Kiwango cha Elimu Tanzania: Nani alaumiwe?

Badala ya kusema nani alaumiwe...sema tufanye nini kupandisha kiwango cha elimu...
Lawama na kunyoosheana vidole havitasaidia...
Tuliteleza wapi je tufanyeje kujizoazoa na kusonga mbele...?

Nimekumbuka Toyota 2009 walipopata skendo ya kutengeneza gari zenye defects ...
CEO alisema kuwa siku waliyoamua kupanua soko (hence production) ndio walipokubali kushusha quality ya magari yao...
Sasa wakaishia kukosa imani ya wateja na ku recall thousands of cars duniani...juzi kati tena wame recal 3.37 million cars kwa sababu ya defects za air bags na emissions...quantity ni sumu ya quality...fikiria hasara wanayopata...sijui kwa nini wamejua sababu lakini hawataki ku learn...
 
Elimu imechafuliwa na siasa. Ukiwapata wanasiasa wasio heshimu wataalam ni tatizo. Je, tutengeneze agency ya elimu itakayoratibu elimu bila kuingiliwa. Tuweke utaratibu mgumu kwa mtu mmoja kuamka na kubadili syllabus. Mtakumbuka Mungai kufuta masomo ya biashara na ku- combine sayansi.
Tuanze sasa kuhakikisha form four hafundishi popote hata kwa division one km tulivyoweza kufuata UPE.
 
Kabla ya kutoa hukumu kwamba elimu yetu imeshuka au kupanda, inabidi kwanza mtuelimishe imeshuka au kupanda kutoka wapi? Yaani kabla ya sasa tulikuwa wapi na sasa tupo wapi, hapo tutaweza kupima. Na wasiwasi bila kuweka vigezo thabiti tutaongozwa na hisia zaidi kuliko ukweli wa mambo.
mkuu Kitila Mkumbo, hivi ni kweli tunahitaji kusomewa takwimu ili kufahamu kama kiwango cha elimu kwa sasa kimeporomoka kulinganisha na mahitaji ya kidunia? mimi kwa ufahamu wangu naona kupanda ama kushuka kwa kiwango cha elimu katika taifa husika hakupimwi na wakati (elimu ya 1970s vs elimu ya 2000s) bali hupimwa kwa uwezo wa elimu inayotolewa kuweza kukidhi mahitaji ya taifa husika kwa ukamilifu. nimejaribu kidogo mkuu.
 
Wakumuuliza aliyechezea na kubadiri mitaala ya elimu alikuwa mwalimu tena mwenye sifa za ualimu miaka yamwanzoni baada ya kuwa jamhuri ya Muungano.
Alitamani watu wote wajue tu kusoma na kuandika iliojulikana kama Elimu ya Ngumbalo,kwa hilo alifanikiwa.
Wanafunzi chuo kikuu cha Dar walipoandamana wakisema afadhali ya mkoloni ndio kabisa lugha ya serikali ya English iliokuwa ndio lugha ya serikali na lugha kuu ya kufundishia ikakabwa koo hadi leo.
Azimio la Arusha japo madhumuni yalikuwa mazuri,lakini likakosa watendaji wasio na nia au uwezo au upeo.
Maamuzi ya bunge na serikali wakati wa chama kushika hatamu yalitawaliwa na propaganda zaidi.
Mwalimu usinibaini wajinga ndio waliwao,wao wakawasomesha watoto wao ulaya na marekani wakisaka elimu bora,waliochakachua wenyewe nyumbani.
 
ELIMU ni jumla ya maarifa,stadi na mielekeo.ELIMU haiwezi kuonekana hasa kwa kipimo cha alama za mitihani zilizopo kwenye vyeti na shahada,bali huonekana kwa jinsi inavyofanya kazi kwa aliyeipata.ELIMU haina mwisho,ni mnyumbuliko na muendelezo wa maarifa na stadi katika kutumia sayansi na teknolojia kuondoa umasikini,ujinga na maradhi,kisha maendeleo huja.
 
Mkandara, naona unakataa kuelewa.

Mwaka 2000, 19% ya watoto waliokuwa darasa la saba walifaulu mtihani wa kuinga kidato cha kwanza. Mwaka 2005, hio asilimia ya kufaulu mtihani wa kuingia kidato cha kwanza iliongezeka ikakafika 48% . Sasa unataka kusema huko sio kuongezeka kwa ubora wa elimu?

Asilimia ya kufaulu kidato cha nne imekuwa ikiongezeka vile vile. Angalia website ya NECTA.

Augustine MOshi
mkuu Augustine Moshi kutoka ufaulu wa 19% mpaka 48% huko ni kuongezeka kwa kiwango cha elimu kwa TZS (Tanzania Standards) lakini je hiko kiwango cha elimu tunachotoa kwa watoto wetu kitatuwezesha kukidhi mahitaji yetu ya ndani pamoja na ya kimataifa?
 
Kama wazee wanapima vijana kwa kipimo walichopimiwa wao then kiwango kimeshuka, kama vijana wanaopata elimu wanaona wenyewe kuwa inawasaidia then hakijashuka.

Japo si mzee wala kijana najua kuwa watu wanakuwa wabinafsi zaidi kadiri siku zinavyoendelea. Asipotokea mtu wa kureverse hii (hopefully JK) tunaishia pabaya very soon.

Tatizo la elimu kama lipo kwa nini halishughulikiwi? Ina maana hakuna wataalamu? Mbona kila siku wanasomeshwa?

Tunasomesha wataalamu wengi sana hatutakiwi kuwa na sector isiyokuwa na wataalamu WA KUSOLVE PROBLEMS. Sio kuandika mada.

Ni aibu kuzuzungumzia hili jambo miaka nenda rudi.

Let us do it, find a solution and stick to it.[/QU
Salama humu?
Tatizo kubwa la elimu yetu kuwa mbovu ni SOKO HURIA KATIKA ELIMU
Taifa lolote makini duniani huwa halifanyi soko huria katika katika elimu ,maana elimu siku zote ndiyo inayoamua ni aina gani ya watu wawe katika taifa hivyo huwa halifanyi mchezo na elimu.
Elimu ya tanzania imegeuka kuwa biashara badala ya huduma kwa wananchi na biashara hiyo kwa kiasi kikubwa wanafanywa na wale walio na dhamana ya kuisimamia nikimaanisha viongozi waliowengi katika serikali.
Katika azimio la Arusha tulikuwa na miiko ya uongozi,miiko ambayo ilikataza kiongozi wa serikali kumiliki makampuni ya kibepari au kuwa na hisa katika makampuni hayo maana Mwl alijua kabisa kuwa kiongozi akimiliki makampuni hayo ni lazima huduma za jamii zitakuwa mbovu ili watu waende kwakwe kupata huduma zilizo bora.
Maana haiwezekani kiongozi mwenye dhamana ya kusimamia elimu akawa anamiliki shule yake binafsi halafu utegemee elimu iwe bora,maana elimu ya umma ikiwa bora basi shule yake haitakuwa na wanafunzi, kwahiyo ili atengeneze pesa nyingi ni kuhakikisha elimu ya umma inakuwa mbovu ili wananchi wapeleke watoto katika shule yake.
Pili kwanini si elimu bora kwa maana ya product tunazozipata au wahitihu kuwa wabovu?
Wahitimu wengi wanakuwa wabovu kwasababu inawezekana kwa kiasi kikubwa hata mitihani inaibwa ili kutangaza majina ya shule,lakini pia hili haliishii kwenye shule za sekondari bali linakwenda mpaka vyuo vikuu,kutokana na kila chuo kuhitaji wanafunzi wengi siku hizi ni nadra sana kusikia wanafunzi wamedisco hili linatokana na waadhiri kupewa masharti kwamba wanatakiwa kuhakikisha wanafunzi wanafauru vizuri ili kuendelea kuvutia wasomaji kuchagua vyuo hivyo.

MATATIZO YANAYOWEZA KUTOKEA HAPO BAADAE KUTOKANA NA UBOVU HUU TULIONAO
1.UDINI
Kama tutakumbuka baada tu ya kupata uhuru 1961 Mwl Nyerere aliamua kutahifisha shule zote zilizokuwa zinamilikiwa na mashirika ya dini ili shule hizo kuwa shule za serikali mfano wa shule hizo ni Ilboru,Ifunda,Pugu,Kibaa,Mzumbe,Tanga techn Moshi sec,na nyingine nyingi,alifanya hivyo kwa sababu zingeendelea kumilikiwa na mashirika ya dini tu maana yake madhehebu yenye shule hizo ndiyo yangekuwa na watu wengi zaidi waliosoma kuliko wengine,kwa kuzichukuwa alizifanya shule hizo zipokee kila aina ya muumini bila kujali dini yake,Tazama leo madhebu mengi leo ndiyo yanayo miliki shule nyingi na bora zaidi maana yake waumini wa dini hizo baada ya muda watakuwa na watu wao wengi walio na elimu na hata ajira zitakuwa kwao maana watakuwa na vigezo.
Inawezekana wanapokea watu bila kujali imani ya mtu lakini imani ni imani tu,huwezi ukawa ni msabato na kanisa lenu likawa na shule yenye sifa sawasawa na shule ya dhehebu lingine halafu uende kwenye dhehebu lingine lazima utachagua kwenda kwenye shule ya kisabato.
2.UKABILA
Nikweli kwamba katika makabila yetu kila kabila linashughuli za asili za kiuchumi,wako wafugaji,wako wakulima zidi, na wapo wafanyabiashara,sasa kutokana na kwamba elimu imekuwa biashara bila fedha nyingi hujapata elimu bora basi makabila yanayojihusisha na biashara yatasomesha zaidi kuliko wengine hivyo kupata watu wengi waliosoma wa kabila lao.Pili kutokana na shule za kata ,vyuo vya kata kwahiyo watu kwasasa hawatoki katika maeneo yao wanasoma hapo awali,sekondari,chuo na kazi hufanya maeneo hayo jambo ambalo litafanya makabila katika baadhi ya maeneo kukua zaidi na kupanuka katika maeneo hayo maana mtu anakua hajui kabila lingine ataacha kuutukuza ukabila wake? lakini kitendo cha kuwachanganya watoto kama ilivyokuwa zamani watanzania walijuana kutoka mashuleni na hivyo kuua ukabila.

3.WASOMI WAJINGA NDANI YA NCHI
Kutokana na elimu kugeuka kuwa biashara maana yake sasa hivi elimu inanunuliwa,kwahiyo tutajikuta tuna watu wengi sana ndani ya nchi waliomaliza vyuo vikuu lakini ni wajinga kuliko watu wasiokwenda shule na ujinga huo unaanzia katika fikra mpaka katika kazi,leo hii msomi wa chuo kikuu ukimwambia simama hapo dakika kadhaa ajieleze hata kuhusu mambo ya kawaida ni aibu,hii nikutokana na kununua elimu lakini pia pamoja na kununua elimu sasa hivi zimekua elimu za photokopy zaidi tofauti na zamani ambapo watu walisoma na kuandika sana hivyo walijenga fikra vema ,hata ukiangalia vitabu vya siku hizi chukua kitabu cha zamani cha Mathematics na cha sasa utaona hivi vya sasa vimeandikwa kijinga sana contents yake ni ndogo na hakuna hata maswali ya kufikirisha hilo nalo nitatizo yaani vitabu sasa hivi vinaandikwa kwaajili ya kurahisisha kukariri hiyo ndiyo shida.
KARIBUNI KWA MJADALA NITATOA BAADAYE NINI KINATAKIWA KUFANYIKA ILI IWE BORA
 
There is a very big demotivation crisis to the teachers,no serous passmark for students of lower class
 
duh sikujua kama kunawatu kama hawa. Hivi hizi shule binafsi kama hizi St. Mary, st. fatuma etc nazo huwa wanapata mitaala wapi? au wanatoka na mitaala yao kiaina? ni nani anaregulate hizi shule?
wale wanachukua cream wanaacha makapi,mimi siwasifii kuwa wanajua sana kufundisha kwa sbabu wanachukua watoto ambao tayari wana upeo/ufahamu mzuri.kwa hiyo huku st kayumba ndo kunakuwa na mixer so zero znakuwepo alikadharika div 1
 
Elimu imechafuliwa na siasa. Ukiwapata wanasiasa wasio heshimu wataalam ni tatizo. Je, tutengeneze agency ya elimu itakayoratibu elimu bila kuingiliwa. Tuweke utaratibu mgumu kwa mtu mmoja kuamka na kubadili syllabus. Mtakumbuka Mungai kufuta masomo ya biashara na ku- combine sayansi.
Tuanze sasa kuhakikisha form four hafundishi popote hata kwa division one km tulivyoweza kufuata UPE.
KIBOKO YENU NI KATIBA MPYA HAPA TUTA TAFUTA MCHAWI WAKATI WACHAWI NI SISI WENYEWE
 
Elimu imechafuliwa na siasa. Ukiwapata wanasiasa wasio heshimu wataalam ni tatizo. Je, tutengeneze agency ya elimu itakayoratibu elimu bila kuingiliwa. Tuweke utaratibu mgumu kwa mtu mmoja kuamka na kubadili syllabus. Mtakumbuka Mungai kufuta masomo ya biashara na ku- combine sayansi.
Tuanze sasa kuhakikisha form four hafundishi popote hata kwa division one km tulivyoweza kufuata UPE.
Siasa au wanasiasa ndio muongozo wa nchi. Unapozungumzia ILANI YA UCHAGUZI, ujue unazungumzia nini. Kiufupi unazungumzia jinsi nchi itavyoendeshwa katika suala la maendeleo ikiwepo na elimu. Wanasiasa tu ndio wanaopanga ni asilimia ngapi ya bajeti ya nchi iende wizara ya Elimu, ni 3%, 10% au 20%. Na huu ndio ukweli wa ubora wa elimu. Huwezi kuwatoa wanasiasa katika suala la elimu.

Pengine wenye makosa na wakulaumiwa ni wananchi ambao huchagua chama kimoja kuongoza nchi yetu pamoja na kutoridhika na masuala mengi ikiwa ni pamoja na elimu. Inawezekana wananchi wameridhika na kiwango cha elimu kilichopo ndio maana huwapa dhamana hao hao kila uchaguzi, au pengine wananchi wameyapa kipao mbele mambo mengine ya maisha yao nje ya elimu. Hii ndio gharama ya demokrasia.

Kwa vyo vyote itavyokuwa, wananchi wapo sawa, ila wewe usifikirie kutenga siasa na mpango wa maendeleo wa elimu.
 
Tatizo la elimu kama lipo kwa nini halishughulikiwi? Ina maana hakuna wataalamu? Mbona kila siku wanasomeshwa? Tunasomesha wataalamu wengi sana hatutakiwi kuwa na sector isiyokuwa na wataalamu WA KU-SOLVE PROBLEMS. Sio kuandika mada. Ni aibu kuzuzungumzia hili jambo miaka nenda rudi. Let us do it, find a solution and stick to it.
.
Nachangia mawazo yatakayomsaidia mleta mada kuboresha hoja yake. Mchango wangu unazingatia text niliyoinukuu hapo juu. Mpaka mwaka 2012, kati ya Watanzania milioni 50 ni asilimia 2.56 pekee walikuwa na elimu ya kidato cha nne au zaidi. Yaani, ama form iv, au form v, au form six, au mwaka wa kwanza chuo, au mwaka wa pili chuo, nk. Hii ni sawa na watu milioni kama 18. Swali ni hili: Je, mahitaji ya rasilimali watu hapa Tanzania kwa sekta zote na kwa mpigo ni kiasi gani? Kasi ya kusomesha ni kiasi gani? majirani zetu wanayo asilimia ngapi ya wasomi wa aina hii? Tuendelee kutafiti.
 
mkuu Augustine Moshi kutoka ufaulu wa 19% mpaka 48% huko ni kuongezeka kwa kiwango cha elimu kwa TZS (Tanzania Standards) lakini je hiko kiwango cha elimu tunachotoa kwa watoto wetu kitatuwezesha kukidhi mahitaji yetu ya ndani pamoja na ya kimataifa?




hivi mjadala hapa unahusu ubora wa elimu waliyopata hao wahitimu wa std vii, au unahusu kiwango walichofikia cha elimu???
 
Badala ya kusema nani alaumiwe...sema tufanye nini kupandisha kiwango cha elimu...
Lawama na kunyoosheana vidole havitasaidia...
Tuliteleza wapi je tufanyeje kujizoazoa na kusonga mbele...?

Nimekumbuka Toyota 2009 walipopata skendo ya kutengeneza gari zenye defects ...
CEO alisema kuwa siku waliyoamua kupanua soko (hence production) ndio walipokubali kushusha quality ya magari yao...
Sasa wakaishia kukosa imani ya wateja na ku recall thousands of cars duniani...juzi kati tena wame recal 3.37 million cars kwa sababu ya defects za air bags na emissions...quantity ni sumu ya quality...fikiria hasara wanayopata...sijui kwa nini wamejua sababu lakini hawataki ku learn...
Hata wewe hujasema tufanye nini!
 
Back
Top Bottom