Kocha wa Taifa Stars ametumia vigezo gani kumuacha Kampombe, Zimbwe, Mzize na Sure Boy na kuita kikosini wakalia benchi?

Jones Clean

JF-Expert Member
Jan 8, 2019
393
678
Salaam,

Binafsi nimeshangazwa sana na uteuzi wa kikosi cha Taifa Stars, ambapo nimeona wachezaji ambao wapo kikosi cha kwanza kwenye timu zao (regular players) wameachwa haswa niliotaja hapo juu. Sio hivyo tu wachezaji hao timu zao zipo kwenye mashindano ya kimataifa wakiwalisha timu zao lakini kuna baadhi ya wachezaji hawana timu mpaka sasa mfano Feisal Salum, unamwitaje kwenye timu wakati hajacheza mechi za mashindano kwa muda mrefu? Tunaheshimu uwezo wa Feisal but anahitaji match fitness. Sure Boy alikuwa perfect choice.

Baka na Kibwana kwenye timu zao sio wachezaji regular wanapambania namba Ili wawe wanaanza imekuwaje wanaonza kwe timu zao wameachwa na ila wanaotafuta namba wameitwa?? No way sioni sababu ya Kapombe na Mohamed Hussein kuachwa. (Sijazugumzia wachezaji wa timu za daraja la kati ambao Kwa Sasa hatukupaswa kuwafanyia majaribio hapa ni kufuzu).

Nimesikitishwa zaidi na kocha kumuacha kijana tunaetegemea aje kuwa hazina ya Taifa hili hapo baadae Clement Mzize kijana ambae anahitaji exposure kama hizi ili aanze kujenga confidence katika michuano ya kimataifa katika level ya timu ya Taifa. Unfortunately kocha wetu sijui ametumia kigezo gani kumuacha (Takwimu zake so far zinaongea vizuri). Japo Mzize huwa anatokea benchi ila mpira ni mchezo wa wazi kijana ana potential sana kwa ma-striker vijana wa kitanzania kwa sasa sijaona kama Clement Mzize.

Personally nimeshindwa kumuelewa kocha. aombe Mungu apate matokeo mazuri kwenye hizo mechi vinginevyo atalijua joto la mpira wa Bongo lilivyo.

Anahitaji kutu-prove wrong otherwise atapishana mlangoni na hao aiowaacha

Mungu ibariki Tanzania.
 
Sina uhakika kama hayo ni mashaguo ya kocha maana siasa kwetu ni numero uno katika kila jambo ila binafsi sina matumaini na timu ya taifa.

Ila nakubaliana na wewe kwa mchezaji kama Kapombe. Anacheza katika kiwango cha juu sana sasa hivi.
 
Back
Top Bottom