Kituko cha mwaka - Wananchi wa Vunjo wamtuma mwakilishi wao Bungeni kuomba kupewa rasmi ardhi na Serikali ili kufanya makazi mapya

Moshi ardhi ni tatizo kubwa, kuna kipindi Nicodemus Banduka akiwa mkuu wa mkoa wa pwani alienda kugombea nafasi ya ubunge kwao moja ya kampeni yake ilikuwa ni kuwatafutia wachaga ardhi pwani.
Kimei kama angepewa uwaziri angefanya kama aalivyofanya CRDB kujaza wachaga, mapovu ruksa.
 
Yaani Mbunge wa Vunjo mwenye PhD anamwomba waziri wa ardhi awapatie Wachagga wa Vunjo ardhi kwingineko katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sababu ni ili walime kwani kwao wamegawana ardhi kwa mila zao na kujikuta na vipande vidogo sana ambavyo mtu hawezi kulima. Eti wamesongamana, si mpunguze kuzaana.

Hivi huyu Mbunge na hao wachagga wenzie hawaijui Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu freedom of movement?

Hivi yeye mhe. Dr Kimei alipojenga Dar es Salaam na kupata ardhi kubwa Dar mbunge wake wa wakati huo ndio alienda bungeni kumuombea hiyo ardhi? Yaani kabisa anataka annexation ya mkoa wa Kilimanjaro! Au Vunjo nzima ni registered company?

Hivi hao Wasukuma waliojaa huko Mbeya na Morogoro waliomba wapewe hayo maeneo bungeni kupitia wawakilishi wao?

Kwa fikra zake kama hizi huyu bwana hafai kabisa kuwa kiongozi wa juu katika taifa hili kutokana na misingi yake.
kuna wengine walipelekwa Sumbawanga wakati wa awamu ya kwanza
 
Maeneo mbona watu wanauziana na kuhamia tu kwa utaratibu nchi nzima.

Unasubiri serikali ikupatie eneo kwani wewe mkimbizi wa Burundi?
Nadhani watu hawa waliitaji eneo kubwa sana mfano wa mkoa nadhani hivyo nadhani pia walipenda hata kuliita eneo hilo jina la kichagga
 
wewe kweli wa jana. kwa taarifa wachaga waliwahi kuhamishiwa handeni, mpanda, kilosa nk. wakati wa awamu ya kwanza ili kuondoa msongamano. Haijaleta ubaguzi wowote na wamechanganyikana na wenyeji wao. Watu wa sasa ndio wabaguzi. NENDA HUKO UKACHUNGUZE
Sasa kama walishahamishwa, na hilo halijaleta ufumbuzi, kwa nini watu wanafikiri kuwahamisha tena watu ndiyo kutaleta ufumbuzi?

Tanzania imetoka kuwa nchi ya watu milioni takriban 30 miaka 20 iliyopita, mpaka watu milioni 60 sasa.

Tukiendelea kuzaana hivi, katika miaka 20 ijayo, tutafikia watu takriban milioni 120.

Tukijaa kote tutaenda kuomba ardhi Congo?
 
Mimi sio mchagga lakini nimeishi moshi zaidi ya miaka 10 sasa na sina mpango wa kuhama. Tatizo kubwa la wachaga ni mila zao za kupenda kila mtoto (wa kiume na sometimes hata wa kike) lazima agawiwe eneo "kihamba" nyumbani kwao na ajenge huko.

Kiuhalisia, mkoa wa kilimanjaro hauna tatizo kubwa la ardhi naweza kusema tatizo lipo huko juu vijiji vinavyozunguka mlima kilimanjaro. Kule watu wanapapenda kwasababu ya udongo mzuri wenye rutuba na hali nzuri sana ya hewa, vijito visivyokauka na mazingira ya kuvutia ya kijani kibichi.

Lakini ukishuka uwanda wa chini barabara ya moshi -dar na moshi - arusha utaona maeneo makubwa sana ambayo watu wameyageuza mashamba ya mahindi na wakaaji ni wachache sana.

Olu in olu mkoa wa kilimanjaro ni mkoa wa tatu kwa udogo kwa Tanzania bara, ukizidiwa udogo na dar na mwanza tu.
 
Yaelekea mtoa mada ni mtoto sana au ukabila unakusumbua sana.

Ngoja nikuelimishe kidogo, miaka Fulani ya nyuma kwenye 70's baba wa taifa mwalimu Julius kambarage nyerere aliwahi kuwashauri wachagga wasigombee ardhi ndogo iliyoko Kilimanjaro Bali waende kutafuta ardhi kwingine maana Tanzania ni kubwa na ardhi ni nyjngi.

Kwenye mchakato huo alitoa ardhi Rukwa, sehemu ambayo kwasasa ni mkoa mpya wa katavi, kuna kijiji ambacho wakazi wake asilimia 90 ni wachagga kutoka mkoa wa Kilimanjaro, eneo hilo liliwahi kuonyeshwa na Tanzania safari channel kuna mto unaitwa mto mapacha!

Pia kuna maeneo ya mkoa wa morogoro ambayo wachagga waliwahi kupewa ardhi sikumbuki ni eneo gani kwajina, kwahiyo utaratibu wa kuomba na kupewa eneo la ardhi sio mgeni wala sio shida,

Jifunze historia mkuu kabla ya kutoa lawama au kulaumu! Ni bora ungeuliza kuliko kujifanya much know kumbe ni tabula rasa!
 
wewe kweli wa jana. kwa taarifa wachaga waliwahi kuhamishiwa handeni, mpanda, kilosa nk. wakati wa awamu ya kwanza ili kuondoa msongamano. Haijaleta ubaguzi wowote na wamechanganyikana na wenyeji wao. Watu wa sasa ndio wabaguzi. NENDA HUKO UKACHUNGUZE
Wa jana ni mbunge wao, na ndiyo maana comments nyingi zinauliza kwani wamezuiwa kwenda kwingine? au wanataka watengewe eneo wawe ni wao peke yao?
 
Back
Top Bottom