Mr George Francis
JF-Expert Member
- Jun 27, 2022
- 279
- 512
Kila nafsi iliyoonja uhai lazima itafikwa na umauti. Sisi sote tutakufa. Hakuna mtu atakayeondoka hapa duniani akiwa hai.
Hii ni lazima na sio hitari. Sio mtoto sio mkubwa. Sio Kijana sio mzee. Sio mwanaume sio mwanamke.
Sio mfalme wala mtumwa. Sio tajiri wala maskini. Sio mwerevu sio mjinga. Sio kiongozi wa dini wala muumini. Imeandikwa "KILA NAFSI ITAONJA UMAUTI."
Kifo kimetuweka binadamu wote kwenye mizani sawa. Hakuna mjanja anayeweza kukiepuka kifo siku yake ikifika.
Lakini kuwepo kwa kifo isiwe sababu ya kuishi kwa huzuni ila iwe sababu ya kutufanya tuishi maisha yenye maana zaidi.
Ukweli kuhusu kifo uwe kama kichocheo cha kuishi maisha yenye maana mbele za Mungu.
▪︎Kuwa mwenye upendo wa dhati kwa watu wote.
▪︎Kufanya kile kinachokuletea furaha na manufaa kwa wengine.
▪︎Acha chuki dhidi ya wengine.
▪︎Usiwatendee wengine ubaya.
▪︎Ishi maisha ya kuacha alama chanya, hata kama ni ndogo.
Kifo kinakuja kwa kila mtu, lakini jinsi tunavyoishi kabla yake ndiyo inayotofautisha.
Mwenyezi Mungu awapumzishe mahali pema peponi ndugu zetu wote waliotangulia mbele za haki.
Mbinguni tunakwenda kwa neema. Mungu atujalie nasi mwisho ulio mwema na atupe neema ya kuiona pepo kama yalivyo mapenzi yake
AMINA.