Kumbe kuna watu wako kwenye payrol,basi kweli bongo inachunwa,kwani icho chombo kisibadili mitaala inakuwaje masomo mengi yote bado wanatumia vitabu vya miaka 47,kwa nini elimu aiendani na wakati.nimepata nafasi ya kuongea na wahitimu wa vyuo vyetu bongo,wengi wao wanaonekana hawajiamini,awawezi hata kujieleza,mtu kasomea uchumi ajawahi hata siku moja kufanya kazi sehemu yoyote ile,katika masomo ayo kasomea tax returns jinsi ya kutengeneza tax returns,ambazo sidhani wengi wao kama watafanyia kazi,hivi kwa nini mwanafunzi wa chuo anayejifunza mambo ya kujenga na kuchora michoro ya ujenzi wasipate ata mienzi 3 ya kufanya kazi katika shirika la nyumba ili apate kufanya kwa vitendo vitu alivyosoma,matokeo yake utakuta mtu ambaye hakusoma hata kidogo anatengeneza michoro na kujenga nyumba vizuri kuliko yule aliyepoteza miaka 5 chuoni.
Cha kusikitisha zaidi watunafunzi wengi Bongo ni wezi wa mitiani,utakuta mtu anaiba kuanzia darasa la saba mpaka chuo,walimu kuuza au kuonga majibu ya mitihani ya taifa,matokeo yake tunawasomi wengi feki wasio na uwezo wowote na ndio maana nchi inazidi kuwa masikini,mtu anatumwa akanunue mashine ya umeme badala ya kuangalia price ya mashine ile kila nchi inauzwa kiasi gani atatoa dili na tutanunua 4x ya thamani alisi ya kitu hicho,mfano Richimond,Rada,pantoni,ndege,nk .