Wazolee
JF-Expert Member
- Sep 1, 2018
- 2,702
- 3,091
Hii nchi inavituko sana kwa hiyo TRA mmeshindwa kupita mitaani kuzisajili nyumba zote zinazofanya biashara na kuamuru wamiliki wa nyumba hizo walipe kodi ya pango badala yake mnataka mkusanye kodi hizo kupitia wapangaji, hichi ni kichekesho!
Eti kifungu cha sheria (82)2(a) kinamtaka mpangaji apeleke kodi ya pango TRA
Hivi kweli wasomi wa Tanzania mnakutana na kutunga sheria mbovu kama hii mbona nyinyi wasomi wa hii nchi mnatutia aibu?!
Vipi huyu mpangaji asipolipa hiyo kodi ya pango, mtampa adhabu gani kwa kutolipa kodi ya pango ya jengo ambalo yeye si mmiliki bali mmiliki wake yupo amekunja 4 sebuleni anaangalia TV?
Ubovu wa sheria zenu mmefanya wafanya biashara wote hapa nchini walipe hiyo kodi ya pango kutoka mifukoni mwao, na sio kama hamjui mnajua sana kuwa hizo kodi mnazowakamua wafanya biashara na wala sio wenye nyumba.
Sasa hawa wafanya biashara hawana jinsi ndio maana mkiwalazimisha walipe hiyo kodi ya pango wanalipa ili kukubali yaishe.
Sasa kwa umbumbu wenu mnadhani na kwa wapangaji wa vyumba vya kulala itakuwa hivyo hivyo, haya ngoja tuone?!
In nature mpangaji huwa anamuomba mwenye nyumba ampangishe nyumba yake, na mwenye nyumba ni uwamuzi wake amkubalie au amkatalie. Kwa hiyo akimkubalia apewe pesa 90% na risiti ya TRA, yani huo mkataba ndio utakuwa umeishia hapo hapo na chumba/Nyumba hatopata, huo ndio ukweli.
Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app