Kongole kwenu viongozi kwa hili; Walichokuwa wanakifanya machinga ni utapeli, uchafuzi na kero

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
8,496
2,000
Naomba kutoa pongezi zangu za dhati kabisa kwa viongozi wote walioratibu zoezi hili la kuondoa machinga katika maeneo yasiyofaa!

Ni nadra sana kuona zoezi linafanyika kwa hekima kubwa kama hili! Pasipo unafiki busara kama hii imekua adimu kwa mda mrefu sana!

Hakuna asiyejua kwamba tatizo la machinga holela lilianza kama upele na baadae kugeuka kansa sehemu ya siri, Utibuji wa kansa hii ya machinga holela ilihitaji busara kama hii!

Hongera sana Rais na watenda kazi wote, hongereni sana Wakuu wa mikoa, hongereni sana wakurugenzi na Ma DC wote, hongereni sana watendaji mliotoa ushauri kwa viongozi wenu, hongereni migambo wote kwa busara hii, hongereni machinga watiifu mlioelewa athali hii nakuondoka kwa hiari!

Hakika kwa hili tunahitaji kuwaunga mkono pasipokujali itikadi za vyama vyetu, Vyombo vya habari vyote pia vinatakiwa viwe mstari wa mbele kuripoti matukio positive ili kufanikisha zoezi hili kwa 100%.
  • Nawapa pole sana wale makaidi wachache ambao pamoja na kupewa taarifa MAPEMA lakini walikaidi kutoka,
  • Nawapa pole sana wale wote waliosoma bango la MARUFUKU lakini wakakaidi
  • Nawapa pole sana waliosikia magari ya matangazo yakiwasihi kuhama lakini WALIKAIDI
Hakika MKAIDI hafaidi hadi siku ya IDD!

Siku za IDD ni usiku wa manane ambapo magari ya manispaa, migambo na polisi watakapoanza kupita wakibomoa na kuteketeza vibanda vyote barabarani pasipo kujali kuna bidhaa ndani au hakuna!

NI UTAPELI NA UCHAFUZI UPI ULIOFANYWA NA MACHINGA

Kwa juu juu huwezi kuuona utapeli wa machinga hawa! Lakini ukitazama walichokuwa wanakifanya wale machinga ni kuchukua bidhaa dukani kwa bei X, halafu na kuiuza inje mbele ya duka hilo kwa bei XL bila risiti. Jambo ambalo linaziba biashara za walipa kodi wengine!

Mambo kama haya ya kutandaza biashara holela yalisababisha hadi wenye maduka kuanza kuagizia vijana mikoani ili waje mijini kufanya umachinga holela na maduka mengi kugeuka store!

Hili peke yake linashusha nguvu kazi ya wakulima huko kijijini kumbilia mijini kiholela!

Pia uholela wa machinga ulichangia kuhatarisha maisha yao wenyewe na ya wengine kwa kupanga bidhaa barabarani jambo lililochangia kero kubwa kwa watumia barabara wengine!

Ukiachilia hatari za kugongwa wale watembea kwa miguu kwa ufinyu wa barabara, pia machinga hawa walihatarisha miundombinu mingine kama transifoma za umeme na madaraja kwa kupanga bidhaa maeneo hatarishi!

Yote tisa, kumi lazima kila kitu kiwe mahala pake, Huruma ya kibinadamu isitufanye kutoona uchafuzi huo!

Uzembe kama huu viongozi walizembea kwenye ardhi na kuzalisha makazi holela Hivyo haiwezekani uachwe pia kuwe na biashara holela!

Hakuna asiyejua Kero ya bar na makanisa holela huko mtaani!

Hivyo nawapongeza sana viongozi kwa kuwapanga Machinga!

Nashauri nguvu iongezwe pale magogoni ferry stendi ilala mnazembea, Yale mabanda yatoke, pia kuna wale bodaboda waliopo jilani na kituo kidogo cha polisi ferry waondolewe pale wasogezwe eneo jingine, ili wasizuie abiria wanaoshuka kwenye pantoni kukosa njia!

Temeke safi, kinondoni safi, kigamboni napo ongezeni jitihada pale ferry kigamboni stand bado pachafu!

KWA WALE MAKAIDI PITENI NA GREDA USIKU WA MANANE asubuhi wakute peupe!

Umoja ni Nguvu! Salaam aleyikum!
 

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
8,496
2,000
Wakimaliza wamachinga ni muda sasa wakuwathibitisha bodaboda.
Kazi ya bodaboda iwe ajira rasmi na watambulike sio mtu unaamka tu unajifunza pikipiki jioni unapakiza watu.
Ajira ni kuwapa mkataba ya kureta hesabu chombo kiwe chake baada ya Target!
 

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
8,496
2,000
Wasiwasi wangu ni kwamba Ugonjwa wa kansa unatabia ya kujirudia!

Chondechonde machinga wasijekurudi tena maeneo hayo
 

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
8,496
2,000
Kuna watu hawatauelewa ujumbe huu,lakini kiukweli machinga lilikuwa limeshakuwa tatizo.
Haiwezekani kila mahala iwe machinga!
Lazima ijulikane mahala A kuna maduka ya jumla, mahala B kuna machinga n.k

Ili machinga wakachukue bidhaa kutoa sehemu A, wakaziuze huko sehemu B !

Sasa walichokuwa wanakifanya machinga hawa ni fujo!
Kwanza waliwasumbua sana wenye magari kupiga piga bodi za gari wanapopita maeneo yao
 

Bulesi

Platinum Member
May 14, 2008
10,724
2,000
Ujumbe murua kabisa!

Defintion ya hawa machinga ni lazima iwe pana zaidi ikijumuisha wale wote wanaofanya biashara zao sehemu zote zisizokuwa RASMI. Kuwapongeza viongozi wa Dar kwa kuwaondoa wamachinga katikati ya jiji peke yake ni kupongeza kazi ambayo haijakamilika.

Wamachinga hawapo katikati ya jiji peke yake; kwamfano huku wilaya ya Kinondoni wamachinga wanafanya biashara kwenye residential plots na kuwalipa kodi walinzi wa viwanja; hivyo kukosesha mapato halmashauri kwani kama wangefanya biashara zao kwenye maeneo yaliyotengwa kama masoko ,fedha wanazowalipa walinzi wa hivi viwanja zingeingia kwenye halmashauri.!!!

Mfano halisi kwa hapo wilaya ya Kinondoni ni sehemu ijulikanayo kama RUNGWE ambapo residential plot imegeuzwa sehemu ya biashara ya machinga na kodi zote hulipwa mlinzi wa kiwanja hicho.

Athari za Hawa wamachinga ni kuchafua mazingira kwani licha ya kuwa wengi lakini hawana mahala pa kujisaidia haja kubwa hivyo kuchafua mazingira na kuwa kero kwa majirani ; licha ya kuwa chanzo cha magonjwa ya mlipuko

Mkuu wa Mkoa wa Dar na wasaidizi wake hasa DC wa Kinondoni hana budi kuwaondoa hawa machinga sehemu hiyo ya RUNGWE na MBUYUNI Kwani pia ni sehemu ambazo biashara ya madawa ya kulevya imeshamiri na uhalifu mwingi wa Mbezi Beach hupangwa hapo.

Bila kuwaondoa wamachinga wa huku pembezoni na kuwaondoa wa katikati ya jiji peke yao mtakuwa mmefanya kazi ya kiini macho na zoezi halitokuwa endelevu!!
 

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
8,496
2,000
Defintion ya hawa machinga ni lazima iwe pana zaidi ikijumuisha wale wote rwanaofanya biashara zao scheme zisizokuwa RASMI. Kuwapongeza viongozi wa Dar kwa kuwaondoa wamachinga katikati ya jiji peke yake ni kupongeza kazi amabyo haijakamilik...
Zoezi ni endelevu
 

Bulesi

Platinum Member
May 14, 2008
10,724
2,000
Zoezi ni endelevu

Ili zoezi lisijirudie rudie na kupoteza fedha kuwaondoa machinga kila siku ni lazima kuwa na COMPREHENSIVE STRATEGY ambayo haitakuwa inatekelezwa kwenye CENTRAL BUSINESS DISTRICTS peke yake bali sehemu zote ambazo biashara hufanyika sehemu zisizokuwa RASMI!!!
 

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
8,496
2,000
Ili zoezi lisijirudie rudie na kupoteza fedha kuwaondoa machinga kila siku ni lazima kuwa na COMPREHENSIVE STRATEGY ambayo haitakuwa inatekelezwa kwenye CENTRAL BUSINESS DISTRICTS peke yake bali sehemu zote ambazo biashara hufanyika sehemu zisizokuwa RASMI!!!
Wazo zuri
 

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Oct 21, 2021
218
500
Defintion ya hawa machinga ni lazima iwe pana zaidi ikijumuisha wale wote wanaofanya biashara zao sehemu zote zisizokuwa RASMI. Kuwapongeza viongozi wa Dar kwa kuwaondoa wamachinga katikati ya jiji peke yake ni kupongeza kazi ambayo haijakamilika. Wamachinga hawapo katikati ya jiji peke yake...
Machinga warudishwe makwao
 

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
43,675
2,000
Kongole kwa serikali kwa kuwapanga upya wamachinga....Msirudi Nyuma ,hakuna anayekubali mabadiliko kama hayo kirahisi lazima kutakuwa na denial kwa baadhi ya machinga hao watakaopinga sheria zichukue mkondo wake ni Fine ya laki 3 ,kifungo cha mwaka mmoja au vyote kwa pamoja.
 

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
8,496
2,000
Kongole kwa serikali kwa kuwapanga upya wamachinga....Msirudi Nyuma ,hakuna anayekubali mabadiliko kama hayo kirahisi lazima kutakuwa na denial kwa baadhi ya machinga hao watakaopinga sheria zichukue mkondo wake ni Fine ya laki 3 ,kifungo cha mwaka mmoja au vyote kwa pamoja.
Umenena vyema sana!
 

Trubarg

JF-Expert Member
Jan 8, 2020
2,530
2,000
Umeandika vzuri..tatizo naloliona ni kuchelewa kuyasafisha maeneo ambayo chingaz wameandoka..unakuta vimebaki vibanda vichache pale na mbao na mabati..sasa wengine wakiona hivyo wanarudi na kuanza kujenga upya...angalia pale Shekilango na kwengine
 

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
8,496
2,000
Umrandika vzuri..tatizo naloliona ni kuchelewa kuyasafisha maeneo ambayo chingaz wameandika..unakufa vimebaki vibanda vichache pale na mbao na mabati..sasa wengine wakiona hivyo wanarudi na kuanza kujenga upya...angalia pale Shekilango na kwengine
Kweli kabisa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom