Black na Green mamba ni kweli wote wana sumu kali sana lakini ni kati ya nyoka waoga na wapolea sana duniani,namaana gani?ni nadra sana kukutana na black mamba,yeye akikiuona anakukwepa,jificha au akimbie,otherwise umkanyage au umguse!...hawa kule moshi kipindi cha baridi wanakimbiliaga ndani ya nyumba,kama hamna tiles au carpet atajificha huko ndani na itakuwa nadra sana kumuona na anaweza toka akaishia zake hata baada ya miez bila nyie kujua,green mamba moshi ndio wako wengi,haswaa baada ya kilimo cha kahawa kuporomoka,yale madawa tuliyokuwa tunapiga shambani yalikuwa makali na nyoka walikuwa hawakai,lakini sasa hivi ikifika saa sita mchana upande mahali pa juu ili uione fensi yenu ya buganvilia kwa juu lazma umuone ''ISALE'' kama wachaga wanavyomuita,anafanana sana na majani na ukimuona dk,ya pili anakupotea,kuna jamaa alimkanyaga usiku black mamba akamuuma,hakufa,tulichukua wembe fasta tukamkata kidogo kidogo eneo alilongatwa alafu jamaa mmoja akavuta kwa mdomo kama mara ishirini ivi tukamuwaisha hospitali usiku ule kufika baada ya kama 2hours mguu umevimba kweli lakini alipona!...cha msingi ukiumwa na nyoka jitaidi kujua ni nyoka aina gani amekuuma sababu sumu zao zinatofautiana na tiba ni tofauti!