Korosho za kangomba mwaka huu zitaua MTU...

Korosho za kangomba mwaka huu zitaua MTU...

Nakumbuka Sera ya ubinafsishaji ya Mzee mkapa Baada ya kelele nyingi alisema : Una kitu chako cha dhamani utashidweje kumpa mtu upate kibaba cha unga ukale na wanao maisha yaendelee.(kwake alikuwa sawa )
Kwenye korosho ni kinyume chake,mkulima anayetegemea korosho yake kuishi angefanyeje? Kama siyo kuuza kwa yeyote kutatua changamoto zake .

Busara ni kununua korosho zote bila kuuliza umezipateje labda kama zimetoka nje ya Nnchi.Hakika tutapata tabu sana kila tunacho jitahidi kufanya ukijua unajikwamua unaambiwa umekosea
Wamesahau kimfaacho mtu chake
 
Mbona jambo rahisi sana unafunga ndoa na mabiti 3 ambao wazazi wana mashamba ya korosho alafu kila 1 unamgeia kiasi na ww unabaki na kiasi mnaenda kupima.
yani ufunge ndoa kisa korosho
 
ok shukrani kwa kunijuza nilikuwa sijuwi maana yake kwa hiyo walanguzi ndo wenye korosho kwa sasa na sio wakulima halisi daah hii nchi kumbe mheshimiwa alivyokuwa anawatetea wakulima kumbe tayari kulikuwa na walanguzi wana korosho ndani.
Hao wanaitwa choma choma kwa design ingine, anakaa kati ya mkulima na serikali hahah mi pia nilitaka nikatest mitambo mwaka huu sema nina nyota kali tu hahah nilihisi manyagunyagu nikaamua kuskilizia mnada wa kwanza! Baada ya mnada kutangazwa na bei iliposimamia kilichofuata nilipanda basi tu nikatembea!
 
Ni haramu coz kuna taratibu ziko wazi za kukusanya na kuuza korosho,km unataka kununua korosho subiri mnada,utanunua then vyama vya msingi vinalipa,mkulima hatakiwi kupokea pesa kutoka kwa mfanyabiashara
Sasa hiki si ndicho kilichofanyika, ila madai ya sasa ni kwamba lazima uwe na shamba na uthibitishe hilo kwa ngazi ya kjiji kwamba hizo tani zote umetolea shambani mwako na hapa ndipo walanguzi watapokula mtama!
 
Mkulima anatakiwa kupata pesa kupitia vyama vya msingi na sio MTU binafsi
Sasa kwenye chama cha msingi bei elekezi ni 1500 na kwa mtu binafsi anakupa 2000-2500 cash haina longolongo, nadhani ni kichaa pekee atakekataa bei ya 2000+ akawekeshe kwenye mnada akisubiria 1500 pamoja na songombingo zote za serikali hadi kufikia malipo! Hio biashara ya ulanguzi ni ngumu kui terminate maana mkulima ana benefit zaidi, faida zaidi na malipo ni instant!
 
Gama huyo IKIRIRI hajui tabu na maisha magumu anayopitia mkulia baada ya msimu. Mf hao wa korosho siku 1 aende kutembea Tandahimba, Nanyamba, Newala, Mahuta, Kitaya nk kuanzia mwzi wa 3 mpk 9 alafu aje akupe jibu hapa. Wengine wanaongea sababu wapo mijini au maofisini hawajui shida anazopata mkulima. Hata eao hawapendi kuuza kg 1 kwa 1500 - 2000 ila tu inawalazimu. Kama mtu unapima korosho mwez wa 9 alafu unalipwa January kwa hiyo 3000 - 3500 @kg na chomachoma unampimia na anakulipa 2000 yako hapo hapo si bora umuuzie chomachoma ufanye mambo yako.
Ni kichaa pekee ataekataa biashara ya Cash in hand!
 
Walitumia pesa halali kununua korosho halali kwa mkulima halali kwa kutumia njia isiyo halali\haramu.
We ni popoma kama walivyo mapopoma wengine, kisicho halali ni nini hapo? Kama ni hivyo basi madalali wote wapelekwe jela maana hamna biashara isio na ulanguzi hata maduka unayoona mtaani kwenu hapo! Sheria ama katiba ya nchi imevunjwa wapi na hao chomachoma?
 
Sijaelewa neno ulanguzi linamaanisha nini? ni kununua kwa bei ya chini kwa mkulima na kuuza kwa bei ya juu kwa wengine. Wajuzi wa haya mambo nifahamisheni.
Ndio maana yake, unanunua ili upige faida kwa mda mfupi yani mfano unanunua nguo kariakoo elfu 16 unaipeleka sinza jioni unaiuza kwa mteja wako elfu 25! Pia inaweza kuwa faida ya muda mrefu\ mbeleni mfano unanunua kuku singida unakuja kuwafungia kwako ukitarajia bei itapanda mwezi ujao ili upate faida!
Kwa kizungu inaitwa speculation, inakuwa interms of Futures (mda mrefu) and Options(mda mfupi)
Natumai nimekupa mwangaza!
 
We ni popoma kama walivyo mapopoma wengine, kisicho halali ni nini hapo? Kama ni hivyo basi madalali wote wapelekwe jela maana hamna biashara isio na ulanguzi hata maduka unayoona mtaani kwenu hapo! Sheria ama katiba ya nchi imevunjwa wapi na hao chomachoma?
Extrovert; kwa mfumo wanaotumia stakabadhi ghalani chomachoma bado anamsaidia mkulima asee. We fikiria unapima korosho mwezi wa 9 majina na hela zinakuja December au January ya mwaka unaofuata hiyo 3400 @ kg wakat chomachoma unapima na kupewa chako hapo hapo 2000@ kg. Wabadilishe mfumo wa ulipaji kingine ni umbali na miundombinu toka mashambani mpk kwenye stoo za kupimia. Chomachoma anakuja na usafiri wake hadi mlangoni kwa mkulima yani kuna mambo mengi sana yanayo pelekea wakulima kuwapigia chomachoma cm tena usiku ili waje kuchukua korosho.
 
Ndio mie nashangaa hata hao wanaolalamika mkulima ananyonywa kwa lipi wakati choma choma anampa hela kubwa kuliko ile ya elekezi tena cash in hand! Elekezi ni 1500 kwa kilo kule mnadani na chomachoma ametoa kati ya 2000-2500 kwa mwaka huu! Sasa huyo mkulima amenyonywa vipi hapo
 
Wengi wanasikia tu hawajafika field wakaona kinachoendelea wapo maofisini na mijini kwenye viyoyozi na kubonya macomputer huku mkulima anaumia shambani. Hata hao viongozi wanao fokafoka na kuwakamata chomachoma unadhani baada ya minada wanaonekana tena huko vijijini??
 
Kwani hiyo Biashara imekua illegal tangu lini?

Ni lipi kosa ka hao/Huyo Mnunuzi Mwenye tani zaidi ya 3?

Yaani kununua na kuhifadhi imekua kosa?
 
Kangomba kama sijakosea ni wale wanaonunua mazao yakiwa shambani kwa bei ndogo kisha wanauza kwa bei kubwa. Yaani wanalalia wakulima. Sio tafsiri rasmi ila tafakuri tu.
Huyo Mkulima anashikiwa mtutu wa bunduki au anakubali kwa ridhaa yake?

Serikali kama ingekua ina dhamira ya dhati kwanini basi isingekuwa na utaratibu wa kuwalipa some cash in advance ili watatue changamoto zao ili baadae wakivuna walipe?

Tatizo kila jambo tunatafuta kichaka cha kujifichia.

Tumesema tunayo fedha ya kununua Korosho yote iliyo vunwa, sasa tatizo ni nini?
 
Korosho ni zao la kudumu huwezi panda ndani ya msimu mmoja na kuvuna hivyo swala la kukodi shamba halipo
Acha kukariri ndugu, hata miembe ipo ya kukodi.

Kuna makubaliano maalum hufikiwa baina ya pande mbili lengo ni ili Mkulima ajipatie fedha za kuhudia Shamba lake hivyo hutenga/kupunguza eneo jingine kwa kulikodi ili apate fedha ya kuhudumia lililobaki.
 
Back
Top Bottom