Kitu gani ni dhambi???

Sawa tu dada,

Ila kama wanajamii wote ni wahalifu...kwa nini wengine waishi keko na kufungiwa kama kuku wa mayai wakati wengine wanatesa uraiani???



Wanakwambia lolote ufanyalo... wewe sio mhalifu mpka ukamatwe... bad statement but soo true!!

Na pia level za uhalifu zapishana DC....
 
Wanakwambia lolote ufanyalo... wewe sio mhalifu mpka ukamatwe... bad statement but soo true!!

Na pia level za uhalifu zapishana DC....

Au labda niulize hivi,

Kama wote tu wahalifu, nani ana jukumu la kubeba kipimo cha ku-determine level ya uhalifu wa mwenzie??

Au tuseme hivi,

Kama sote tu maiti...kwani maiti wengine wapekekwe mortuary?
 
Duhhhhhhhhhhh.....Lizzy...Umeniamsha usingizini mdogo wangu!!

My take...
1. Ukimuibia RA ni poa tu....unafanyiwa bonge la party!!
2. Kama wewe na mwenzi wako wote mnabanjua ile amri ya God kwa kwenda mbele ni poa tu...
3. Mengine ukifanya kwa kiasi na kusababisha moderate damage ni ruksa...

Tuendeleee...Akili inaanza kurudi sasa!!


Babu nafurahi kusikia kwamba Akili inaanza kuridi sasa!!

Hapo kwa kumwibia RA yani safi kabisa...lolzz!

Mi ndio maana nikisikia kibaka kachomwa moto kwa kukwapua sijui simu ya laki mbili wakati aliyekwapuliwa ana uwezo wa kununua nyingine wiki ijayo naumia sana.Au majambazi yaliyokua yanaiba bank yameshutiwa yote natamani isingekua hivyo maana wanaoibiwa kule haswa haswa ni mafisadi!!!Ila wale wanaovamia watu makwao na kawacherenga mapanga hao kwakweli hua wananiudhi!!!
 
There are currently 6 users browsing this thread. (4 members and 2 guests)

ukimwacha mmoja tu hapo siye wengine tukalale.....tusije tukatenda dhambi hapa......

Binadamu kweli tuna akili nyingi sana hadi zinatushinda (nimecheka hadi wanangu wanastuka usingizini.....)!!

Sasa hapo tunagawanaje mkuu????? Au tunahitaji Berlin conference!!
 
Au labda niulize hivi,

Kama wote tu wahalifu, nani ana jukumu la kubeba kipimo cha ku-determine level ya uhalifu wa mwenzie??

Au tuseme hivi,

Kama sote tu maiti...kwani maiti wengine wapekekwe mortuary?


Mzee DC sababu sio maiti zoote huenda mortuary... Nyingine huzikwa hapo hapo hamna haja... nyingine haijulikani kua ni maiti mpaka harufu itoke... otherwise mnaweza hata msijue kua ni mzoga...
 
Sweetie nisha kuambia mda... tangulia sitachelewa but hutaki naona...lol...

(sasa umeona nimechakachua thread ya Mzee DC?? lol - basi naja sasa hivi...)[/QUOTE]

Usijali AshaDii,

Ni lazima kazi na dawa viende pamoja....

Ngonja nikalale niache kutenda dhambi ya kuwaamsha wajukuu!!

Muda wa daku utanistua sawa ehhh????
 
Usitamani chochote cha jirani yako, wala mke wake, wala ng'ombe wake wala punda wake
hii ni amri ya ngapi?
 
Wanakwambia lolote ufanyalo... wewe sio mhalifu mpka ukamatwe... bad statement but soo true!!

Na pia level za uhalifu zapishana DC....

Hah! ADI umenikumbusha kile kitu cha pressumption of innocence, kwamba "an accused is innocent until proved guilty"! Na mbaya zaidi unaweza ukaprove alafu ukaambiwa kuna exceptions! Lol! Kaazi kweli kweli!
 
Naomba mnisamehe ndugu zangu...Hii akili ya 1947 ime-jam!

Hivi kwa mazingira yetu ya sasa ya dot com, ufisadi, ulegelege wa wakulu (Maranya kaita urojo rojo), uzembe, umbeya, kupigana mabao, kungonoka zaidi ya wanyama na kila aina ta ya vituko....kitu gani tunaweza kusema kuwa ni dhambi??

Naona kama huu msamiati sinao tena ingawa walau nachukua uongo (ukiacha ule uongo uliobarikiwa tunaotumia mimi na bibi)!!


Babu DC (1947)

tencom06.jpg
...dhambi ni chochote kinachomkasirisha Mwenyezi Mungu ila dahhh?...mnh acha tu!

 
Mbu hii kitu umeipata wapi maana inafanana na ile aliyokabidhiwa Moses pale mlimani
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
zingatia amri kumi za Mungu tu
na ktk amri zote, ilio kuu ni upendo.
Upendo huvumilia, hauhesabu mabaya, pia upendo "husitiri wingi wa dhambi"
haya ni baadhi tuu ya mafundisho/nukuu ktk Bible, that means tangu zamani wakati Bible inaandikwa dhambi zilikuwa nyingi tuu! kwa akili zetu wenyewe hatuwezi kuzishinda, twaokolewa kwa neema tu.
 
Naomba mnisamehe ndugu zangu...Hii akili ya 1947 ime-jam!
Hivi kwa mazingira yetu ya sasa ya dot com, ufisadi, ulegelege wa wakulu (Maranya kaita urojo rojo), uzembe, umbeya, kupigana mabao, kungonoka zaidi ya wanyama na kila aina ta ya vituko....kitu gani tunaweza kusema kuwa ni dhambi??

Naona kama huu msamiati sinao tena ingawa walau nachukua uongo (ukiacha ule uongo uliobarikiwa tunaotumia mimi na bibi)!!

Babu DC (1947)

Mkuu mbona umetupa mtihani mkubwa ambao naamini hata wale wanazuoni wa imani ukiwaambia wakuambie dhambi zao watashindwa kutaja...na kuishia kusema vitu ‘generic'.

Na sisi ambao tumeshakata tiketi ya kuwa kuni za motoni ukiuliza dhambi tutakwambia moja tu inayohusu yale yote yanayolenga kuvunja amri ya kutokula tunda la kati bila ruhusa maalumu..

Binafsi naona ziko dhambi nyingi nyingi sana, zilizotajwa na wadau hapo juu ni baadhi tu ambazo jamii imezipitisha...Lakini mbona hamtaji zile ambazo ziko lakini jamii haizioni? Kwanini tusitaje zile hisia toka moyoni ambazo zinatusuta daima?

Hebu fikiri unaenda kazini kwenye kagari kako.. uko peke yako unakula kiyoyozi na joto la bongo huku ukiwaacha wengine wamejazana kwenye daladala hata hewa hawana..Hiyo siyo dhambi?." Eti..Moyoni unajisemea wakiangaika kama mimi basi nao watapata usafiri wa kiyoyozi" ....

Wakati wa birthday yako; Christmas, Pasaka, Eid au wakati wa mfungo mtukufu wa Ramadhani..yaani mara moja kwa mwaka ..unaandaa chakula na mapochopocho na kula pamoja na watoto yatima..picha kibao kwenye blog n.k... halafu unawaacha waendelee kufa na njaa kwa siku zilizobaki 364 hadi mwakani..hiyo siyo dhambi?

Unaugua..unalipia ndugu yako pale kwenye hospitali ya ghali. ingawa unashindwa kumwacha ndugu yako afe.. lakini kwa hela ya kumwona dokta tu pale hospitali ya hela ungeweza kutoa huduma ya dawa za malaria kwa kijiji kizima kwa siku 2 kule nyanda za juu..Hiyo siyo dhambi?

Hebu fikiri ..kutokana na mgawo wa umeme..umenunua kagenerator kako..kanapiga kelele mtaa mzima..watoto hawalali..kina mama wajawazito vitoto vinacheza tumboni kwa ajili ya kelele za kagenerator yako.. hiyo siyo dhambi?

Mkuu mimi binafsi huwa nikifikiri na kuona hata nifanye nini nishakuwa kuni za kule Jehanamu kwenye Moto..labda Mola anionee huruma na kuhisi kuni mimi nimelowa na mvua na kunitupa porini ..yaani hata kama sitaenda kwenye pepo nikiwa na zagaa zagaa huko porini mbinguni powa tu…

Kwa upande wa pili nikiachana na fikra za kuwa kuni wa jehamanu .....namuunga mkono LizzY
Nadhani kila ambacho sio haki kumtendea mwenzako/wenzako!!!

Na pia namuunga mkono AshaDii
Dhambi Mzee DC ni relative term... kilicho dhambi kwa huyu sio dhambi kwa yule... hio kutokana na ukweli kua kila jamii ina Imani zake na beliefs zinazowaongoza ni jinsi gani waishi kati ya mtu na mtu au jamii na jamii...


Kimsingi kabisa waweza kuta kila litndwalo hapa duniani ni dhambi kwa mmoja na sio kwa mwingine... hivo kikubwa kwa mwanadamu yeyote it is beta asimamie misingi ya tamaduni zake hasa zile ambazo ni muhimu mno katika kumdefine na pia kuendeleza tamaduni...

Hizo comments mbili za dada zetu hapo juu zaweza kupingana kidogo sana..lakini kwa hali halisi ya hapa duniani..ni sawa tu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom