Kongole kwenu viongozi kwa hili; Walichokuwa wanakifanya machinga ni utapeli, uchafuzi na kero

Naomba kutoa pongezi zangu za dhati kabisa kwa viongozi wote walioratibu zoezi hili la kuondoa machinga katika maeneo yasiyofaa!

Ni nadra sana kuona zoezi linafanyika kwa hekima kubwa kama hili! Pasipo unafiki busara kama hii imekua adimu kwa mda mrefu sana!

Hakuna asiyejua kwamba tatizo la machinga holela lilianza kama upele na baadae kugeuka kansa sehemu ya siri, Utibuji wa kansa hii ya machinga holela ilihitaji busara kama hii!

Hongera sana Rais na watenda kazi wote, hongereni sana Wakuu wa mikoa, hongereni sana wakurugenzi na Ma DC wote, hongereni sana watendaji mliotoa ushauri kwa viongozi wenu, hongereni migambo wote kwa busara hii, hongereni machinga watiifu mlioelewa athali hii nakuondoka kwa hiari!

Hakika kwa hili tunahitaji kuwaunga mkono pasipokujali itikadi za vyama vyetu, Vyombo vya habari vyote pia vinatakiwa viwe mstari wa mbele kuripoti matukio positive ili kufanikisha zoezi hili kwa 100%.
  • Nawapa pole sana wale makaidi wachache ambao pamoja na kupewa taarifa MAPEMA lakini walikaidi kutoka,
  • Nawapa pole sana wale wote waliosoma bango la MARUFUKU lakini wakakaidi
  • Nawapa pole sana waliosikia magari ya matangazo yakiwasihi kuhama lakini WALIKAIDI
Hakika MKAIDI hafaidi hadi siku ya IDD!

Siku za IDD ni usiku wa manane ambapo magari ya manispaa, migambo na polisi watakapoanza kupita wakibomoa na kuteketeza vibanda vyote barabarani pasipo kujali kuna bidhaa ndani au hakuna!

NI UTAPELI NA UCHAFUZI UPI ULIOFANYWA NA MACHINGA

Kwa juu juu huwezi kuuona utapeli wa machinga hawa! Lakini ukitazama walichokuwa wanakifanya wale machinga ni kuchukua bidhaa dukani kwa bei X, halafu na kuiuza inje mbele ya duka hilo kwa bei XL bila risiti. Jambo ambalo linaziba biashara za walipa kodi wengine!

Mambo kama haya ya kutandaza biashara holela yalisababisha hadi wenye maduka kuanza kuagizia vijana mikoani ili waje mijini kufanya umachinga holela na maduka mengi kugeuka store!

Hili peke yake linashusha nguvu kazi ya wakulima huko kijijini kumbilia mijini kiholela!

Pia uholela wa machinga ulichangia kuhatarisha maisha yao wenyewe na ya wengine kwa kupanga bidhaa barabarani jambo lililochangia kero kubwa kwa watumia barabara wengine!

Ukiachilia hatari za kugongwa wale watembea kwa miguu kwa ufinyu wa barabara, pia machinga hawa walihatarisha miundombinu mingine kama transifoma za umeme na madaraja kwa kupanga bidhaa maeneo hatarishi!

Yote tisa, kumi lazima kila kitu kiwe mahala pake, Huruma ya kibinadamu isitufanye kutoona uchafuzi huo!

Uzembe kama huu viongozi walizembea kwenye ardhi na kuzalisha makazi holela Hivyo haiwezekani uachwe pia kuwe na biashara holela!

Hakuna asiyejua Kero ya bar na makanisa holela huko mtaani!

Hivyo nawapongeza sana viongozi kwa kuwapanga Machinga!

Nashauri nguvu iongezwe pale magogoni ferry stendi ilala mnazembea, Yale mabanda yatoke, pia kuna wale bodaboda waliopo jilani na kituo kidogo cha polisi ferry waondolewe pale wasogezwe eneo jingine, ili wasizuie abiria wanaoshuka kwenye pantoni kukosa njia!

Temeke safi, kinondoni safi, kigamboni napo ongezeni jitihada pale ferry kigamboni stand bado pachafu!

KWA WALE MAKAIDI PITENI NA GREDA USIKU WA MANANE asubuhi wakute peupe!

Umoja ni Nguvu! Salaam aleyikum!
Ninaunga mkono hoja, lakini, mimi shukrani zangu ninazihifadhi hadi uchaguzi ujao utakapopita.

Maana tushazoea swaga hizi
 
Linalofanyika sasa lisingoje kesho
Tulifunzwa pia kuwa baadhi ya semi zina madhara. Wakati baadhi ya mambo kanuni hufanya kazi, yapo maeneo hufeli kulingana na hali ama mazingira ya wakati husika.
 
Kati ya post za kipumbavu nilizowahi kusoma hapa JF hii ni kiboko!
 
Back
Top Bottom