HOJA Kivuko cha MV Magogoni kipo wapi? Bado tu kipo kwenye matengenezo?

HOJA Kivuko cha MV Magogoni kipo wapi? Bado tu kipo kwenye matengenezo?

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Habari Mkuu naomba kuwasilisha kero kwenu leo hii. Mimi ni mkazi wa KIGAMBONI nadhani kwa sasa Kigamboni ina mbunge mpya anitwa somebody SANGA baada ya kifo cha DR. NDUNGULILE.

Kuna kero ya kivuko hapa na hatujui nani atatusemea ikiwa mbunge mwenyewe hatujawahi kumsikia hata Bungeni akichangia hoja. Hapa kwa sasa kipo kivuko kimoja cha serikali [MV. KAZI] na vilipaswa kuwa viwili pamoja na kila cha [MV. MAGOGONI] hivi ndo vivuko vya umma vyenye unafuu kwa ajili ya watu wa kipato cha chini ndo vinachaji 200 ukiachana na vile vya BAKHRESA [SEA TAX] ambavyo ni Tsh. 500.

MV MAGOGONI kilipelekwa KENYA [MOMBASA] kwa matengenezo tangu Mwaka 2023 kwa kumbukumbu zangu huku kikipitishwa Bungeni na Bajeti yake ya kati ya Sh BILIONI 11 kama sijakosea.

Kuna mbunge aliwashauri kuliko kwenye kutumia gharama hizo kubwa kurekebisha kwanini kisitengenezwe kingine lakini Makofi mengi bungeni yalipitisha kikarekebishwe waziri wa uchukuzi akiwa MAKAME.

Matokeo yake hadi leo MV MAGOGONI na bajeti yake ya Billions of money hakijulikani kilipo na kuko kimya hakuna mbunge wa kuhoji. Hivi hii nchi inaelekea wapi??

Ikituokea MV KAZI imepata hitilafu inatulazimu watu kutumia gharama za ziada kwa SEA TAX za Bakhressa na yeye pia vyombo vyake vilizidiwa na foleni kubwa hadi usiku.

Je, MV. MAGOGONI kilipopelekwa Kenya [MOMBASA] kwa matengenezo kiliuzwa moja kwa moja? Mapema mwaka huu 2026 walisema kinaratajiwa kutejea Februari hadi Aprili, lakini imepita miezi mitatu sasa kimya.
 
Back
Top Bottom