Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Bro ni nadra sana kumuona pamoja na maeneo kama tabora, itigi, manyoni kuwa na koboko wengi ila waliobahatika kuwaona wanaweza kuwa wachache mno
Hawa nyoka wapo. Ila si busara wakawa kila sehemu. Ni wakali na wakatili sana. Kwenye majumba ya kuhifadhia nyoka wapo. Arusha na Mikumi nimeona hawa nyoka
 
Dag
mimi na nyoka haziivi kabisa... na kingine ni vile sipendi beef nao. so kama tunakutana napenda kila mtu ashike hamsini zake... nlishawahi kutana na nyoka arusha kipindi flani barabaran akanipa tu hi nami nikampa hi nikalala mbele.. siku nyingine tena napita hiyo njia naye alikuwa anakatiza kwenda kwenye mishe mishe zake... basi nikaona oooooh.... isiwe tabu nikahamia njia nyingine ya mbali sana.maana hii ilikuwa ni short cut lakini nilipoona two times nakutana na mchizi yule yule nikajua hapo karibu anaweza kuwa na maskani au hata jamaa zake wanaishi eneo hilo. nami najijua siwezi beef nao hawa wadudu hata akiwa ame dead mimi simwezi. nina nyokaphobia. ukinambia njia ya huku kuna simba na huku kuna nyoka chagua kwa kupita ntapita nikapambane na simba but si nyoka...

mimi na nyoka haziivi kabisa... na kingine ni vile sipendi beef nao. so kama tunakutana napenda kila mtu ashike hamsini zake... nlishawahi kutana na nyoka arusha kipindi flani barabaran akanipa tu hi nami nikampa hi nikalala mbele.. siku nyingine tena napita hiyo njia naye alikuwa anakatiza kwenda kwenye mishe mishe zake... basi nikaona oooooh.... isiwe tabu nikahamia njia nyingine ya mbali sana.maana hii ilikuwa ni short cut lakini nilipoona two times nakutana na mchizi yule yule nikajua hapo karibu anaweza kuwa na maskani au hata jamaa zake wanaishi eneo hilo. nami najijua siwezi beef nao hawa wadudu hata akiwa ame dead mimi simwezi. nina nyokaphobia. ukinambia njia ya huku kuna simba na huku kuna nyoka chagua kwa kupita ntapita nikapambane na simba but si nyoka....
Dah 'Nyokaphobia' 🙌🏾😅
 
Kuna jamaa kwenye chanel flani ivi anawakamata hawa nyoka kirahisi mno , nafikiri mna wa over rate japo uwezo wanao.
 
Sio yule jamaa na mkewe kweli! Kwenye kipindi cha snake in the city Mkuu' maana na wao si haba against thy black mambas
Yah wamejichora tatoo za majoka ivi , hao nyoka ni wakali kweli ila sio kihivyo ! Kiasi cha kutisha binadamu.
 
Kuna kipindi nilikuwa Kigoma maeneo ya Uvinza nilinunua eneo heka 2 sasa naskia maeneo Yale wapo Koboko kibao Mara kibao nilikuta ngedere, nyani wamekufa wenyeji wakasema ni koboko ndo wauaji hadi sasa sijarudi kucheki Shanna hili naogopa
 
View attachment 344445
MAMBAS ni aina ya nyoka wakali wapatikanao ktk dunia ya leo. Ni nyoka wenye sumu kali na wenye kasi ktk mwendo na wana sifa ya kutaga mayai (oviparous).

Kuna aina mbili za mambas :
1. GREEN MAMBAS.
2. BLACK MAMBAS.

Green mamba wanasumu aina ya NEUROTOXIC na HAEMOTOXIC. Wanaishi miaka 12 hadi 14 (makadirio kulingana na takwimu za sayansi) wanataga mayai na kuanguliwa kwa siku 80 hadi 90.

BLACK MAMBA pia wanauwezo wa kupanda miti wakati wakitafuta chalula na wanaurefu kati ya sentimita 220 hadi 320. Ni kati ya nyoka wenye sumu kali wapatikanao Afrika. Wanataga mayai kati ya 12 na 18,na kuangua kati ya siku 80 hadi tisini.

Mambas ni nyoka wakali na wenye kung'ata zaidi ya mara moja kwa sababu meno yao hayang'ooki wakti wakigonga kitu. Meno yanayong'ooka kwa nyoka yanaitwa FRONT FANGED MOVABLE na yasiyong'ooka yanaitwa FRONT FANGED FIXED.

Iwapo nyoka huwa wata kung'ata utaweza kuishi kati dakika 20.
View attachment 344446

=========

@Ipycalypse,

Habari wanaJF,

Leo nataka tufahamishane kuhusu nyoka huyu hatari kwa sisi waswahili tunamuita KOBOKO lakini kwa lugha ya kiingereza huitwa Black Mambas

Black mamba ni moja ya nyoka hatari sana katika dunia. Nyoka hawa hupatikana katika sehemu Mashariki na Kusini mwa Afrika. Black mamba anaweza kuishi katika aina mbalimbali za mazingira: savanna, mabwawa, misitu na maeneo ya miamba. Makazi yoyote ambayo hutoa joto na unyevunyevu ni sehemu nzuri ya kuishi Black Mamba. Kutokana na uharibifu wa mazingira na kuongezeka kwa kilimo, makutano kati ya Black Mamba na binadamu yameongezeka zaidi.


1- Black mambas ni nyoka mwenye sifa ya urefu anaweza kufikia miguu 14 urefu na 1.58757 katika uzito.

2- Black mamba ana mwili mwembamba kufunikwa na ngozi yenye magamba kama ilivyo kwa nyoka wa jamii nyingine, Pamoja na wao kujulikana kwa kiingereza kama Black mambas lakini hawana rangi nyeusi katika ngozi na rangi ya mwili inategemea makazi yao na inaweza kuwa ya kijani, kijivu au njano.

3- Black mambas ni jina lake kwa sababu sehemu ya ndani ya vinywa vyao ni nyeusi kabisa. Black mamba kuonyesha kinywa chake cheusi wakati anakabiliwa na hatari.

4- Nyoka huyu huanza kutanua shingo yake lakini sio kama afanyavyo COBRA na hutoa sauti kama ile ya tairi likiwa inatoka upepo na hii ni ishara nyingine kwamba kiumbe hutayari shambulio. Ukiona amena moja ya hizo ishara unashauri wa usifanye chochote kwasababu kwa kasi aliyonayo hutaweza kumuwai kifupi tulia mpaka hasira zishuke na ajiondokee narudia usithubutu kujifanya unafurukuta matendo yako hayatawahi tendo lake.

5- Ingawa nyoka huyu amebeba sifa ya kuwa nyoka mjeuri na mkali sana, lakini nayeye hujaribu kutoroka kabla mashambulizi lakini hushambulia kwa ukatiri sana ikibidi. Kumbuka kwa mtulivu ukikutana nae

6- Sasa upande wa sumu hapa ndipo patamu Black mamba ana aina mbili ya sumu zinazozalishwa katika mwili wake moja ni huitwa Neuro – hii huathiri mfumo wa neva na nyingine ni Cardio-toxin hii huathiri mfumo wa moyo na sumu hizi zinaweza kuua binadamu chini ya dakika 20. Pia imethibitika kuwa matone mawili ya sumu yake inaweza kuua.

7-Black mamba anatumia sumu kuwinda aina mbalimbali za ndege na wanyama wadogo. Na hutumia kama kitoweo chake

8- Black mamba anaishi katika mashimo ya miti na katika mashimo ya miamba. Pamoja na kiasi kikubwa cha sumu kali sana aliyonayo, lakini hana ujanja mbele ya Nguchiro na Mbweha, na Nyegere.

9- Black mamba hutembea haraka sana akiwa juu ya ardhi. Anaweza kusafiri umbali mrefu kwa kasi ya maili hadi 12 kwa saa. Hivyo usijaribu kukimbia atakufukuza mpaka akugonge sehemu ya mwili wako.

10- Jike hutaga mayai kati ya 10 na 25 katika kiota juu ya ardhi. Joto ni muhimu kwa ajili ya incubation ya mayai. Na mayai hujitotoa baada ya miezi 3. Na vijinyoka hivyo vichanga huanza kujihudumia kwa kila kitu na huwa na sumu ile ile kama ya nyoka mkongwe hivyo usije ukadharau.

11- Black mamba anaweza kuishi hadi miaka 11 katika pori na hadi miaka 12 katika kama atafugwa.

PIA Unaweza SOMA: Ni kwanini nyoka aina ya Koboko anaogopeka kuliko Simba na Chui maeneo ya porini? - JamiiForums
Hii story ya kitambo mno
 
Back
Top Bottom