Kodi ya nyumba imetaka kumliza mtu, tuweni makini

Kulupango

JF-Expert Member
Mar 19, 2020
288
534
IMG-20200709-WA0004.jpg

Kuliluwa na stress za kodi ya nyumba ya mama mwenye nyumba, na pesa ilikuwa imeshapatikana kwa ajili ya kulipwa, khafla meseji hiyo ikaingia. Jamaa akataka kuituma lakini roho ikasita, kumfata mwenye nyumba kasema hiyo meseji haitambui na wala hajatuma meseji hiyo na wakati matukio ya kuzoza kuhusu kodi na kuingia kwa meseji hiyo yamefatana.

Ujumbe kutoka Vodacom


IMG-20200709-WA0005.jpg
 
Angeituma ingefaa watu mchukue marungu mmuweke mtu kati mponde hicho kichwa kabisa.
Utapeli wa kizamani mno.
 
Shida ni kwamba meseji imeingia nayeye yupo kwenye pirika za kupeleka hiyo pesa, kwa haraka haraka unaweza kuchanganyikiwa
Ni kama ile ya mzazi aliye na mtoto boarding school kutumiwa message ya hivyo kuwa mwanawe kazidiwa anafaa atume kiasi fulani cha pesa.Halafu mtuma ujumbe anajitambulisha kama mwalimu.

Hapo ukituma unakuwa choko! Namba ya mhusika unayo(mwalimu,mwenye nyumba n.k) unashindwa vipi kuuliza kupata uhakika kwanza,Halafu mtu katumia namba ngeni hajajitambulisha hata!

Mtu angetapeliwa hivi miaka kama mitatu iliyopita ningemsikitikia.Ila kipindi hiki ambapo hata mwananchi wa kijijini ashafahamu hizi janja hamna siwezi kumwelewa.Na wenyewe wanatuma hizi message random hivi wanafahamu mbili tatu hivi lazima ziwapate wahusika tu.
 
Back
Top Bottom