Kombe la Mapinduzi linatukumbusha haya ndiyo "Mapinduzi ya Zanzibar"

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,136
7,903
Kuna wakati mtaani kulikuwa na msemo wa "Mapinduzi ya Zanzibar" kumaanisha mambo yanayotokea yasiyoeleweka au yanayochanganya kiasi cha kuvuruga akili za watu. Tumeona katika nusu fainali hii ya Simba vs Singida maana halisi ya msemo huo.

Tukianzia, dakika za nyongeza zilitajwa 8 halafu zikapunguzwa hadi 6, inawezekana refa hakuwa anajua dakika kupunguzwa na sielewi pia kwa nini zipunguzwe toka 8 ukichukulia mpira ulisimama sana. Juzi juzi kuna watu walipewa dakika 9 ili wasawazishe.

Tuchukulie kweli zile za nyongeza ziliisha, tukumbuke hata mwezi sidhani kama umeisha toka Simba walipokuwa wahanga wa hali hiyo hiyo kule Morocco. Kawaida refa hawezi kumaliza mpira katikati ya set piece, lazima ipigwe kwanza na iwe clear kuwa imeokolewa hapo ndiyo anaweza kumaliza mpira.

Tukienda kwenye maamuzi ya refa kuhusiana na ile kona ya mwisho, refa alikuwa sahihi kabisa maana Saidoo alipoupiga mpira, beki wa Singida aliugonga ndiyo maana kipa alienda kujaribu kuudaka ingawa ukawa umeshatoka. Ule mpira ungekuwa haujaguswa na mchezaji wa Singida, usingeona golikipa akijaribu kuudaka.

Huyu anampindua huyu, na hapo hapo aliyepindua naye anakuja kupinduliwa na mwingine. Haya ndiyo Mapinduzi ya Zanzibar, tuyasherehekee.
 
Ingiza u tube uangalie vizuri liletukio, hakuna mchezaji wa Singida aliye ugusa mpira wakati Saidoo anaupiga.
Saidoo alipiga na kipa akaudaka ila mpira ulisha vuka mstari na aliudakia nje kwaiyo haikustahili pigo la Kona.
 
Kuna wakati mtaani kulikuwa na msemo wa "Mapinduzi ya Zanzibar" kumaanisha mambo yanayotokea yasiyoeleweka au yanayochanganya kiasi cha kuvuruga akili za watu. Tumeona katika nusu fainali hii ya Simba vs Singida maana halisi ya msemo huo.

Tukianzia, dakika za nyongeza zilitajwa 8 halafu zikapunguzwa hadi 6, inawezekana refa hakuwa anajua dakika kupunguzwa na sielewi pia kwa nini zipunguzwe toka 8 ukichukulia mpira ulisimama sana. Juzi juzi kuna watu walipewa dakika 9 ili wasawazishe.

Tuchukulie kweli zile za nyongeza ziliisha, tukumbuke hata mwezi sidhani kama umeisha toka Simba walipokuwa wahanga wa hali hiyo hiyo kule Morocco. Kawaida refa hawezi kumaliza mpira katikati ya set piece, lazima ipigwe kwanza na iwe clear kuwa imeokolewa hapo ndiyo anaweza kumaliza mpira.

Tukienda kwenye maamuzi ya refa kuhusiana na ile kona ya mwisho, refa alikuwa sahihi kabisa maana Saidoo alipoupiga mpira, beki wa Singida aliugonga ndiyo maana kipa alienda kujaribu kuudaka ingawa ukawa umeshatoka. Ule mpira ungekuwa haujaguswa na mchezaji wa Singida, usingeona golikipa akijaribu kuudaka.

Huyu anampindua huyu, na hapo hapo aliyepindua naye anakuja kupinduliwa na mwingine. Haya ndiyo Mapinduzi ya Zanzibar, tuyasherehekee.
Mapinduzi matukutu.
 
Kuna wakati mtaani kulikuwa na msemo wa "Mapinduzi ya Zanzibar" kumaanisha mambo yanayotokea yasiyoeleweka au yanayochanganya kiasi cha kuvuruga akili za watu.

Huyu anampindua huyu, na hapo hapo aliyepindua naye anakuja kupinduliwa na mwingine. Haya ndiyo Mapinduzi ya Zanzibar, tuyasherehekee.
Tarehe kama ya leo 11/01/1964 miaka 60 iliyopita, ndio Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalifanyika!. Alfajiri ya Tarehe 12 Januari, 1964 ilikuwa ni kutangazwa tuu!.

Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Paskali
 
Back
Top Bottom