Korosho za kangomba mwaka huu zitaua MTU...

Korosho za kangomba mwaka huu zitaua MTU...

Ndio hivo tena mkuu. Si unajua uelewa na umaskini wa wananchi wetu. Unampa buku kwa kilo kwasababu ya njaa zake wewe unapiga 3,300
So ukifanya hivyo unakua umefanya kosa la jinai?
 
Acha kukariri ndugu, hata miembe ipo ya kukodi.


Kuna makubaliano maalum hufikiwa baina ya pande mbili lengo ni ili Mkulima ajipatie fedha za kuhudia Shamba lake hivyo hutenga/kupunguza eneo jingine kwa kulikodi ili apate fedha ya kuhudumia lililobaki.
Labda huko kwenu; kwetu Uhani hakuna mzee anakodisha shamba lake la mikahawa eti aje mtu mwingine kuvuna
 
Labda huko kwenu; kwetu Uhani hakuna mzee anakodisha shamba lake la mikahawa eti aje mtu mwingine kuvuna
Sawa ndugu kwa kuwa kwenu Uhani hakuna basi usifikirii kwamba nchi nzima ina behaviors za huko..

No hard feelings!!
 
Wengi wanasikia tu hawajafika field wakaona kinachoendelea wapo maofisini na mijini kwenye viyoyozi na kubonya macomputer huku mkulima anaumia shambani. Hata hao viongozi wanao fokafoka na kuwakamata chomachoma unadhani baada ya minada wanaonekana tena huko vijijini??
hao wakulima hata wakipewa hizo elfu 3 still watalalamika wana nyonywa, nature ya hela huwa haitoshi na ikiwepo mahitaji yanaizidia!
 
Biashara zote kubwa duniani zinaendeshwa na speculators ambao huku tunawaita walanguzi. Hawa kazi yao ni ku take market risks and returns. Wengi wao wanatumia futures and options kama financial instruments. Sasa sijui kwa nini huku iwe ni shida au biashara haramu!
What is the difference between options and futures?
Uko sahihi,tatizo ni watu wenye mamlaka na kutuongoza hawana uzoefu au ujuzi wowote wa kibiashara.Tuko katika uchumi wa soko huria Ila wao wanafikiri na kutenda kwa uchumi wa kijamaa.
 
Ni haramu coz kuna taratibu ziko wazi za kukusanya na kuuza korosho,km unataka kununua korosho subiri mnada,utanunua then vyama vya msingi vinalipa,mkulima hatakiwi kupokea pesa kutoka kwa mfanyabiashara
Ikiwa wewe ni mkulima unayehitaji pesa lakini chama cha ushirika,benki,ndugu au serikali wote hawawezi kukukopesha pesa na mazao yako shambani,anakuja mfanyabiashara anayekubali kukupa mkopo kwa kubadilishana na mazao shambani, wewe ungefanyaje?
 
Kangomba ni kifaa kama kikombe ila chenyewe ni kikubwa mno, kinaweza kuchukua kg 1.5-2 za korosho ghafi! kwaiyo mfanya biashara anawafuata wakulima huko mashambani anawalaghai wanamuuzia kwa kangomba moja/ kg 1.5-2 kwa Tsh 1000-1500 ye anakuja kuuza ghalani 3000+ kwaiyo mtu kati/middle man ana uhakika wa kutengeneza hela kubwa kuliko mkulima ndiyo maana ilipigwa marufuku.
Kwa nini hawakujikita katika kusimamia na kuhakikisha vipimo sahihi mkulima ajue anauza kiasi gani kwa uhakika badala yake wakapiga marufuku biashara nzima?
Magari yakizidisha uzito barabarani yanapigwa faini,mzigo unapunguzwa na biashara inaendelea barabara au biashara hazifungwi kabisa.
 
Ndio mie nashangaa hata hao wanaolalamika mkulima ananyonywa kwa lipi wakati choma choma anampa hela kubwa kuliko ile ya elekezi tena cash in hand! Elekezi ni 1500 kwa kilo kule mnadani na chomachoma ametoa kati ya 2000-2500 kwa mwaka huu! Sasa huyo mkulima amenyonywa vipi hapo
Na ataenda kulipa tozo zote za halmashuri na export levy juu,ni ngumu sana kuwaelewa hawa watu.
 
Kipindi mh raid anasema serikali inanunua mlicheka mkijua mzee kaingia choose cha kike, kiukweli wafanya biashara wa bongo kuna ujinga furani wanao ule ujinga anunue shilingi mia auze elfu moja hii kitu mbaya sana ndio inafanya kila siku tunalia maisha magumu maana hakuna janja janja tena mzee kabana kwenye korosho mnaanza tafutana, haya uko arusha maduka ya kubadilishia pesa za kigeni kumenuka napo hali ni tete

Hapa kazi tu
 
Kweli mkuu..pia kuna dada wa kujiuza walikuwa wanapewa pesa badala ya korosho, yaani unakuta changudoa anazo ndani hadi gunia kumi sasa kwa hili kwake kuonyesha shamba itakuwa ngumu.
 
Back
Top Bottom