KKKT labariki unywaji wa Pombe

KKKT labariki unywaji wa Pombe

Habari yako ni ya kinafiki na kizushi sana.

Kumbuka vita yako ni ya kimwili na vita ya Wakristo ni ya kiroho.

Utashindwa na kaibika
 
Kweli hizi ni nyakati za mwisho kanisani badala ya kuhubiriwa injili watu wajiandae na hukumu ya mwisho wamrudie Muumba wao inahubiriwa pombe?

Yesu nipe uvumilivu figisu ni mob.
 
Unajua tofauti kati Kilevi na ulevi au Pombe na ulevi?

Kama hujui. Cheki Wasabato wanavyoangaika kukwepa kilevi. Majani ya chai, soda cocacola nk.

Kama unakunya soda Cocacola, majani ya chai nk vina kilevi hivyo.

Hii itakusaidia kidogo.

Ulevi, ujulikanao pia kama uraibu wa pombe, ni ulemavu tegemevu wa kudhuru. Dalili zake ni unywaji pombe kupindukia bila udhibiti pombe licha ya madhara yake hasi kwa afya ya mnywaji,, mahusiano na hadhi yake machoni pa jamii. Kama matatizo mengine ya kiafya, ulevi ni mojawapo ya magonjwa yanayoweza kutibika.neno " ulevi" limetumika kwa muda mrefu tangu kubuniwa mwaka wa 1849 na Magnus Huss, ila katika nyanja ya utabibu istilahi hii iligeuzwa kuwa "utumiaji pombe vibaya" na " utegemezi pombe" katika miaka ya 1980 DSM III.Aidha mwaka wa 1979 kamati ya wataalamu ya Shirika la Afya Duniani haikupendelea kutumika kwa neno "ulevi" kama istilali ya kiafya, huku ikipendekeza dalili za "utegemezi pombe". Katika karne ya 19 na mapema karne ya 20, utegemezi pombe uliitwa dipsomania kabla ya kubatilishwa kuwa ulevi"

Source: wikipadia.

Bila shaka utakuwa umeelewa.
Najua na haibadilishi kauli
 
Dini za kuuunga unga ndio zilivyo,jana pombe haramu,leo inafaa,kesho kunywa lakini usinywe sana.
Pombe ina madhara hata kama unatumia kiasi kidogo,kwa afya ya binadamu,ndio maana imeandikwa Pombe ni "hatari kwa afya yako".
Katika uislamu kila kilicho haramu ni kwa waislamu wote,hakuna kutofautiana.
Sasa dini ya kuunga ni Ukristo au uislam unaowakataza watu kunywa pombe ILA bado inawaahidi watakaofanikiwa kuingia peponi watakutana na mito itiririshayo Mvinyo?

Bado na zile ahadi zingine...
 
Pombe inasababisha ulevi pale inapozidishwa na mtumiaji

Pia pombe inaweza kitumiwa kidogo kama dawa na si kilevi

Unalijua hilo?

Huwezi kunywa pombe bila kukupelekea kutenda dhambi. Pombe = dhambi
 
Pombe inakatazwa!
Isaya 28:7 kileo humfanya mtu kumkosea Mungu.
Hosea 4:11 pombe huondoa fahamu,ndiyo maana wanajinyea
Hosea 4:18 pombe huchochea zinaa.
1kor 6:9-10 walevi mbinguni si kwao
waefeso 5:19-21 matendo amboyo ni dhambi ni pamoja na ulevi wa mvinyo.HUKUNA sehemu yeyote ya kuverify kwamba timotheo aliambiwa anywe pombe kwa kutibu tumbo.
Wewe kweli ni Mbojo

Umezungumzia Kilevi, kilevi ni pale pombe inapokuwa na uwezo wa kulewesha !

Pombe inamlewesha mtu aliyezidisha, kama haijanilewesha nikalewa nitawezaje kufanya maovu?

Itawezaje kuniondolea fahamu?

Usikariri tu maandiko pia elewa.
 
Huwezi kunywa pombe bila kukupelekea kutenda dhambi. Pombe = dhambi
Huo ni Uongo na Umbea

Kwanini siwezi kunywa pombe bila kutenda dhambi? Mbona nakunywaga na sitendi dhambi?
 
KKKT labariki unywaji wa Pombe

ASKOFU Mkuu wa zamani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa, amebariki rasmi unywaji wa pombe katika kanisa hilo kongwe nchini, anaripoti Mwandishi Wetu.

Akizungumza katika mkutano wa 33 wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, wiki iliyopita, huko Seminari ya Kisarawe, mkoani Pwani, Askofu Malasusa amesema, ” katazo la unywaji wa pombe lililetwa na wamisionari, lakini pombe kama pombe haina tatizo.”

Askofu Dk. Malasusa, ndiye askofu mkuu wa kanisa la KKKT, Dayosisi ya Mashariki na Pwani. Askofu Dk. Malasusa alikuwa akikamilisha majibu yaliyotolewa na Askofu Keshomshahara wa kanisa hilo, Dayosisi ya Bukoba aliyoyatoa kwa swali lilioulizwa na Prof. Mjema wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Katika swali lake, Prof. Mjema alihoji, nafasi ya pombe katika dhana ya Mtume Paulo anapozungumzia kutiwa unajisi kwa vyakula na vinywaji wanavyokunywa wakristo.
Alitaka kupata ufafanuzi wa msiamo wa kanisa juu ya msemo wa “kimuingiacho mtu na kimtokacho mtu.” Awali katika majibu yake, Askofu Keshomshahara amesema, “pombe ni kinywaji tu kama vinywaji na vyakula vingine” na kwamba pombe inapaswa kutumiwa kwa kiasi na kwamba “hata sakramenti takatifu ya Meza ya Bwana inayotumika kanisani mwao ni pombe.”

Baada ya majibu hayo, ndipo Askofu Dk. Malasusa aliposisitiza kuwa makatazo ya pombe kanisani ni “busara ya wamisionari wa kwanza walioleta injili Afrika baada ya kuona Waafrika walikuwa wakilewa bila kiasi na kukosa ustaarabu.”
Aliendelea kusisitiza kuwa “pombe itumike kwa kiasi na hasa kwa wakristo wachanga.”

Majibu hayo ya maaskofu yaliwachanganya wajumbe wengi na kusababisha mijadala baada ya mkutano. Mjumbe mmoja aliyeongea na gazeti hili huku machozi yakimlenga anasema, “nimesikitika sana kuona maaskofu wetu wanalipotosha kanisa. Hivi kweli sakramenti ni pombe?” Dayosisi ya Mashariki na Pwani kupitia katiba yake, inapiga marufuku wazee wa kanisa kutomiliki vitega uchumi vinavyouza pombe.

Aidha, sherehe zote za kanisa haziruhusiwi kuwa na pombe huku baadhi ya waumini wakipewa adhabu na wachungaji wao kwa kunywa pombe au kufanya biashara ya pombe. Msimamo wa maaskofu hawa wawili unaliweka kanisa Zima la KKKT katika njiapanda ya kulifafanua jambo hili huku waumini wengi wakitishia kuhamia makanisa ya kiroho kukimbia upotoshaji wa wazi wa maakofu wa KKKT. Mkutano huo wa 33 ulijaa vitimbi vingi vinavyoonyesha dayosisi hiyo haiko shwari.

Akiongea kwa uchungu kwenye mkutano huo, Mchungaji wa kanisa hilo usharika wa Kigogo, jijini Dar es Salaam, Richard Ananja alimtaka Askofu Dk. Malasusa kuachia kiti mara moja kwa kuwa amepoteza sifa kwa kashfa za ngono zinazomkabili.

Amesema Dk. Malasusa anakabiliwa na tuhuma nzito za matumizi ya madaraka, uvujaji wa fedha za dayosisi, hujuma kwa Benki ya Maendeleo, kugushi vyeti ya elimu, ukabila, chuki na visasi kwa wachungaji.

Hivyo basi, ili kulinda hadhi na heshima ya kanisa na yeye binafsi, ni vema Askofu Malasusa “akaachia ngazi kwa hiari, badala ya kusuburi kufukuzwa.”
Hoja hiyo ilipozwa na katibu mkuu wa Dayosisi hiyo, Godfrey Nkini aliyedai kuwa kamati ya maadili inashughulikia tuhuma hizo.

Siku moja kabla ya kufungwa kwa mkutano, mchungaji wa kanisa la KKKT, Usharika wa Kibaha, Amani Lyimo katika mahubiri ya ibada ya asubuhi, aliushambulia utendaji wa Askofu Dk. Malasusa kuwa ni wa uonevu, usijali kweli, uliojaa udhalimu, ubabe na matumizi mabaya ya madaraka.
Amesema uongozi wa Dk. Askofu Malasusa unakomoa watu kuliko uongozi wowote uliopita katika dayosisi hiyo.

Kabla ya kufungwa kwa mkutano huo, Mwenyekiti wa kamati ya maadili wa dayosisi hiyo, Ibrahim Kaduma, alidai kuwa tuhuma juu ya Askofu Dk. Malasusa, si za kweli na zinachochewa na gazeti moja (hakulitaja) lakini akadai ni chuki ya uislamu dhidi ya kanisa.

Maelezo hayo yalipingwa na wachungaji wengi hali inayoonyesha kuwa Askofu Malasusa hayuko vizuri na wachungaji wake. Wachungaji walidai kamati imeleta “majibu mepesi” kwa tuhuma za ngono zinazomkabili Dk. Malasusa na kwamba kinachobakia sasa wao kumwaga hadharani yaliyositiriwa kulilinda kanisa, alisisitiza mmoja wa wachungaji wa kanisa hilo mwenye taaluma ya sheria.

Katika hatua nyingine, ajenda ya marekebisho ya katiba ya dayosisi hiyo, iliburuzwa ili kumwepusha Askofu Malasusa na hoja ya ukomo wa madaraka yake. Siku za karibuni, Askofu Dk. Malasusa amekumbwa na tuhuma mfululizo, zikiwamo matumizi mabaya ya madaraka, ngono na ubaguzi.

Hata hivyo, Dk. Malasusa amekuwa akijibu tuhuma hizo kwa kuwanyooshea kidole waumini wanaotoka mikoa ya Kaskazini kuwa wanamsakama kwa vile katika uchaguzi mkuu uliyopita, limuunga mkono Rais Magufuli na kumsaliti swahiba wake wa miaka mingi, Edward Lowassa.

Chanzo: Mwanahalisionline
mbona hii habari ni kama iko outdated?

hii habari imepikwa kwa makusudi maalumu. huu ni ufaatani!!
 
Ni sawa na zuzu anayesema Gari ni Ajali..
mtu anapokunywa pombe lengo lake alewe,akilewa anapata uwezo kufanya au kusema mambo bila kujidhibiti. Busara na hekima inakuwa haipo katika kufanya uamuzi sahihi unaotakiwa
 
Pombe ni hatari kwa afya yako MADHARA YA POMBE KIAFYA. | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today
Iki tukuelewe vizuri kwamba humchukii na huna bifu na Malasusa na kwamba hujatumwa

Hebu tuambie haya:-

Hiyo Tuhuma ya ngono kumuhusu Malasusa ni Ipi? Una ushahidi uuweke hapa?

Huo Ubaguzi wa Malasusa ni Upi? Hebu thibitisha hapa mfano wa ubaguzi wake.

Jibu hayo tu.

Mkuu ungejua imani yangu ,ungejishangaa kwanini umesema hivyo,miaka kadhaa nikisali ukonga hapo kanisa fulan nilienda kushiriki meza ya bwana,ile kumaliza kupiga ule mnvinyo nilipepesuka na hata nikasahau nilipokuwa nimekaa,mpka baada ya muda ndo nikagundua

Ulitaka ulewe madaraka?

Hapana! Hakuna mahali imeandikwa pombe ni hatari kwa afya yako..

Imeandikwa

ULEVI NI HATARI KWA AFYA YAKO
 
Hata shetani lazima amshangae huyo askofu. Hivi hata kwa kuangalia madhara ya pombe kijamii tu haitoshi mtu kuelewa kuwa pombe ni kitu haramu ambacho Mungu mtakatifu anayejali ustawi wa viumbe wake ansingewez kuruhusu pombe kuwa sehemu ya mpango wa chakula au kinywaji kwa viumbe wake. Hii haihitaji kuwa mtaalamu wa Biblia kulielewa bali common sense. Wanaounga mkono unywaji wa pombe ni mateka wa Shetani ambao wamepotoshwa na mafundisho potofu ya kanisa Katoliki na mabinti zake yanayohalalisha pombe kwa kutafsiri Biblia kulingana na tamaa zao.
Ni pombe tu ina madhara kati ya vitu vinavyoliwa? Vipi kuhusu red meat?
 
Shida ni kuwa watu wanachanganya neno POMBE na neno ULEVI. Kilicho dhambi ni ulevi na sio pombe. Pombe ikitumika vizuri kwa makusudio yake ni jambo la kheri kabisa kwa mwanadamu, lakini ikitumika kama ulevi ni katazo kwa Mungu.
Hata Madaraka yaweza kutumika kama ulevi na kuleta madhara jee madaraka nayo ni dhambi? Kwa sababu Pombe na Madaraka vyote ukivitumia vibaya vinakuwa ulevi!
Kunywa pombe kistaarabu, burudisha nafsi yako. Na hasa kwa wakati huu ambao mambo ni vululu vululu kiuchumi basi ukipiga mbili tatu zako taratibu unajikuta unaburudisha ubongo na kukuepusha na ghadhabu au chuki kwa wengine.
Kama mmeweza kuhalalisha ushoga hats pombe mtahalalisha! Kkkt sio kabisa bali Ni NGO.
 
Kama kweli kasema huvyo, basi ndio haya makanisa hayakui kiroho.
 
mtu anapokunywa pombe lengo lake alewe
Kwanini unataka wapandikiza watu uovu? Aliyekuambia mtu akinywa pombe lengo lake ni kulewa ni nani..??
,akilewa anapata uwezo kufanya au kusema mambo bila kujidhibiti.
Ok! Na kama hajalewa??? Hivyo unakubaliana na mimi hayo yote uliyoyasema hapo ili yatokee lazima ulewe sio....,,,yani unywe kupita kiasi....Je! Kama hajalewa...??

Busara na hekima inakuwa haipo katika kufanya uamuzi sahihi unaotakiwa
Kwahiyo busara na hekima huondoka pale unapolewa ila si kunywa pombe..

Unajua ndugu, unafiki ni kitu kibaya sana...Utazunguuka weweee, ila tunarudi kwenye point ile ile pombe na elevi ni vitu viwili tofauti
 
Back
Top Bottom