SIRI: Timu yetu ya Taifa Stars isipokuwepo na promo ya media,ahadi za wanasiasa,kocha akipanga timu mwenyewe bila shinikizo mara nyingi tunafanikiwa

mazaga one

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
2,463
3,932
Mods naomba msiunganishe hii thread!

Leo hii kila Mtanzania akiwa na Furaha baada ya timu yetu ya Taifa Stars Kufuzu Afcon mwakani.

Sasa kila Mtanzania ana uhakika wa Kukaa kwenye TV na kuona Vijana Wetu wakiliwalisha Taifa Huko Ivory Coast...

Sasa tumegundua ya kuwa timu yetu Ili kufanikiwa inahitaji sana kupewa kila mahitaji vyema ya maandalizi kuelekea mechi za Mashindano hayo mwakani, ambapo naimani Kubwa na serikali hii italibeba Hilo jukumu na tutafanya maandalizi mazuri kabisa kwenda kushiriki vyema na sio kuwa wasindikizaji..

Lakini pia nitoe pongezi Kwa TFF Kwa Mafanikio haya ya Soka Kwa miaka hii yote Toka Karia amekuwa Rais, lakini pia nawapa pongezi TFF Kwa kumuacha Kocha Kuwa Huru kwenye uchaguzi wa wachezaji wake anaowaona yeye na hata upangaji wa Kikosi unaona kabisa Yuko Huru.

Mfano Kuna mtu alitegemea Haji Mnoga kuanza? Kuna mtu alitegemea Mudathir Yahya kuwa Benchi?

Hii inatukumbusha ya kuwa Kocha ana taaluma yake na iheshimiwe.

Kingine presha za wanasiasa huwa zinatuumiza sana kwenye kutafuta matokeo ya Muhimu,mambo ya kutembelea tembelea Kambi kila siku huwa wanakosea sana.

Rejea mechi ya Congo na Uganda zile za nyumbani tulifungwa kisa Wanasiasa wetu Hawa.Natoa ushauri Kwa baadhi ya Wanasiasa wetu wamuige Rais Samia yeye anaongea mara moja tu kuwatakia Kheri labda na kutoa Ahadi tu halafu anaishia Hapo.

Nyie Wanasiasa wengine wa Chama Changu hivi mfano nyie wabunge kama mnamuunga mkono Dkt.Samia Leo tumefuzu mkitoa mil 5 Kila mmoja wenu mkongeza kwa Mhe.Rais alizotoa mil 500 si nanyi mngeonekana mpo pamoja na Timu yetu ya Taifa kama mwanzo mnavyokuwaga lakini leo wote mpo kimya tu.

Kuhusu Media za Bongo,Media za Bongo nyingi huwa mnatukosea sana,ninyi ndio watu wa Kukaa kimya kwenye suala la Timu ya Taifa,acheni Ujuaji wa kijinga na ilhali hata ukocha hamjasomea.

Muwe mnawaacha Makocha wafanye kazi zao kama ninyi mfanyavyo,Ujuaji wenu huo Kocha Adel Amrouche naona ashaanza kuwaumbua..

Nakumbuka mechi ya Tanzania Vs Uganda hapa tulifungwa kisa nyie wenyewe kuleta presha ya wachezaji wetu wa Simba Kapombe na Zimbwe Jr kutoitwa, lakini baadae waliitwa hakuna walichokifanya na Kikosi kilivurugika sana Siku hiyo ilhali wao Uganda tulishawafunga Kule Ugenini, Naimani kila mtu anakumbuka Hiki,na ilikuwa siku mbaya sana kwetu Watanzania wengi.

Sisi sio kichwa Cha mwendawazimu,Wachezaji wetu Sasa wanajituma sana,Tumuache Kocha wetu Afanye kazi yake kama ambapo Serikali yetu ya Rais Samia ilibeba jukumu la kumlipa Mshahara basi naye anajua kabisa ana deni Kwa Wapenzi wa Soka la Tanzania.Hongera sana Rais kwa hili kwa kweli.

Ni Mimi Shabiki wa Simba.
Hongera Taifa Stars.
 
Jukumu la Tifa Stars ni la TFF. Ukishaingiza serikali mambo yote yatakwama.

Tunajua nini kinatokea kila wakati serikali ikitia mkono wake. Hakuna kinachofanikiwa.

Chonde chonde hands off kwa serikali kwenye timu yetu !
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom