KKKT ni kanisa kubwa kuliko mtu, Kiburi kimemponza Mchungaji Kimaro

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,333
24,227
Kanisa ka Kiinjili, la Kilutheri Tanzania, KKKT ina historia , na ni taasisi ya muda mrefu.

Ina taratibu na kanuni zake , mchungaji au mtumishi atafanya mbwembwe zake zoote lakini lazima awe ndani ya utaratibu wa Kanisa.

Mtumishi akiwa na Karama au upako lazima aongozwe na hekima, na siyo jeuri na kiburi cha kufanya na kusema atakavyo kwa kujiona yuko juu ya taratibu zilizowekwa.

Hakuna Mtumishi aliye juu ya KKKT kama taasisi.
KKKT ni kubwa kiasi kwamba hata askofu hayupo juu ya KKKT.
Sasa hivi tunaona watumishi wanao lipatia kanisa au usharika mafanikio.
Cha kushangaza mafanikio yao yanawapanda kichwani na kuanza jeuri, dharau na kiburi.

Sababu kubwa ni ukubwa wa wafuasi binafsi walionao.

Mwaka jana katika Dayosisi ya Konde , Askofu wake Dr Mwaikali alivuliwa uaskofu. Wengi wa tulioifuatilia ile ibada ya kumvua Uaskofu tulisononeshwa na ukaidi wa Askofu Mwaikali.

Leo, Dayosisi ya KKKT Konde na kanisa linaendelea.

Kama mtumishi anajiona ana karama na unapendwa na watu wengi, bado una wiwa kufuata taratibu za Kanisa.

Kinyume na hapo kwa karama zako anzisha taasisi yako,

Jeuri na kiburi alichoanza kuonyesha hadharani huyu Dr Rev Eliona Kimaro ni upungufu wa maono ya kutoona mbali.
Kuna fununu kuwa Kimaro alionywa mara kadhaa juu ya tabia yake binafsi kujiona yuko juu ya utaratibu, akakaidi, na wakati mwingine anajibu hadharani, na clips zipo.

Sasa inaelekea anavuna alichopanda.
1674132981328.jpeg

Waumini(predominantly women) aliowalea Rev Dr Kimaro wakiandamana.
Mpaka unajiuliza alipanda roho gani ndani yao?
"WE LOVE YOU DADY"
 
Rubbish tupu. Kwa taarifa yako tu, kanisa hai lenye kumwabudu Mungu katika roho na kweli huwa halizuiliwi na mipaka, mapokeo ya kibinadamu. Refer kina Petro na Yohana baada ya kumponya yule kiwete pale kwenye mlango mzuri wakati wanakwenda kusali.

Viongozi wa dini wakawaita na kuwapiga biti mbaya kabisa, unajua walichosema? Walijibu "IMETUPASA KUMTII MUNGU, KULIKO WANADAMU". Wachungaji wa kweli husimama na kweli, no matter what.
 
Alionywa kwa kosa lipi?

Waliogopa tu kuwa siku akisimama kugombeya U Askofu atawabwaga wote.

Yupo huyo mkuu wa jimbo naamini ana lenga kuwa Askofu, anadhoofisha wengine nguvu.

Je mmesahau huyu mkuu wa jimbo kufikia hapo alifanya kitu gani?

Na hapa wanajiandaa kumdhoofisha pia Matsai
 
Rubbish tupu.Kwa taarifa yako tu, kanisa hai lenye kumwabudu Mungu katika roho na kweli huwa halizuiliwi na mipaka, mapokeo ya kibinadamu. Refer kina Petro na Yohana baada ya kumponya yule kiwete pale kwenye mlango mzuri wakati wanakwenda kusali.
Viongozi wa dini wakawaita na kuwapiga biti mbaya kabisa, unajua walichosema?.Walijibu "IMETUPASA KUMTII MUNGU, KULIKO WANADAMU". Wachungaji wa kweli husimama na kweli, no matter what.
Kutokuwa na mipaka ni anarchy.

Na kama unachosema ni kweli basi mshaurini Kimaro aondoke KKKT akawe kama Yohana mbatizaji, aliyekuwa sauti iliayo nyikani.
 
Back
Top Bottom