KIWIRA na MCHUCHUMA: A Campaign To Reclaim...

KIWIRA na MCHUCHUMA: A Campaign To Reclaim...

Babu Ataka Kusema!

Naungana na wewe kwa Ngeleja kukiri kwamba Mkapa amerudisha Kiwira nin ushindi mkubwa kwa wapiga kelele hapa jamii wakiongozwa na M.M.Mwanakijiji na makala zake kwenye gazeti la Mwanahalisi.

Itabidi tujiandae kuchukua madaraka siku si nyingi zijazo. Tukusanye pesa tufungue kesi ya kuishitaki serikali ya CCM kwa Ujambazi wanaofanya. Kwa kurudisha ni ushahidi tosha kwamba waliipora na kwa sababu hawajalipa hata senti tano basi tungojee kama huyo mwanasheria feki kwa jina la Bill Ngeleja endapo atawafidia na yeye tumwunganishe++ Yes

Mkapa amekopa pesa zaidi ya shillingi bilion 34 kutoka NSSF na CRDB kwa ajili ya kuimarisha mradi wa Kiwira, ameziweka wapi? Mikopo yote miwili alidhaminiwa na serikali! halafu serikali hiyo hiyo inataka kulipa fidia? Hili ni jambo la hatari sana! Ni kiama dhidi ya watanzania wanaoteseka kila siku kutokana na seriakli kutumia vibaya rasilimali za umma.
 
wanajaribu kumsafisha mkapa kwa kubeba mzigo wake..serekali ni ya wananchi na sio viongozi..JK is more like FRANK LUCAS in american gangster movie...he will try to get what he wants nomatter what.kwamba yuko radhi kuwakumbatia wakina RA,EL,BMW na wengine wengi kwasababu wamemweka hapo alipo na wataendelea kumsaidia kuwepo pale.kama anavyodai,hana ubia na kwamba usemi wake ni wa mwisho.hawa wote wamesahau kitu kimoja,kwamba sisi wote ni binadamu sawa na wote tunastahili maisha bora hapa duniani,na pia dunia ni sehemu ya kupita tu,nomatter how much money you get sikumoja utakufa kama wengine....I pray to GOD that,nyie wote mnaoiba pesa za nchi,kuweka matabaka kati yetu,kujilimbikizia umaskini,kutreat wananchi wengine kama wajinga na wasioelewa mnayoyafanya na kudanganya watu, you will all burn in hell.and one thing that i know for sure is that,u will not cheat us forever.
 
Date::7/23/2009
Serikali yajitwika mzigo wa Kampuni ya Makaa ya mawe Kiwira

Na Kizitto Noya, Dodoma
Mwananchi
​

SERIKALI imesema kutokana na kasoro nyingi zilizojitokeza katika ubinafsishaji wa Kampuni ya Kiwira Coal Mines Limited (KCML), ikiwamo hisia miongoni mwa jamii kuhusu ubinafsishaji wake; imeamua kuchukua hisa zote za mgodi huo na kuilipa kampuni ya KCPL gharama zote zilizotumia kuuendesha.

Kauli hiyo iliyotolewa kwa maandishi ya kurasa saba na kusomwa jana bungeni na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja imeonyesha kuwa serikali imeamua kubeba mzigo wa mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira ambao unamilikiwa na familia ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na Waziri wa zamani Nishati na Madini, Daniel Yona.

"Kwa kuwa kumekuwapo na kasoro katika uendeshaji wa mradi huu zilizosababisha hisia mbalimbali miongoni mwa wananchi na kwa kuwa hisia zilizoibuka kuhusu ubinafsishaji wa kampuni ya KCML (baadaye ilibadili jina na KCPL), zimeathiri mazingira ya kampuni kuweza kutekeleza na kutimiza malengo yake kama yalivyoainishwa kwenye mkataba na hivyo kuiathiri nchi..., tumeamua kuchukua hisa zake zote," alisema Ngeleja.

Alisema kampuni hiyo kutokana na matatizo yaliyojitokeza ilishindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi wapatao 500 kwa zaidi ya mwaka sasa inayofikia Sh1.5 bilioni.

Hivyo, sekta ya nishati kwa mashauriano na serikali, kampuni ya KCPL imeona ni busara irudishe mgodi wa Kiwira na mradi wa kuchimba makaa ya mawe na kuzalisha umeme serikalini kwa makubaliano kwamba, serikali itarudisha gharama zilizotumiwa na KCPL endapo zitathibitika kwa kuwa za kweli.

Baada ya uamuzi huo, serikali imeanza mchakato wa kupata uratatibu muafaka wa kuendesha mradi kama ilivyokusudiwa kwa kuangalia fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuingia mkataba wa uendeshaji na kampuni itakayopewa mamlaka ya kujenga na kuuendesha mradi huo.

"Chini ya mkataba wa uendeshaji, mkandarasi atapewa jukumu la kujenga uwezo wa mashirika ya STAMICO (Shirika la Madini) na Tanesco ili kuyawezesha kumiliki na kusimamia mradi huo," alisema.

Kwa mujibu wa Ngeleja, hatua ya awali ya mpango wa serikali kuanza
kuundesha mradi huo zimeanza kwa kuhakikisha kuwa wafanyakazi waliopo wanalipwa haki zao zote na kuwawekea mazingira mazuri ya kuendelea na kazi.

"Serikali pia imezungumza na serikali rafiki ya China iliyoanzisha na kuendesha mradi huo ili kupata mkopo wa kuufufua na kuhakikisha mradi wa kuzalisha umeme wa MW 200 unakamilika mapema iwezekanavyo," alisema.

Akizungumzia suala la Rais Mstaafu Mkapa ambaye aliomba kumiliki hisa 200,000, kupitia kampuni yake ya ANBEN Limited, alisema kuwa kiongozi huyo wa zamani alinyang'anywa hisa hizo Januari 10 mwaka 2005 baada ya kushindwa kuzilipia.

"Mheshimiwa Spika, tarehe 10 Januari, 2005, (Siku 13 tangu kuanzishwa kwa TPR), ANBEN Limited iliondolewa kuwa miongoni mwa wamiliki wa hisa kwa vile haikuweza kulipia hisa ilizokuwa imechukua wakati wa usajili wa TPR.

Hivyo wamiliki wa TPR waliobaki walikuwa ni DevConsult International Ltd, Universal Technologies Ltd, Choice Industries Ltd na Fosnik Enterprises Ltd zote zikiwa na hisa 200,000," alisema Ngeleja.

Hata hivyo wanahisa katika kampuni hiyo ni Nick Mkapa, Fostar Mkapa na B. Mahembe ambao wanamiliki Kampuni ya Fosnlid wakati kampuni ya Devconsult LTD wamiliki wake ni D.Yona na Danny Yonna J.R.

Awali akitoa historia ya mradi huo, Ngeleja alisema ulianza mwaka 1983 na kukamilika 1988 kwa gharama ya Sh4.29 kwa ushirikiano kati ya Serikali ya China na Tanzania.

Alisema KCML iliyosajiliwa Oktoba 3 mwaka1988 kama kampuni tanzu ya Stamico, iliyoundwa kuendesha shughuli za kuchimba makaa ya mawe na kuzalisha umeme kutoka mgodi wa Kiwira kwa matumizi yake na wilaya za Rungwe, Ileje na Kyela mkoani Mbeya.

"Uchimbaji wa makaa na uzalishaji wa umeme ulianza rasmi Novemba 1988 ambapo makaa yaliyochimbwa yalitumika kuzalisha umeme kwa ajli ya matumizi ya mgodi wenyewe.

Ziada ya makaa ya mawe yaliyopatikana iliuzwa kwa kiwanda cha kutengeneza saruji cha Mbeya na Southern Paper Mills (SPM) kilichopo Mgololo, Iringa na ziada ya umeme iliyopatikana iliuzwa kwa Tanesco, alisema na kuongeza:

"Kufuatana na upembuzi yakinifu kiasi cha mashapo ilikadiriwa kuwa tani milioni 35.14 na uhai wa mgodi ulikadiriwa kuwa miaka 65 kuanzia mwaka 1988 kwa kasi ya uchimbaji wa kati ya tani 150,000 na 300,000 kwa mwaka.

Hata hivyo, KCML haikuwahi kufikia makadirio hayo kwani kiwango cha juu cha uzalishaji kilikuwa tani 80 tu kwa mwaka.

Kwa mujibu wa Ngeleja, kutokana na KCML kujiendesha kwa hasara, serikali iliubinafsisha mgodi huo kwa kampuni ya China Hunan International Economic and Technical Cooperation Corporation (Chitec) kwa hisa 62 na yenyewe (serikali) ikibaki na hisa 38.

Alisema uchambuzi baada ya ubinafsishaji huo ulibaini kuwa mradi wa makaa ya mawe wa Kiwira na soko lake haukuwa na manufaa kibiashara hivyo waliazimia kuunganisha na mradi wa kuzalisha umeme ambao hata hivyo haukuendelea kutokana na kukatishwa tamaa na Tanesco iliyosema wakati huo ilikuwa na umeme wa ziada hivyo hawahitaji wa kutoka Chitec na kusababisha kampuni hiyo kujitoa.

"Baada ya CHITEC kujitoa, Serikali iliamua kuubinafsisha mradi huu kwa wawekezaji binafsi katika mkakati wa kuukwamua.

Wakati KCML inasajiliwa ilikuwa na mtaji wa Sh30 milioni yaani hisa 30,000 zenye thamani ya Sh 1,000 kila moja. Kampuni ilimilikiwa na serikali kwa asilimia 100 kupitia STAMICO na baadaye mwaka 1997 ilihamia kwa Msajili wa Hazina kupitia GN Na. 547/1997," alieleza.

Alisema jitihada mbalimbali za kuukwamua mgodi wa KCML zilifanyika kwa muda mrefu na ilipofika Februari 14 mwaka 2005, serikali iliamua kuongeza mtaji kwa njia ya kuingaia ubia na kampuni binafsi bila kuathiri hisa zake kwenye mradi huo.

"Mwaka 2005 kampuni ya Tan- Power Resources Company Limited TPR iliyosajiliwa na Msajili wa Makampuni Desemba 29 mwaka 2004, ilinunua hisa 700,000 za KCML sawa na asilimia 70 ya hisa zote na serikali ilibaki na hisa 300,000.

Mtaji wakati kampuni inaanzishwa ulikuwa Sh2 bilioni hisa za kampuni milioni 2 za Sh1000 kila moja.

Tarehe 9 Julai, 2008, kampuni ya TPR iliongeza mtaji na kufikia Sh15 bilioni na kuwa na hisa 15,000,000 za Sh1000 kila moja," alisema na kuwataja wanahisa wakati kampuni hiyo inaanzishwa kuwa ni ANBEN Limited, DevConsult International Ltd, Universal Technologies Ltd, Choice Industries Ltd na Fosnik Enterprises Ltd zote zikiwa na hisa 200,000 kila moja.
 
Serikali inabidi kuhakikisha mkopo wa shilingi bilioni 10 ambayo kampuni ya Mkapa na Yona ilipewa na NSSF ambao waliahidi kuurudisha katika kipindi cha miezi sita na riba yake unarudishwa haraka sana maana mkopo huo hivi sasa uko over due

Gharama za mishahara ya shilingi 1.5 billioni ambapo kampuni hiyo ya Mkapa na Yona ilishindwa kulipa na sasa italipwa na Serikali, gharama hizi zichukuliwe kama ni za kampuni hiyo.

Mgodi huo kutokana na kutofanya kazi kwa muda wote ambao ulikuwa chini ya miliki ya kampuni ya Mkapa na Yona sasa hivi umekuwa katika hali mbaya sana. Gharama za kuufanyia ukarabati ili uweze kuanza tena uzalishaji zibebeshwe kampuni ya hiyo ya Mkapa maana wao ndiyo wanahusika na mgodi huo kuwa katika hali mbaya.

Je, ni kampuni gani itakayoteuliwa kuhakikisha gharama ambazo Kampuni ya Mkapa na Yona wanataka warudishiwe ni gharama za kweli? watakuwa ni Wakaguzi huru wa kampuni binafsi au CAG?

Je, Mkapa na Yona walilipwa pesa zozote na TANESCO pamoja na kuwa kampuni yao haikuzalisha hata tone la umeme? kama walilipwa, walilipwa kiasi gani na kwa nini pesa hizo wasirudishiwe TANESCO?

Maskini nchi yetu ya Tanzania. Mijitu inajifanya ni viongozi wazuri na kumwaga sera za kuhakikisha wanaingia madarakani. Mara wakiingia madarakani wanakuja na usanii wa sera mbali mbali, huyu alikuja na "Uwazi na Ukweli" kumbe ni mwizi tu ambaye alitaka kutumia wadhifa wake aliokabidhiwa na Watanzanai kujitajirisha yeye na familia yake!!!! Halafu hakuna hata wa kumfikisha kizimbani kujibu tuhuma chungu nzima dhidi yake!!! halafu tunaambiwa kwamba serikali ya awamu ya nne inapambana na ufisadi uliokithiri nchini!!!!!

Maskini Tanzania na Watanzania wake!!!!! 🙁
 
"...Hata hivyo wanahisa katika kampuni hiyo ni Nick Mkapa, Fostar Mkapa na B. Mahembe ambao wanamiliki Kampuni ya Fosnlid wakati kampuni ya Devconsult LTD wamiliki wake ni D.Yona na Danny Yonna J.R...."

Najaribu kuwaza na kuwazua lakini sipati jibu; hao wamiliki wa FOSNIK na DEVCONSULT wanauhusiano gani na Mkapa pamoja na Daniel Yona ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini? Ni ajabu sana mporaji wa mali za umma anapotafutiwa namna ya kulipwa fidia kwa gharama alizoingia wakati wa kupora mali hizo!!!!
 
mi nikifikiria mambo ya serikali hii ya awamu ya 4 napata kichefuchefu tupu.najuuuta kuzaliwa Tanzania
 
Hii nchi haina mwenyewe???haina system??haina hata jeshi kukemea??nani anatakiwa kupiga kelele??je sisi wananchi tupo??tunafanya nini??tunajua haki yetu ndani ya nchi yetu??naumia sana sana.....viongozi wamekuwa miungu watu hawaguswi wanalindana....wimbi hilo liendeleee kuwa hivyo....nasikitika sana .......
 
Nadhani siku ya hoja ya Kiwira ilipangwa tarehe 21/7/09 bungeni sasa sijui Zitto yupo? simuoni siku hizi hapa ndo mahala pake; usimungunye wala usiteme
 
SERIKALI imesema kutokana na kasoro nyingi zilizojitokeza katika ubinafsishaji wa Kampuni ya Kiwira Coal Mines Limited (KCML), ikiwamo hisia miongoni mwa jamii kuhusu ubinafsishaji wake; imeamua kuchukua hisa zote za mgodi huo na kuilipa kampuni ya KCPL gharama zote zilizotumia kuuendesha.

Hivyo, sekta ya nishati kwa mashauriano na serikali, kampuni ya KCPL imeona ni busara irudishe mgodi wa Kiwira na mradi wa kuchimba makaa ya mawe na kuzalisha umeme serikalini kwa makubaliano kwamba, serikali itarudisha gharama zilizotumiwa na KCPL endapo zitathibitika kwa kuwa za kweli

Sasa hapo kwenye gharama walizotumia ambazo Serikali itarudisha ndio changa la macho linaanzia hapo.
 
Nadhani siku ya hoja ya Kiwira ilipangwa tarehe 21/7/09 bungeni sasa sijui Zitto yupo? simuoni siku hizi hapa ndo mahala pake; usimungunye wala usiteme

Nadahani pia yupo Oscar Mukasa aliyeingia juzi baada ya nguvu ya kubwa kutumika, tumsikie nae anasema nini. Kaenda bungeni kama Mbunge au nae Kandambili?
 
Yaani garama zote zinazodaiwa kiwira zitalipwa na serikali? Mbona sielewi hapa.kama mkapa alikuwa mjasiriamali sasa kashindwa biashara iweje madeni yake yote ya mabilioni haliyokopa benki yalipwe na pesa za wananchi? Sijaelewa nielimisheni
 
Nchi yangu Tz wee.

Yaani wanafikiria kumlipa mfanyabiashara alihujumu nchi!! Yaani hao waliojiuzia wapewe kibano na waadabishwe kama wamevunja sheria za nchi hasa za manunuzi.

Ngeleja simwelewi, tena ni mwanasheria ila anatoa majibu utadhani wako yuko kwenye kesi ya ukoo ya kugawana shamba..
 
Tanznia inahitaji tupate 'MWANAWASA' ndio nchi itakwenda! lakini kama viongozi ndio hao ambao wanatunga sheria ya kuwawekea kinga ilihali wanajua ni wachafu tuitabaki na siasa za KUSAFISHANA.
Kiongozi anitia nchi katika lindi la umaskini kwa kuuza nchi, leo eti mnasema 'mwacheni apumzike alifanya kazi nzuri'
Hebu tazameni uuzaji wa NBC, umilikishwaji wa migodi, Net Group, Kiwira, TISCS, navinginevyo vingi tu wamepewa watu buuree! halafu msaliti huyo anatetewa kwa nguvu zote! tutafika kweli?
Wakati wa SULIVAN SUMMIT kwenye tafrija pale Ngurudoto, Hope Masters na Adtew young walitushangaa kuona watanzania baada ya mika 50 ya uhuru pamoja na utajiri tulio nao na kale ka wimbo ketu UTULIVU NA AMANI bado nchi ni fukara,barabara zimejaa mahandaki! Anrew Young akaifikia hata kusema pale uwanjani walipokuwa wanafanyia sherehe ukichimba lazima uta kuta ka sio madini basi kuna mafuta au gesi!
Yule dada, Hope Masters alifikia hata kutoa machozi na kumuuliza Rais wetu 'watanzania mna tatizo gani?' akazidi kuumbua kuwa ndio maana alikacha msafara kwenda kijiji(jina limenitoka) kwa kujua barabara ni mbovu na ikamlazimu aanzishe harambee ya papo kwa papo kwa ajili ya ujenzi wa hiyo barabara kwa kiwango cha lami!
Hebu tuangalie mfano mdogo tu wa haya madini ya Tanzanite. Pamoja na madini haya kuwa ni ya pekee hapa duniani(yapo Tanzania tu) bado nchi haijafaidika chochote kama sio kuwafaidisha hao makaburu! Hii ni aibu kubwa serikali inadiriki kuwanyanyasa watu waku ili kuwafurahisha hao wezi wa aliasli zetu!
NET GROUP walifanywa kusindizwa na FFU ili waingie ofisini kuja kuvuna shmba la bibi! hebu tujiulize, ni kipi walikifanya TANESCO kwa muda wote waliokuwapo? Serkali yetu inayotufanya watu wake mbumbu ilidiriki kuongopa kuwa Hao makaburu wameongeza ukusanyaji mapato! wakati kilichokuwa kinafanyika ni serikali kuyalipia madeni wizara zake na mashirika ambayo yalilimbizwa kwa muda mrefe ili kuonyesha mapato yameongezeka!
Hiyo ni mifano michache ya huu ufisadi wa hali ya juu,halafu eti mtu ANASAFISHWA. 'anaetaka kumsafisha amsubiri mahakamani kumtetea'
wasalaam,
 
Naamini mungu wetu atatenda kitu kwaajili yetu katika uchaguzi wa mwaka 2010,naamini kwamba haya yanayofukiwa leo yatakwenda kufukuliwa na kuanikwa kwa kadri mungu atakavyotuongoza wakati si mwingi ujao.

Na wale wote walioyatenda haya kwa nchi yao hakika mungu hatawaacha!

Naona kiswahili kingine kinanishinda acha nitoe ujumbe kwa kutumia neno pengine mafisadi wataelewa!
 
Kiwira mine saga: Mkapa, Yona in line for yet another big pay day

-Minister's statement in parliament leaves so much room for speculation

THISDAY REPORTER
Dodoma
​

THE families of ex-president Benjamin Mkapa and former energy and minerals minister Daniel Yona, which spent just 70m/- to buy the Kiwira coal mine four years ago, could now receive a pay-off of not less than 50bn/- from the government to relinquish their shares in the mine.

This follows an announcement by the Minister for Energy and Minerals, William Ngeleja, in Parliament yesterday to the effect that the government intends to refund the current Kiwira mine owners ''all costs they incurred after taking over the mine.''

Following its dubiously-handled privatisation in 2005, the formerly state-owned mine in Mbeya Region was sold off to TANPOWER Resources Limited, a private company established by Mkapa, Yona and some of their closest relatives at a time when the ex-president and ex-minister were still occupying their powerful public offices.

A public statement issued by the reconstituted Kiwira Coal and Power Limited (KCPL) company management last year - at the height of allegations of serious improprieties in the mine's privatisation process - said the new owners had already invested more than 48bn/- on new equipment.

In the wake of Ngeleja's parliamentary statement yesterday, therefore, the potential payments to be made by the government to the TANPOWER Resources shareholders (almost all of them being close relatives of Mkapa and Yona) could end up exceeding this figure by far.

It could even include the 700m/- spent by TANPOWER Resources to purchase an initial 70 per cent majority stake in the mine; a price that in itself was equivalent to 'peanuts' given that the mine was built in the 1980s - with financial assistance from the Chinese government - at a total cost of 4.29bn/-.

According to the expenses breakdown presented by Ngeleja in Parliament, KCPL spent another 3.9bn/- on various consultancies on coal mining and power generation activities at the mine premises; plus a further $6m (approx. 8bn/-) on initial payments to a contractor for the construction of turbines, generators and boilers with a combined capacity of generating 200 megawatts of electricity.

In addition to these costs amounting to well over 12bn/-, the minister listed a catalogue of other potentially multi-billion shilling costs also incurred by TANPOWER Resources through KCPL.

They include an environmental impact assessment (EIA) for a 200MW power plant; a feasibility study for a 200MW power plant conducted by international consultancy firm PB Power; an engineering and procurement contract with Shanghai Electric and COMPLANT companies of China; and a survey of the area prior to the power plant construction work actually beginning.

Ngeleja listed other costs purportedly incurred by TANPOWER Resources through KCPL as the designing of a proposed Kiwira-Mwakibete power transmission line to connect to the national power grid; and preparations for the payment of compensation to residents who would have had to be relocated to pave the way for the proposed power line.

The minister also said the mine owners have so far concluded an environmental audit, an environmental study for an open cast coal mine in the Kabulo area, and scoping and feasibility studies on both the existing coal mine at Kiwira and proposed new mine at Kabulo.

''An international tender for the expansion of the original Kiwira coal mine has already been advertised, with the bids expected to be opened this month,'' Ngeleja told the House.

Despite the multi-billion-shilling costs already incurred, however, the minister said the mine owners have for the past year failed to pay the salaries of the 500 employees at the mine, amounting to 1.5bn/- in arrears.

''Following consultations with the government, KCPL has decided that it is wise to return the Kiwira mine and power generation project to the government on the understanding that the government will refund all actual costs incurred by KCPL,'' Ngeleja declared.

He said the government is considering several options for further development of the Kiwira mine once it regains full control from TANPOWER Resources/KCPL.

One option he mentioned is for the recruitment of an external private company to run the mine under a management contract, similar to the Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO)/ NetGroup Solutions arrangement of the recent past.

''Under such a contract, the contractor will be given the responsibility of building the capacities of both STAMICO (State Mining Corporation) and TANESCO to ensure they can own and run the Kiwira mine themselves in the future,'' he stated.

At he same time, Ngeleja also sought to clear ex-president Mkapa from inappropriate involvement in the whole Kiwira coal mine privatization saga.

According to the minister, ANBEM Limited � the private company owned by Mkapa and former first lady Anna Mkapa - withdrew itself from TANPOWER Resources Ltd 13 days after the latter company was registered.

He named the current shareholders of TANPOWER Resources Ltd as DevConsult International Limited, Universal Technologies Limited, Choice Industries Limited, and Fosnik Enterprises Limited.

THISDAY has long ago reported that Fosnik Enterprises is a company run by the ex-president's son Nicholas Mkapa and his wife Foster Mbuna Mkapa; shareholders of DevConsult International Ltd are ex-minister Yona and his own son Danny; Choice Industries is owned by the recently-deceased lawyer Joseph Mbuna - who was also Nicholas Mkapa's father-in-law; and Universal Technologies Limited is owned by one Wilfred Malekia.
 
Habari ya utawala wa Tanzania inafanana na hadithi ya KALMAKENGE, tabu ni kuwa mbuzi wa kunywa maji ili ya zime moto, moto uchome fimbo, fimbo imchape kalmakenge na kalmakenge akubali kwenda shule hataki.

Bila huyu MBUZI kupatikana tutaendelea kuogelea ktika dimbwi hili la umaskini wa kutupa. Hawa kina Ngeleja na Pinda ni kama moto na fimbo, hawawezi kutenda kazi inayokusudiwa kwa sababu Huyu mbuzi "Rais", hataki kunywa Maji, ili mtiririko ushuke umfikie Kalmakenge ambao ndio fleet yote ya wezi na mafisadi wa mali ya Umma.

Jamani, stahili ya huyu mbuzi ni nini?
 
Kiwira mine saga: Mkapa, Yona in line for yet another big pay day

-Minister's statement in parliament leaves so much room for speculation

THISDAY REPORTER
Dodoma
​

THE families of ex-president Benjamin Mkapa and former energy and minerals minister Daniel Yona, which spent just 70m/- to buy the Kiwira coal mine four years ago, could now receive a pay-off of not less than 50bn/- from the government to relinquish their shares in the mine.

Mkapa na Yona walikuwa na vyanzo vipi vya pesa za kuweza "kuinvest" shilingi billion 50!?

Tunachokijua hadi sasa ni kwamba walipata mkopo wa shilingi bilioni 10 toka NSSF ambao hadi leo hii wameshindwa kuurudisha. Je, hizo shilingi 40 bilioni zaidi walizipata wapi? Walikopa toka bank? Je, walizichota toka EPA kupitia Kagoda? Itakuwa vizuri wakitufahamisha hizo bilioni 50 walizitoa wapi isije zikawa ni pesa za walipa kodi Watanzania walizozikwapua kwa njia za kifisadi.
 
Habari ya utawala wa Tanzania inafanana na hadithi ya KALMAKENGE, tabu ni kuwa mbuzi wa kunywa maji ili ya zime moto, moto uchome fimbo, fimbo imchape kalmakenge na kalmakenge akubali kwenda shule hataki.

Bila huyu MBUZI kupatikana tutaendelea kuogelea ktika dimbwi hili la umaskini wa kutupa. Hawa kina Ngeleja na Pinda ni kama moto na fimbo, hawawezi kutenda kazi inayokusudiwa kwa sababu Huyu mbuzi "Rais", hataki kunywa Maji, ili mtiririko ushuke umfikie Kalmakenge ambao ndio fleet yote ya wezi na mafisadi wa mali ya Umma.

Jamani, stahili ya huyu mbuzi ni nini?

I like this! So painfully true.
 
Kiwira mine saga: Mkapa, Yona in line for yet another big pay day

-Minister’s statement in parliament leaves so much room for speculation

THISDAY REPORTER
Dodoma
​

THE families of ex-president Benjamin Mkapa and former energy and minerals minister Daniel Yona, which spent just 70m/- to buy the Kiwira coal mine four years ago, could now receive a pay-off of not less than 50bn/- from the government to relinquish their shares in the mine.

This follows an announcement by the Minister for Energy and Minerals, William Ngeleja, in Parliament yesterday to the effect that the government intends to refund the current Kiwira mine owners ’’all costs they incurred after taking over the mine.’’

Following its dubiously-handled privatisation in 2005, the formerly state-owned mine in Mbeya Region was sold off to TANPOWER Resources Limited, a private company established by Mkapa, Yona and some of their closest relatives at a time when the ex-president and ex-minister were still occupying their powerful public offices.

A public statement issued by the reconstituted Kiwira Coal and Power Limited (KCPL) company management last year - at the height of allegations of serious improprieties in the mine’s privatisation process - said the new owners had already invested more than 48bn/- on new equipment.

In the wake of Ngeleja’s parliamentary statement yesterday, therefore, the potential payments to be made by the government to the TANPOWER Resources shareholders (almost all of them being close relatives of Mkapa and Yona) could end up exceeding this figure by far.

It could even include the 700m/- spent by TANPOWER Resources to purchase an initial 70 per cent majority stake in the mine; a price that in itself was equivalent to ’peanuts’ given that the mine was built in the 1980s - with financial assistance from the Chinese government - at a total cost of 4.29bn/-.

According to the expenses breakdown presented by Ngeleja in Parliament, KCPL spent another 3.9bn/- on various consultancies on coal mining and power generation activities at the mine premises; plus a further $6m (approx. 8bn/-) on initial payments to a contractor for the construction of turbines, generators and boilers with a combined capacity of generating 200 megawatts of electricity.

In addition to these costs amounting to well over 12bn/-, the minister listed a catalogue of other potentially multi-billion shilling costs also incurred by TANPOWER Resources through KCPL.

They include an environmental impact assessment (EIA) for a 200MW power plant; a feasibility study for a 200MW power plant conducted by international consultancy firm PB Power; an engineering and procurement contract with Shanghai Electric and COMPLANT companies of China; and a survey of the area prior to the power plant construction work actually beginning.

Ngeleja listed other costs purportedly incurred by TANPOWER Resources through KCPL as the designing of a proposed Kiwira-Mwakibete power transmission line to connect to the national power grid; and preparations for the payment of compensation to residents who would have had to be relocated to pave the way for the proposed power line.

The minister also said the mine owners have so far concluded an environmental audit, an environmental study for an open cast coal mine in the Kabulo area, and scoping and feasibility studies on both the existing coal mine at Kiwira and proposed new mine at Kabulo.

’’An international tender for the expansion of the original Kiwira coal mine has already been advertised, with the bids expected to be opened this month,’’ Ngeleja told the House.

Despite the multi-billion-shilling costs already incurred, however, the minister said the mine owners have for the past year failed to pay the salaries of the 500 employees at the mine, amounting to 1.5bn/- in arrears.

’’Following consultations with the government, KCPL has decided that it is wise to return the Kiwira mine and power generation project to the government on the understanding that the government will refund all actual costs incurred by KCPL,’’ Ngeleja declared.

He said the government is considering several options for further development of the Kiwira mine once it regains full control from TANPOWER Resources/KCPL.

One option he mentioned is for the recruitment of an external private company to run the mine under a management contract, similar to the Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO)/ NetGroup Solutions arrangement of the recent past.

’’Under such a contract, the contractor will be given the responsibility of building the capacities of both STAMICO (State Mining Corporation) and TANESCO to ensure they can own and run the Kiwira mine themselves in the future,’’ he stated.

At he same time, Ngeleja also sought to clear ex-president Mkapa from inappropriate involvement in the whole Kiwira coal mine privatization saga.

According to the minister, ANBEM Limited � the private company owned by Mkapa and former first lady Anna Mkapa - withdrew itself from TANPOWER Resources Ltd 13 days after the latter company was registered.

He named the current shareholders of TANPOWER Resources Ltd as DevConsult International Limited, Universal Technologies Limited, Choice Industries Limited, and Fosnik Enterprises Limited.

THISDAY has long ago reported that Fosnik Enterprises is a company run by the ex-president’s son Nicholas Mkapa and his wife Foster Mbuna Mkapa; shareholders of DevConsult International Ltd are ex-minister Yona and his own son Danny; Choice Industries is owned by the recently-deceased lawyer Joseph Mbuna - who was also Nicholas Mkapa’s father-in-law; and Universal Technologies Limited is owned by one Wilfred Malekia.

Hizi lugha za kirafiki mbona zinatumaliza,how can it be wise to return to the Government and then pay compasation kwa huyo mwekezaji??
Walikuwa wapi wasichukue hatua hizo hapo awali na badala yake kuwapatia hawa jamaa..?? sasa wamefanya nini muda woote wakiwa wameshikiria mradi huu..?? inasikitisha sana kuona hawa jamaa kutufanya sisi sote ni vilaza kiasi hichi
 
"...Hata hivyo wanahisa katika kampuni hiyo ni Nick Mkapa, Fostar Mkapa na B. Mahembe ambao wanamiliki Kampuni ya Fosnlid wakati kampuni ya Devconsult LTD wamiliki wake ni D.Yona na Danny Yonna J.R...."

Najaribu kuwaza na kuwazua lakini sipati jibu; hao wamiliki wa FOSNIK na DEVCONSULT wanauhusiano gani na Mkapa pamoja na Daniel Yona ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini? Ni ajabu sana mporaji wa mali za umma anapotafutiwa namna ya kulipwa fidia kwa gharama alizoingia wakati wa kupora mali hizo!!!!

Kilichofanyika hapa ni ufisadi juu ya ufisadi. Huwezi kumlipa mwizi fidia ya kitu alichokinunua kwa kutumia hela yako. Halafu unamwambia akurudishie kitu hicho kwa wewe kukinunua tena.

Maana yake hapo ni "zero sum game" imechezwa au "kipeuo cha kwanza cha moja", tena usikute imekula kwa wananchi tena maana kuna-kuoverstate the real value ya mgodi kwa kisingizio kuwa waliingia gharama kuu-upgrade.
 
Back
Top Bottom