Kituo cha afya chazinduliwa bila choo Ikungi, Singida. MoH mko wapi?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Na Gregory Jumbe Mahanju,


Tunaambiwa kua uyaone, tembea uone mengi, ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni. Hizi methali nilipokua mdogo nilidhani tu misemo tu ya waswahili làkini kumbe ni ukweli wenyewe unaotendeka kwenye jamii yetu.

Katika hali ya kustaajabisha kabisa, baada ya Malalamiko ya wananchi ya kuliwa kwa pesa za TOZO zilizotolewa na serikali shilingi 500 nchi nzima kwa ajili ya ujenzi kwa vituo vya Afya, huko Singida katika wilaya ya Ikungi, kata ya Ntuntu kwamba ujenzi wa kituo cha Afya Ntuntu unasuasua na kulazimu mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Ndg Miraji Jumanne Mtaturu fanya ziara ya kushtukiza na kukuta Madudu kibao yaliyoleta wasi wasi kua pesa za kituo hicho zinaliwa maana wananchi hawakuwahi kupewa taarifa za ujenzi wa kituo hicho, Risiti za manunuzi ya vifaa vya kituo hicho hazikuoneka, Ununuzi wa vifaa tofauti na ramani ya ujenzi ilivyotawataka.

Kwa bahati mbaya sana Watendaji wa serkali yetu walivyowageiza wananchi kua ni wajinga, waliita timu kutoka TAMISEMI nà kuiandalia taarifa yao iliyopotosha ukweli halisi. Timu iliulyoka TAMISEMI haijulikani ilipewa zawadi gani ikaishia kusema ujenzi unaendelea vizuri. Kwenye hili kuna haja ya TAKUKURU kutoka makao makuu kufanya uchunguzi kuujua ukweli ambavyo TAMISEMI walipotoshwa..TAKUKURU wa kutoka makao makuu kwa sababu wa ndani ya Wilaya hiyo inasemekana wako pamoja na DED.

Katika hali ya kustaajabisha isiyokuwa ya kawaida, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo ambaye ndio wananchi wana wasi wasi naye kuhusu Kusuasua kwa kituo hicho, alitoa maelekezo eti Kituo hicho ambacho hakijakamilika kuanza kutumika, Yaani kitu kianze kutumika choo hakuna, mifumo ya maji hakuna, umeme haujaunganishwa,majemgo yenyewe hayajakamilika, vumbi tupu kila mahali. Mtu mzima unajiuliza, hii michezo ya watendaji wa serikali kuchezea maisha ya wananchi mpaka lini? Haya ndio maisha bora kwa kila mtanzania? Unaanzaje kutoa huduma za afya hakuna maji, Choo wala umeme? Hivi huku ni kutoa huduma au kuongeza matatizo?

Kwa taarifa zilizopo ni kwamba DED alitoa maelekezo ambayo anaonekana kua ni siasa bila kuzingatia utaalam kituo hicho kianze kutumika ili kuficha Madudu yake ndani ya kituo hiko. Hii ni danganya Toto kwa wasiofika ili ionekane huduma zinatolewa kufumba macho watu wasifustilie ubadhirifu wa pesa za umma ndani ya kituo hicho. Tafadhali TAKUKURU makao makuu hivi kitu isiachwe ikapita wakati jamii inateseka.

Alipoulizwa Mkuu wa Wilaya hiyo ndugu Jery Muro kuhusu upotoshwaji waliopewa timu kutoka TAMISEMI ni tofauti na taarifa ya Mbunge iliyoonesha dalili zote za kutafunwa kwa pesa, naye akajibu kwa jeuri kwamba maswali hayo waulizwe TAMISEMI kwamba wao ndio wenye majibu pesa zimeliwa au Laah. Hawa ndio watendaji tunaosema wanamsaidia Mama na CCM kweli?

WIzara ya Afya(MOH) tafadhalini sana kwenye fanyeni Ukaguzi kwenye kituo hicho mtajionea kwa macho yenu juu ya kinachoendelea Ntuntu huko Singida. Hatuwezi kukubali Afya za wananchi zinachezewa kiasi hiki kwa sababu ya watu wachache wasiokua waadilifu. Hili halikubaliki.


Gregory Mahanju,
mahanjuwanegregory@yahoo.com
KAZI IENDELEE!

=====

Na Dotto Mwaibale, Singida

WANANCHI wa Kata ya Ntuntu Walayani Ikungi mkoani hapa wanatarajia kuanza kupata huduma za kitabibu katika Kituo kipya Cha Afya Cha Ntuntu baada ya ujenzi wake kukamilika kwa asilimia 99.
1669611711129.png

Akizungumza hivi karibuni wakati wa ziara yake Mkurugenzi wa Huduma za Afya Lishe na Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR- TAMISEMI) Dkt.Ntuli Kapologwe amesema ifikapo jumatatu ya Novemba 28 mwaka huu kituo hicho kiwe kimeanza kazi na kuhudumia wananchi.

Aidha ameeleza kwamba hatua iliyofikia kituo hicho inastahili kuendelea kutoa huduma kwa wananchi wa maeneo hayo wakati vitu vidogo vidogo vilivyobaki vikiendelea kukamilishwa.

Hata Hivyo Dkt.Kapologwe ameagiza Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwa kushirikiana na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida kuendelea na maandalizi ya kupokea vifaa tiba ili ifikapoa Novemba 28,2022 huduma ziwe zimeanza na wananchi wanapata matibabu.

"Tumeambiwa jengo limefikia asilimia 99 kukamilika kwa hatua hii ni lazima huduma zianze kutolewa hata kama kuna vitu vichache vya kumalizia " alisema.

Hata hivyo ameendelea kueleza kwamba Serikali ipo hatua ya mwisho ya kuleta vifaa tiba katika kituo hicho ambapo amesema kufikia jumatatu vitakuwa vimeshafika.

"Serikali ipo kwenye hatua za mwisho za uletaji wa vifaa tiba mbalimbali katika kituo cha afya hivyo wananchi waanze kupata huduma" alisema Dkt. Kapologwe.

Dkt. Kapologwe ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi na timu nzima ya usimamizi wa ujenzi wa kituo hicho cha afya kwa ukamilishaji mzuri wa majengo matatu ya awamu ya kwanza (Jengo la Wagonjwa wa Nje OPD, Jengo la Maabara na Kichomea Taka) ambao mpaka sasa umekamilika kwa asilimia 99%.
1669611732382.png

Aidha majengo matatu mengine ni pamoja na Jengo la Wodi ya Wazazi (Maternity), Jengo la Upasuaji (Theatre) na Jengo la Kufulia (Laundry) ambapo ujenzi huyo umefikia zaidi ya asilimia 60% huku Dkt.Kapolongwe akiwataka kuongeza kasi ya ujenzi ili kufikia Disemba 30 majengo hayo yawe yamekamilika.

Ujenzi wa vituo vya afya ni moja ya mkakati na kipaumbele cha serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya katika maeneo ya karibu na makazi yako.
 
Hapo kuna harufu ya upigaji,ccm na upigaji ni uji na mgonjwa.
Waje hao TAKUKURU makao makuu,wa wilayani ni walewale
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom