Mwanasheria na Msimamizi wa Wachezaji Dada Yasmine: TFF iachane upesi na Kocha Adel Amrouche kwasababu zifuatazo.....

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,647
109,036
1. Ni mbaguzi wa Wachezaji

2. Alimkataa Clement ( Warid ) Mzize asiichezee Taifa Stara kwakuwa tu alikataa awe Wakala wake

3. Ni Mtu wa Majungu, Mfitini na Muongo

4. Amechangia pakubwa kwa Mchezaji Simon Msuva kupata matatizo ya kutochezea Timu Kubwa nchini Algeria kutokana na kumkataa asiwe Wakala wake

5. Ana tabia za Kuwatukana sana Makocha Wasaidizi wa Taifa Stars akina Morocco na Mgunda

6. Ni mbabe na hapendi Ushauri

7. Ana dharau

"Nashangaa kwanini hadi sasa Adel Amrouche bado ni Kocha Mkuu wa Taifa Stars wakati ana Mapungufu mengi ambayo hata Wachezaji wenyewe anaowaita na baadhi yao ambao nawasimamia wameshawaeleza sana Viongozi wa TFF. Ni Mtu hatari ndani ya Taifa Stars" amesema Mwanasheria wa Michezo na Msimamizi wa Wachezaji Dada Yasmine.

Huyu Dada Yasmine pia ni Msimamizi wa Sheria wa Wachezaji wengi wa Timu mbalimbali za Tanzania akiwemo Clement Mzize, Feisal Salum'Feitoto' na wale walioko nje barani Afrika kama Fiston Mayele na baadhi walioko Ligi mbalimbali za Ulaya hasa Ufaransa, Ubelgiji na Uingereza ila wenye kutoka Barani Afrika.

Na kwa wale wengine ambao hamjui ni kwamba pamoja na yote haya ila huyu Dada Yasmine pia ndiyo Mratibu Mkuu na Msimamizi wa Sheria kwa Wanamuziki wote wakubwa kutoka Congo DR kuanzia Fally Ipupa, Koffi Olomide, Ferre Gola, JB Mpiana,. Ngiama Makanda Werrason na Felix Wazekwa.

Na hakuna Mwanamuziki yoyote yule wa Congo DR anayekuja kufanya Ziara ya Kimuziki nchini Tanzania na hapitii kwa huyu Dada Yasmine.

Kwa wale mnataka kumuona zaidi tafuteni Video Clip ya Fally Ipupa Live in Dar es Salaam au Koffi Olomide live in Dar au Wenge BCBG live in Dar mwaka 2012 pale Leaders Club mtamuona akiwa nyuma Stejini na mara zote hawa Wanamuziki huwa wanamtaja.

Mwisho nawaombeni kwa Umakini wenu mkubwa Sikilizeni hiki Nilichokirekodi kutoka Kipindi cha Sports Headquarters cha EFM Radio ambapo Dada huyu Yasmine alikuwa akihojiwa Maswali mbalimbali na muhimu yahusuyo Mpira wetu nchini Tanzania, Kocha Mkuu wa Taifa Stars Adel Amrouche na Ustawi mzima wa Wachezaji kama sehemu ya Kusindikiza haya yote niliyoyaandika hapa.
 
Naombeni msaada kila nikijaribu kuiweka ( attach ) hii Sauti ya Kipande cha Kipindi nilichokirekodi EFM Radio hapa inakataa wakati kwa Vitu vingine kama Video au Screenshots nikiweka tu haraka sana zinakubalika.

Kipande cha Sauti nilichonacho ni cha dakika. 13 na Sekunde kadhaa ambapo huyu Dada Yasmine kafunguka mengi mno ambayo nilipenda nanyi pia muyasikie.

Naombeni utaalam zaidi ili niiweke hapa muisikie. Nitawashukuru kwani nimejaribu sana na nimechemka au huenda kuna sehemu ndogo tu naikosea.

Nitawashukuru.
 
Tatizo Una camera yenye simu, utakapoanza kumiliki simu zenye camera huwezi kupata shida hiyo.
 
Tatizo Una camera yenye simu, utakapoanza kumiliki simu zenye camera huwezi kupata shida hiyo.
Unajisikiaje kuchangia Uzi wa Mtu ambaye kwa muda mrefu ulikuwa ukiwataka JamiiForums Moderators na hata JamiiForums Founder Mwenyewe WASINIFUNGULIE tena GENTAMYCINE hili Jukwaa la Michezo?
 
ID zako 18 zote zilikuwepo jukwaani, au niwaambie Mods waziunganishe ndio usikie Raha?
Msalimie MINOCYCLINE
Unajisikiaje kuchangia Uzi wa Mtu ambaye kwa muda mrefu ulikuwa ukiwataka JamiiForums Moderators na hata JamiiForums Founder Mwenyewe WASINIFUNGULIE tena GENTAMYCINE hili Jukwaa la Michezo?
 
Tatizo Una camera yenye simu, utakapoanza kumiliki simu zenye camera huwezi kupata shida hiyo.
Hata haichekeshi sana sana tu inathibitisha jinsi ulivyo Kubwa Jinga na Punguwani Wahed Mwandamizi hapa JamiiForums.
 
Unajisikiaje kuchangia Uzi wa Mtu ambaye kwa muda mrefu ulikuwa ukiwataka JamiiForums Moderators na hata JamiiForums Founder Mwenyewe WASINIFUNGULIE tena GENTAMYCINE hili Jukwaa la Michezo?
Na wewe sijui lini utakua. Kama hutaki aangalie si uache kuandika. Utoto unakuzidi
 
Nitajie makocha watatu tu wazawa wanaofundisha Ligi za ushindani nje ya Tanzania.
Unajisikiaje kuchangia Uzi wa Mtu ambaye kwa muda mrefu ulikuwa ukiwataka JamiiForums Moderators na hata JamiiForums Founder Mwenyewe WASINIFUNGULIE tena GENTAMYCINE hili Jukwaa la Michezo?
 
Na wewe sijui lini utakua. Kama hutaki aangalie si uache kuandika. Utoto unakuzidi
Naona umekuja na ID yako nyingine.

Nauliza tena.......

Unajisikiaje kuchangia Uzi wa Mtu ambaye kwa muda mrefu ulikuwa ukiwataka JamiiForums Moderators na hata JamiiForums Founder Mwenyewe WASINIFUNGULIE tena GENTAMYCINE hili Jukwaa la Michezo?
 
huyo dada yupo sahihi kabisa .

Wizara ya Michezo na Tff hawapo serious kuendesha Michezo Tanzania .
Ingekuwa wapo serious Hata asingekuwa kocha tangu afcon ianze angeshafukuzwa muda mrefu ukiangalia namna timu ilivyofuzu afcon na ile mechi ya Morocco pale kwa mkapa ilikuwa ni 🚩 .
Mechi za kombe la dunia zinakuja lakini utashangaa hakuna maandalizi yoyote ya kuleta kocha wa viwango yotote kutoka nje ya afrika watabaki hawa hawa wazawa wasio na uwezo , wao wanaona mwezi june au July ni mbali sana sana .
Hawana plan yoyote ya kuanza scout ya maana kuona ni wachezaji gani wana uasili uasili wa Tanzania walio ligi kubwa au timu kubwa nje ya Tanzania sio daraja la 4 ,5 au la 7 Kama haji , Terryn na barke.
Hawa viongozi utawaona wapo serious ikifika mwezi mmoja kabla ya mechi kwa kuleta harambee, kuhamasisha redioni, tv , kuteua kamati za kina mwijaku , levo nk Kwenye maandalizi Yao ya zimamoto .
 
Attachments

  • E385F4CA-BEE2-4FD3-BEC3-5D1D9862ADEA.jpeg
    E385F4CA-BEE2-4FD3-BEC3-5D1D9862ADEA.jpeg
    557.6 KB · Views: 4
Back
Top Bottom