Kiwango cha Elimu Tanzania: Nani alaumiwe?

Nakumbuka elimu ya kujitegemea (Self Reliance). Hii ndio elimu niliyokuwa naipendaa sana kwa wakati ule. Tulifundishwa kilimo bora, kwamba kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi wa nchi yetu. Sijui kwa sasa kama hilo somo linaexist kwa wanafunzi wa sasa baada ya Mungai kubadili sylabus ya Elimu ya Tanzania na kuleta ya kwake kwa maslahi yake binafsi
 
Mfumo wetu wa elimu unahangaishwa na maadili ya viongozi tulionao, akina Mungai waliofuta michezo mashuleni!!!!!!!!!!! ajabu, wenzetu wanatoa scholarships kwa wanaoonyesha vipaji vya michezo.

Hii elimu itakomaa tutakapoingia kwenye EAC and free labour movement, maana kutakuwa na ubora wa mfanyakazi, kutokana na uwezo wa mtu.
 
The function of education is to teach one to think intensively and to think critically. Intelligence plus character – that is the goal of true education: Dr. Martin Luther King, Jr
 
Labda kwenye EK (Elimu ya Kujitegemea) angalau kuna kitu kilikuwa kinapatikana. Lakini elimu ile imewahi kukuongezea kufikiri au kukariri. Nakumbuka kulikuwa na vitabu vinaitwa Jiandae kumaliza elimu ya Msingi. Ni maswali na majibu tu
 
Kiswahili kingekuwa ni lugha ambayo inatumika mashuleni huku pia tukiwa na lugha za kigeni kama masomo ambapo mtu anaweza kufanya zaidi ya moja akipenda. Mara nyingi huwa najiuliza hivi elimu yetu ya Tanzania haiwezi kuboreshwa zaidi au kubadilishwa iwe bora zaidi!!! Jibu hili nakuwa sipati ukizingatia kuwa viongozi wetu wanaishi wakati wao katika kipindi cha sasa hivyo mabadiliko kwao inakuwa kama si kitu au jambo la muhimu.

Kifupi ni kuwa elimu yetu ya Tanzania yahitaji mabadiliko makubwa sana kuanzia msingi hadi vyuoni ingawaji sehemu muhimu sana ni msingi hadi sekondari. Kuna baadhi ya maeneo ambayo hayagusi sana curriculum za shule ila kwa kiasi kimoja ama kingine yanaelekea huko ni kama ifuatavyo;

1. Kingereza kiwe kinatumika kama lugha ya mawasiliano ya biashara pamoja na chuoni.

2. Mashule yawe rated kulingana na uwezo wao na wanafunzi wao kimasomo na kusiwe na sababu za kufeli kwa wanafunzi.

3. Elimu iendeshwe kama vile biashara zingine zinavyoendeshwa kumaanisha kuwa kuanguka kwa waanfunzi ni kama kufeli kwa kampuni yako ya biashara.

4. Walimu waongezewe mishahara mara mbili yake ili wapate hamasa za kuwafundisha wanafunzi kuanzia msingi hadi vyuoni.

5. Shule za Walimu ziboreshwe pia ili kutoa walimu walio na uwezo wa kufundisha mtu kwa uelewa na wajue ethics zao za kazi yao si kutumia ubabe wao katika kutoa points/grade.

6. Walimu wasiofuzu warudishwe shule ama wapelekwe katika idara nyingine mbali na ufundishaji.

7. Michezo irudishwe mashuleni kuanzia msingi hadi vyuoni nchini kote ili kuweza kutoa wasomi walio wanamichezo na pia kupata vipaji vitakavyoisogesha nchi mbele.

8. Tuwe na utamaduni wa kuwasaidia wale ambao hawajabahatika kufanya vyema katika masomo yao.

Ikumbukwe kuwa uhuru, Ushindani na Uhuru wa Kuchagua ndivyo vitakavyonyanyua elimu kwa kiasi kikubwa sana. Inabidi sote tuwe tunaangalia hivi vyote ili kudumisha na kuboresha elimu ya Tanzania. Hapo Maghembe na Maggie Sitta inabidi wafanye juhudi sana tu ili tuvuke upande.
 
jamani, tatizo kubwa kwenye elimu yetu ni lugha ya kufundishia! ile sylabus ya juma na roza ilikuwa nzuri sana na ilipata mafaniio lakini mfumo wa maarifa yaliyokusudiwa kwa mwanfunzi yaliparaganyika mara tu kufumba na kufumbua kiingereza kilipochukua nafasi kuazia kidato cha kwanza. hapo ndipo peny tatizo. elimu ya msingi tuliyoipata vizuri ikapata msukosuko wa kubadili lugha na matokeo yake hata yale ambayo tukiwa shule ya msingi tulitarajia tutayaelewa vizuri tukifika shule za upili, yalishindikana!, tukabaki tunakariri tu yaani tunameza tu bila kutafuna na tunaenda haja (mtihani) bila tulichomeza kumeng'enywa. ndivyo walivyokuwa walimu wetu na ndivyo walivyo leo!

tukitatua tatizo la kusuasua kutumia lugha yetu kama lugha ya kufundishia na kujifunzia, atoto wetu watapata maarifa halisi yanayokusudiwa. kumbuka elimu nzuri si ya kukuwzesha kupambana na watu kwani utakuwa na maana kuwa kama mapambano hayapo, basi elimu yako haitahitajika!, bali elimu ya maana ni ile ya kukuwezesha kuelewa na kutawala mazingira yako. ukifikia lengo hili, ushindi kwenye mapambano utakuja wenyewe.
 
Inawezekana kabisa elimu ya Juma na Roza ilikuwa na nafasi ila naitazama zaidi kwa wakati ule ambapo teknolojia yetu ilikuwa duni saana.

Pia inawezekana kabisa elimu ile ndioimetufikisha hapa tulipo maana wengi wanaongooza sasa hivi ni watu wa Juma na Roza. Wkt huo wengi wa waalimu walikuwa wa UPE (wamesihia darasa la saba wanakwenda kufundisha darasa la saba tena walikuwa failures). Tulikuwa kwenye mfumo wa kijamaa.

Tumejifungia mlango tukiamini kuwa sisi ni bora kumbe hatuoni nje. nakumbuka miongoni mwa mambo yaliyokuwa yakisimuliwa eti "sisi tuna idara bora ya usalama wa Taifa na pia jeshi letu lina nguvu sana". Kuamini huku kulitokana na kukosa utandawazi.

Nadhani inahitajika jitihada kwenye elimu sio siasa ya kujenga madarasa mengiiiiiiiiii quality ovyo.

Ila sijui kuruhusu uwepo wa shule zinazojiita english medium kumeathiri vipi elimu yetu!
 
Tulichukua watu waliofeli tukawapa ualimu, sasa tunaona matokeo yake. Haiwezekani mtu aliyepata Div IV points 28 akamfundisha mtu akafaulu vizuri.

Mara nyingi hawa utakuta hesabu na kiingereza kwao ni shida sana, hivyo wanafunzi wanatoka shule za msingi hawana msingi mzuri wa hesabu na kiingereza – hivyo na huko mbele matokeo ni yale yale.

Katika nchi nyingine ualimu ni kazi ya watu waliofanya vizuri kabisa katika masomo yao, na ndiyo huweza kuwafundisha vizuri wanafunzi wao kwani wanajua vyema kile wanachokifundisha.

Hapa Tanzania si ajabu kwa mwanafunzi kumuuliza mwalimu swali, nae akashindwa kujibu!

Angalia vyuo vikuu vya wenzetu, ni vituo vya utafiti na ugunduzi wa mambo mbalimbali ya kisayansi – sisi hapa ni vyuo vikuu vingapi vinafanya utafiti wa kisayansi na matokeo yake yaliyotangazwa ni mangapi na yapi?

Tumeshuhudia hivi karibuni degree feki! Huyu mwanafunzi aliyefundishwa na mwalimu feki, na ikadaiwa amefaulu – naye si amefaulu katika ufeki tu!.

Hatua za kuchukua:
Kuanzia sasa, watu wa kusomea ualimu kwa waliomaliza kidato cha nne, wawe wamefaulu kwa Div III. Tusilazimishe kuwa na walimu wengi ambao ni mabomu – tutazidi kutumbukia shimoni.

Wanafunzi wa shule za msingi wanaofaulu hisabati, kiingereza na sayansi, wapelekwe kwenye shule za sekondari ambazo kuna uhakika wa waalimu wa kuwaendeleza. Tumeshuhudia hivi sasa wote wakipelekwa shule za kata ambazo tunakiri hazina waalimu – tunawapoteza watoto hawa!.

Tunaweza kwa kuanza kutenga shule moja katika kila tarafa na kuipa kipaumbele hicho – waalimu wa sayansi na hisabati, na mabweni, ili kwa kila tarafa wale wanafunzi waliofaulu vizuri masomo hayo waende kwenye shule hizo

Mshahara kwa wanasayansi uwe mkubwa – kuanzia kwa mwalimu anayefundisha masomo hayo ngazi yoyote ile hadi kwa wanaofanya kazi za kisayansi.

Mwanafunzi mmoja nilikuwa namhimiza asome hisabati na sayansi ili aje ashike nafasi yangu ya uhasibu, aliniuliza- hivi wewe na Meneja wako nani ana mshahara na marupurupu zaidi – nilimjibu kuwa ni meneja wangu. Akaniuliza, yeye amesomea nini?

Tufike mahali wataalamu tuwape malipo mazuri, zile enzi za kusema meneja ana majukumu ya kiuongozi hivyo alipwe zaidi kuliko mtaalamu aliye chini yake, zimepitwa na wakati.

Matokeo ya mtihani wa Form II yaliyotangazwa jana ni ushahidi tosha
 
Katika nchi zisizojali elimu ni Tanzania. Ukimpa elimu mtu basi atafahamu mambo na atadai haki zake kiusawasawa. Hii ndo fimbo inayotumika na serikali, NYIMA ELIMU. TAWALA KIULAINI.

Watanzania wakipewa elimu kisawasawa, wataiweka matatani serikali hii ya kifisadi.

Nimewahi kusoma katika moja ya shule za secondari wanazoziita special. Mi sielewi kwanza huu uspecial unatoka wapi, ila ntakubaliana nao kama watasema wanafunzi ndio special maana wengi wao wanakuwa waliofaulu sana. Katika shule hizi kuna walimu wengine wabovu kabisa ambao hawafai kuwepo pale. Hata mfumo wa ufundishaji ni MBOVU, uko EXAM ORIENTED badala ya PROFFESIONAL ORIENTED. Hii ni aibu sana. Lakini poa acha watunyime elimu ili watutawale vizuri, ila ipo siku.

Kwa hiyo kwa mfumo huu wa kuchukua walimu wasiojiweza kwenda kufundisha ni kudidimiza nchi, maana uti wa mgongo wa maendeleo ktk nchi yoyote ile ni Elimu, na si kilimo kama tunavyojidanganya.. Elimu ni kila kitu. Taifa likiwa limeelimika hata maendeleo ya Kilimo, afya, na maeneo mengine yatakuja tu kwa kasi mpya.

Ukitaka uone jinsi ambavyo uandaaji wa walimu ni mbaya fatilia vyuo vya walimu, na vyuo vikuu wakati udahili unafanyika.

Ukiulizwa, " Umeomba kozi gani?"
Ukijibu, " Ualimu! "
Basi utachekwa na utadhalauliwa sana kwa sababu zifatazo:
1: Umepotea njia (Umepoteza mwelekeo)
2: Maisha yako unayaweka pabaya maana mshahara wako baadae ni kiduchu.
3: Inaonesha umefeli sana.

Au utasikia mtu(rafiki au mzazi) anamwambia mwenzake aliekosa udahili:

"Hata ualimu(Education) umekosa???????!!, aya yaya yaa yaa duh!

"Hata ualimu!!!!!!!!!! nao umekosa
"

Ualimu umedhalauliwa sana na haupewi nafasi yake kama inavyotakiwa.

Watu wengi wana talent za ualimu na ni wazuri ktk masomo. Lakini, nani aende ualimu wakati wengi wanaoenda huko ni feliaz na wanahofia mapato yao ya baadae!!.

Kwa kweli inasikitisha, inatia uchungu sana. Ila tutafika tu siku moja..
 
Nimekusanya taarifa mbali mbali kuhusu hali halisi ya kada ya elimu nchini Tanzania.

Taarifa hizi zimenisukuma kleta mjadala mezani ili SISI wadau tuweze kuchangia na kuwaambia watawala wetu ambao siku zote wamekuwa SIYO wasikivu kwa hoja muhimu kama hizi. LAkini mchango wako na wangu utatutoa lawamani kwani tutakuwa TUMETIMIZA WAJIBU.

Hivi karibuni Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi alikutana na waandishi wa habari kutangaza matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha pili, katika maelezo yake amekiri kushuka kwa kiwango cha kufaulu kiasi kwamba SERIKALI imeamua kwamba ambao waliopata alama hafifu yaani waliofeli wameruhusiwa kusonga mbele kwa uangalizi maalum kimasomo. Pia Wizara SERIKALI imekiri kugaragazwa na shule binafsi katika kutoa matokeo bora ya wanafunzi wanaofanya vyema masomoni. Hivi karibuni pia tumeshuhudia kupitia vyombo vya habari na kuona picha mbali mbali za shule ambazo nyingine hazina walimu seuse majengo kiasi kwamba wanafunzi wanasoma chini ta miti.

Hivi karibuni pia mwishoni mwa mwaka jana tulipata kujuzwa matokeo ya mitihani ya kidato cha nne ambapo hadithi ni ile ile ya viwango vya kufaulu na ile hadithi maarufu ya wizi wa mitihani ikiendelea kupata rangi isiyopauka. Naamini baadhi yetu humu ni wafuatiliaji wazuri wa takwimu mbali mbali ambapo tukilinganisha wimbi la utitiri wa shule na vyuo nchini haujaweza kukidhi tuoaji wa elimu bora tena inayoendana na wakati.

Takwimu nyingi zinaonesha madhaifu mengi katika tasnia ya elimu nchini. Si ajabu ukakuta mwanafunzi amefaulu kuingia sekondari lakini ukimwambia aandike jina lake ni kama umempa adhabu kubwa. Uwezo wa wahitimu wengi wa shule na vyuo wamekosa ujasiri wa kujieleza au hata kuitumia elimu yao kwa manufaa ya UMMA, sana sana vijana wengi wanasaka vyeti ili kuvitumia as stepping stone (ngazi/ daraja) kupata ajira.

Ninawafahamu wahitimu wachache ambao walihitimu masuala ya sayansi ya vyakula, elimu ya viumbe bahari, na kadhalika lakini wengi wameajiriwa katika nafasi ambazo siyo taaluma yao. Hawa mawaziri wetu hawana lolote laq maana zaidi ya kuongeza contents katika CV zao kuwa waliwahi kuwa mawaziri, kama si kweli basi waje watuoneshe kazi walizofanya ili tuzipime kwa MOTO.

Hayo yote na mengine mengi, ni matokeo ya kushuka au kudharau nidhamu ya elimu tija. Sijaona mahala popote ambapo waziri au hata naibu wake wakielezea mikakati ya kuondoa tatizo la kushuka viwango vya elimu nchini, na ukiangalia sura zao wakati wanatangaza matokeo ya mitihani hawaoneshwi kukerwa na uporomokaji wa viwango vya kufaulu. Sana sana watakwambia namna watakavyowashughulikia wanaoiba mitihani lakini KAMWE hawasemi watawasaidiaje waliopo mashuleni kutojiingiza katika wimbi la kuibia mitihani ya taifa.

Ningelikuwa mimi ni rais ningemwambia waziri wa elimu wakati akila kiapo kwamba wizara yake nitaiangalia kama timu ya taifa yaani matokeo yakiwa mabaya sina radhi naye na nitamtimua bila kigugumizi. Haiwezekani wakati miaka ya uhuru ikiongezeka na elimu yetu ishuke. Na wanajukwaa amini nawaambia kwamba hali ya elimu nchini haiwanyimi usingizi watawala wetu kwani wao wanasimamia MITAALA ambayo hawaiamini kamwe, kama unabisha fanya uchunguzi uniambie motto gani wa waziri ambaye anasoma elimu ya msingi katika shule za serikali? Watoto wao na wakurugenzi wao wanasoma katika shule binafsi na zaidi wanasoma nje ya nchi ili waje kutawala pale baba na mama zao watakapokuwa nje ya mfumo. Tukiendelea hivi tutajikuta ni taifa linalotawaliwa kifikra na si kujitawala kifikra.

Naamini hatujachelewa KUANZA upya kuangalia mustakabali wa TAIFA letu na uwezo wetu kitaaluma. Elimu iwe nyezo muhimu kuikwamua jamii kutoka katika lindi la ufukara wa kifikra ili WATANZANIA waweze kuwekeza nchini na duniani pia. Lazima tuwe na mitaala inayokidhi mazingira yetu na wakati, pia ni lazima tuweke miiko ya taaluma zote NAAM zote kwani bila principle there is no order.

Una maoni gani?
 
Elimu imebinafsishwa nchi hii ndugu yangu. Watasoma vizuri watoto wa walioko kwenye mikondo ya rushwa na ufisadi tu. Mitihani ya NECTA na kwingineko imeingizwa sokoni kama bidhaa nyingine yoyote. Shule za Msingi na sekondari za serikali zimetelekezwa. Hazina Walimu, hazina vitabu vya kiada na ziada, hazina madarasa, madawati watoto wanaambiwa wanunue wenyewe,,,,
 
Elimu imebinafsishwa nchi hii ndugu yangu. Watasoma vizuri watoto wa walioko kwenye mikondo ya rushwa na ufisadi tu. Mitihani ya NECTA na kwingineko imeingizwa sokoni kama bidhaa nyingine yoyote. Shule za Msingi na sekondari za serikali zimetelekezwa. Hazina Walimu, hazina vitabu vya kiada na ziada, hazina madarasa, madawati watoto wanaambiwa wanunue wenyewe,,,,
.....halafu kila mwaka Waziri wa elimu na manaibu wake watakuwa wanatusomea matokeo ya mitihani......
Kweli tumeuzwa
 
.....halafu kila mwaka Waziri wa elimu na manaibu wake watakuwa wanatusomea matokeo ya mitihani......
Kweli tumeuzwa
Kama Kova anavyofanya na bunduki zake kwenye luninga zetu huku ujambazi unaendelea. Kila mtendaji serikalini anajitajihidi aonekane kwenye Tv na kesho yake magazeti yaandike.
 
"Education of the Rejected in Tanzania" refer; http://vangidunda.blogspot.com/2010/01/education-for-rejected-in-tanzania.html
Tunakoelekea nafikiri si kuzuri. Na hii ni hatari sana kwa watoto wa wakulima, maskini wasiokuwa na uwezo wa kuwapeleka watoto wao kwenye shule za binafsi ambazo zina walimu wa kutosha, maabara, vitabu na vifaa vya kufundishia.
Na zaidi ya yote, shule za vipaji maalum zinaonekana kufanya vizuri ilihali, na ukiangalia mtoto wa mkulima hana pia uwezo wa kuchaguliwa katika shule hizo kutokana na mazingira mabovu anayosomea, halafu mwisho wa siku anafanya mtihani mmoja na wale ambao wamesoma shule zilizo bora.
Nafikiria, natafakari, nashindwa kuelewa hatma ya nchi yetu ni nini?
Na hizi shule zetu za kata, ndo balaa zaidi. Ningetamani kama siku moja ningemkuta mtoto wa waziri anasoma kule. Inashangaza kwamba wanafanya mambo substandard kwa kuwa tu hayawahusu. Kwa kuwa wanaosoma kwenye shule mbovu si watoto wao basi wacha tu ziwe hovyo! Tutafika kweli kwa mtindo huu?
Bado tuna safari ndefu sana.
 
Kama Kova anavyofanya na bunduki zake kwenye luninga zetu huku ujambazi unaendelea. Kila mtendaji serikalini anajitajihidi aonekane kwenye Tv na kesho yake magazeti yaandike.
Ah hizi TV zetu zinawapumbaza watendaji wetu kweli kweli.
Lakini aibu ya kushuka viwango nani anaibeba iwapo wenye dhamana hawaoneshi kustuka??
Wanalalamika hakuna walimu wakati wanao uwezo, kama waziri anatoa sababu ambazo hazina tofauti na sababu za kocha wa stars inapofungwa tufanyaje?
 
Elimu ndio msingi wa maendeleo ya nchi yeyote ile duniani, Uchumi wa nchi hauwezi kustawi pasipo elimu bora. Nakubaliana na msanii elimu yetu, imeporomoka na hakuna mwenye uchungu na kiwango cha elimu yetu.

Matokeo ya Mtihani wa darasa la Saba na Kidato cha pili ni dira tu ya kiwango cha mambumbu katika nchi yetu. Kwa maoini yangu shule za Kata ni sumu kwa maendeleo ya elimu Tanzania, Kwa nini?
1) Elimu haipatikani darasani tu, hata kuchanganyika kwa tamaduni za Jamii tofauiti Kunachangia uchangamfu wa mawazo. Lea hii mjomba, binamu, kaka, dada... wanamaliza shule ya msingi kijiji kimoja wanaingia sekondari kijiji hicho hicho hata hawaoni tofauti ya shule ya msingi na sekondary (Fikra zimedumazwa)

2) Elimu bora ni pamoja na walimu wakutosha na walio bora. Tazama shule zetu za kata wianisha idadi ya walimu, jumlisha na ubora wao kisha ongeza idadi ya watoto wanao vuka kutoka darasa la saba yamkini sijui kwa kufaulu au kwa propaganda za kufaulisha ili nchi ionekane imeendelea, then jawabu utapata......

3) Then Namna gani vijana wetu wanafika darasani, na vipi wanarudi nyumbani na wakifika huko wanakuwa katika mudi gani?... Yamkini kila mwana JF anaelewa hali halisi ya usafiri kwa wanafunzi wetu....

Hizo ni baadhi tu ya ishara za ubovu wa elimu yetu, na hakuna aliye tayari kuchukua hatua kwa sababu watoto wao hawasomi hapa....Watahukumiwa na historia katika kizazi kijacho.

Maoni:
Hakuna haja wala faida ya kuwa na majengo mengi ya vijishule vidogovidogo visivyo na walimu wala vitendea kazi. Muafaka ni kujenga shule chache, na kubwa mfano kama Mkwawa ya Zamani, au Tosa Maganga ambazo zitakuwa katika maeneo mazuri ambayo yatafikika na walimu bila hata kubembelezwa watapenda kufundisha. Shule za mfano huu zijengwe katika kila miji na miji midogo na zichukue vijana kutoka maeneo tofauti kama ilivyokuwa hapo kale badala ya shule za kata sasa.

Maslahi ya walimu ya zingatiwe na walimu wa waandaliwe vyema. Nchi kama Sweedeeni mwalimu anaheshimika kulio mtumishi yeyote wa UMMA, hii ni kwa sababu wanaamini mwalimu ni uti wa mgongo wa nchi.

Kwa kumalizia ningependa kusisitiza kwamba hali y a elimu inatisha Katika nchi yetu na tusipokuwa makini nhi itagawanyika katika matabaka ya waliosoma vizuri na waliosoma vibaya ambayo vita yake haitaisha.

Hayo ni maoni yangu huru wana JF.
 
Kwa hiyo kwa mfumo huu wa kuchukua walimu wasiojiweza kwenda kufundisha ni kudidimiza nchi, maana uti wa mgongo wa maendeleo ktk nchi yoyote ile ni Elimu, na si kilimo kama tunavyojidanganya.. Elimu ni kila kitu. Taifa likiwa limeelimika hata maendeleo ya Kilimo, afya, na maeneo mengine yatakuja tu kwa kasi mpya.

Ukitaka uone jinsi ambavyo uandaaji wa walimu ni mbaya fatilia vyuo vya walimu, na vyuo vikuu wakati udahili unafanyika.

Ukiulizwa, " Umeomba kozi gani?"
Ukijibu, " Ualimu! "
Basi utachekwa na utadhalauliwa sana kwa sababu zifatazo:
1: Umepotea njia (Umepoteza mwelekeo)
2: Maisha yako unayaweka pabaya maana mshahara wako baadae ni kiduchu.
3: Inaonesha umefeli sana.

Au utasikia mtu(rafiki au mzazi) anamwambia mwenzake aliekosa udahili:

"Hata ualimu(Education) umekosa???????!!, aya yaya yaa yaa duh!

"Hata ualimu!!!!!!!!!! nao umekosa "

Ualimu umedhalauliwa sana na haupewi nafasi yake kama inavyotakiwa.

Watu wengi wana talent za ualimu na ni wazuri ktk masomo. Lakini, nani aende ualimu wakati wengi wanaoenda huko ni feliaz na wanahofia mapato yao ya baadae!!.

Kwa kweli inasikitisha, inatia uchungu sana. Ila tutafika tu siku moja..

Nakubaliana na wewe. Ni kweli wale wanaofaulu vizuri hawataki kwenda ualimu kwa kuwa kwenye ualimu kumejaa walioshindwa. Imekuwa ni kimbilio la walioshindwa na labda ndiyo sababu mshahara ni mdogo.
Hivyo basi, inabidi tuanze mara moja kuwapa motisha wale ambao wamo kwenye ualimu lakini wanafanya vizuri kwenye masomo ya hisabati, kiingereza na sayansi, na tuache mara moja kuchukua failures, yaani tuwe tuna-phase out taratibu, labda baada ya miaka 20 watakuwa wameisha.
NImesoma magazeti ya leo kuwa waziri ameunda kikosi cha kufuatilia suala hili
"Hatua hiyo itakayowahusisha walimu wa shule za msingi, sekondari, wahadhiri wa vyuo vikuu na wadau wengine wa elimu Januari 19 mwaka huu, itakuwa na nia ya kujadili na kupata chimbuko la sababu za kudorora kwa ufaulu wa wanafunzi nchini".-Gazeti la Majira 14 Jan 2010

Sidhani kama waalimu watakuwa tayari kumweleza waziri kuwa wanafunzi hawawezi hisabati kwa kuwa sisi (Waalimu) hatujui hesabu, au tuliingia huku kwenye ualimu kama kimbilio baada ya kufeli.
Ni vizuri wana JF mumpenyezee waziri hii thread, maana sisi kama wadau wa elimu tayari tunaanza kutoa michango yetu.
 
"Alisema wanafunzi walioshindwa mtihani huo ni 126,131 ambao ni sawa na asilimia 34.6. "- Gazeti la Mwananchi 14 jan 2010. Haya ndiyo matokeo ya form II mwaka huu (jana) 2010. Bado na hawa walioshindwa wataendelea hadi kidato cha nne, maana rais alishasema kuwa mtihani wa form II uwe ni wa kupima tu kujua wapi mwalimu arekebishe na usitumike kuchuja.
Kwa mantiki hayo basi wanafunzi hawatilii maanani mtihani huu kwa kuwa hauna athari kwao. Hivyo hii yaweza pia kuwa sababu. Na yote hii ni ukosefu wa sera zenye dira maana kila anayeingia madarakani anafanya atakavyo.
Tukirudi kwenye mada - hawa wamefeli bado wanaendela halafu unategemea matokeo yao wakimaliza form IV yaweje?
 
Back
Top Bottom