa bei ndogo kisha wanauza kwa bei kubwa. Yaani wanalalia wakulima. Sio tafsiri rasmi ila tafakuri tu.
Na ndicho kilichotokea
 
Sijaelewa neno ulanguzi linamaanisha nini? ni kununua kwa bei ya chini kwa mkulima na kuuza kwa bei ya juu kwa wengine. Wajuzi wa haya mambo nifahamisheni.
 
Mkuu heshima kwako. Msaada kama ukipanda miche 100 am 600 utavuna kilo ngapi na inahitaji heka ngapi na shingi ngapi kupanda.

Natanguliza shukran zangu za dhati kabisa
Mkurugenzi mimi nafuatilia kwa karibu tu hii issue sio mzoefu sana ninaweza kukupotosha ikiwa unataka kuwa mwekezaji serious
 
Kwenye hili sakata, madalali watatapeliwa sana. Serikali inaweza kulipa nusu ya korosho hizo nyingine wakachukua bure na wakulima wakalipwa mara mbili.
 
Ndio maana unasikia tani kadhaa zimekamatwa zikitoroshwa halafu zinataifishwa kiana
Wewe una akili sana, asilimia kubwa ya korosho itaporwa kwa watu walionunua kwa wakulima, watatishwa na kusingiziwa walanguzi na wahujumu uchumi, hivyo serikali na jeshi itaokoa hela nyingi ilizopaswa kulipa watu wa korosho MUNGU INUSURU HII NCHI..watu watakuwa maskini wa kutupwa na hapo ndio itakuwa furaha ya watawala..Ni rahisi mno kuwatawala watu maskini..
 
Hapana wakulima wamelanguliwa sana

Ushawahi kujiuliza hao wakulima huwa wanapata wapi mtaji wa kununua pembejeo? Hao mnaowaita ni walanguzi au madalali ndio hao hao huwakopesha wakulima na baadae kununua mazao yao (na mikopo kurejeshwa). Japo ni kweli hununua mazao kwa bei ya chini lakini angalau wanawawezesha wakulima kwa kuwapelekea pembejeo (kazi ambayo ni ya serikali lakini hawaifanyi). Sasa serikali hii inawapora watu korosho eti ni wakulima fake! Subirini mwakani mtajionea wenyewe
 
Mbona jambo rahisi sana unafunga ndoa na mabiti 3 ambao wazazi wana mashamba ya korosho alafu kila 1 unamgeia kiasi na ww unabaki na kiasi mnaenda kupima.
Mkuu majina yalishaenda tulizoea hivyo kiufupi hiyo imetoka ikirudi pancha
 
Yote tisa ila hakuna wanaolia kwa uchungu kama wale wafanyabiashara waliogoma kununua sababu wengi wao walichukua pesa za mikopo, wengine magunia tayari walishanunua na gharama chungu mzima

Walikua wanafikiria Magufuli alikua anawatania mpaka saivi hawaamini kama wapo Tanzania au kitandani
 
Back
Top Bottom