Kitu gani ni dhambi??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitu gani ni dhambi???

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Dark City, Aug 11, 2011.

 1. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Naomba mnisamehe ndugu zangu...Hii akili ya 1947 ime-jam!

  Hivi kwa mazingira yetu ya sasa ya dot com, ufisadi, ulegelege wa wakulu (Maranya kaita urojo rojo), uzembe, umbeya, kupigana mabao, kungonoka zaidi ya wanyama na kila aina ta ya vituko....kitu gani tunaweza kusema kuwa ni dhambi??

  Naona kama huu msamiati sinao tena ingawa walau nachukia uongo (ukiacha ule uongo uliobarikiwa tunaotumia mimi na bibi)!!


  Babu DC (1947)
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Nadhani kila ambacho sio haki kumtendea mwenzako/wenzako!!!

  Yote ambayo yanafahamika na kukubalika kwamba ni mabaya kwa kiasi kikubwa (na wengi) hata kama na wenyewe wanayashiriki!
   
 3. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #3
  Aug 11, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Babu hebu fafanua zaidi dhambi kwa nani? Maana kuna
  Dhambi kwa mpenzi/mwenzi/spouse,
  Dhambi kwa mwajiri/waajiri
  Dhambi kwa MUNGU

  Sasa sijui unataka dhambi ipi Babu yangu..........................
   
 4. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #4
  Aug 11, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hahahah Lizzy umesema sawa mie naona nami kama Babu akili ya uzeeni imechakachuka siku hizi,,,,,,,,,,nlijua kumgomea kufanya kazi mwajiri kwa kuwa sina mafuta/daladala hazendi na hakuna umeme ni sawa; kumchapa kibao fisadi ni sawa kumbe ningechemka!!
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Lizzy,

  Ni yapi hayo?? Nimesema akili imegota Kigoma mwisho wa reli mwenzenu!!
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  MJ1 mjukuu wangu mpendwa...umesoma vizuri kweli?

  Mbona nimeshasema kuwa akili ya Babu ime-jam?
   
 7. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  zingatia amri kumi za Mungu tu
   
 8. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #8
  Aug 11, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Rejea maandiko ya mungu.
   
 9. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hivi bado zipo au zimeshafanyiwa uchakachuaji??
   
 10. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #10
  Aug 11, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Dhambi Mzee DC ni relative term... kilicho dhambi kwa huyu sio dhambi kwa yule... hio kutokana na ukweli kua kila jamii ina Imani zake na beliefs zinazowaongoza ni jinsi gani waishi kati ya mtu na mtu au jamii na jamii... Nasema Dhambi ni relative sababu wanaohusika na kufafanua hiki ni dhambi ama sio dhambi ni wale ambao wana dini zao (hivo kuongozwa na vitabu vya dini) na kuna wale ambao hana imani na Mungu yoyote BUT still nae huona kua kitu fulani ni dhambi au lah!

  Hivo DC kuchanganikiwa kwako kujua lipi dhambi na lipi sio ni kutokana na kubadilika kwa hii dunia ya sasa- dot com hasa (Globalised vilage in the real sense)... Tumechanganyikana watu wa race/imani/mazingira tofauti kabisa!! hivo kubadilika kwa tamaduni za maeneo na mataifa tofauti imekua sasa ni inevitable... na wale walio ni world powers; wakihakikisha kua wana tawalisha culture zao zaidi... Mfano mzuri saana ni issue nzima ya Ushoga! Sad.

  Kimsingi kabisa waweza kuta kila litndwalo hapa duniani ni dhambi kwa mmoja na sio kwa mwingine... hivo kikubwa kwa mwanadamu yeyote it is beta asimamie misingi ya tamaduni zake hasa zile ambazo ni muhimu mno katika kumdefine na pia kuendeleza tamaduni...
   
 11. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2011
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  S, ile ya upendo ni ya ngapi ktk kumi?

  narudi baa...
   
 12. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Yapi?

  Na yanahifadhiwa wapi ambako wengi wetu hatuyaoni???
   
 13. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #13
  Aug 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hahahaha....MJ mami hata kumdanganya mwajiri kwamba umeshindwa kwenda kazini leo kwasababu umekwama kwenye foleni ya mafuta ni dhambi kwasababu UMEDANGANYA japo uongo wenyewe hauna madhara kiviiiile!!!

  Babu DC nikwambie kitu...mi hua nasema hivi dhambi ni dhambi iwapo kilichofanyika kitakua na madhara either kwa mtendwa au mtenda!Na ukubwa wa dhambi (kwangu mimi) unaonyeshwa kwa ukuvwa wa dhara litakalotokana na hicho kitendo!!

  Kwa maelezo hayo naomba nikwambie dhambi kwa nnavyoina mimi na sio collectively!!
  Kumdanganya mwajiri iwapo uwongo wako unamcost yeye...if not ahhh well kila mtu anastahili break now and then.

  Kumwibia mtu ambae kureplace kile ulichomwibia itakua kazi sana kwake.Mfano ni kumwibia mama mfanya biashara wa nyanya za reja reja mtaa kwa mtaa simu ya sh. 40,000 maana kuipata alijipinda sana so thats to me is unfair.Ila ukimwibia mwingine ya million kama 20 bank ahhj naona poa tu hata kama ni mimi nimeibiwa!Na nilishawahi kuibiwa na mwizi wangu nikamjua ila nilimsehe kwa sababu hii hii!

  Kumcheat mtu ambae ni mwaminifu kwako..,ila kama wote ndo wale wale wakomoane tu!!

  Kumsingizia/kumtuhumu mtu kitu ambacho ni uongo!!Inamuumiza sana mhusika!!!

  Kutamani kitu usicho na uwezo nao hata kufikia kufanya mambo ya ajabu ili kukipata!!Mf. Kumwendea mwabaume kwa mganga...kuiba...kudhulumu...n.k

  Kumdhulumu yatima...mtu ambae hana kwingine kwa kukimbilia so unfair!!

  Kumsingizia/mpakazia mtu kitu hata kufikia kumharibia sifa yake na kumchafua kwenye jamii/familia haifai kabisa!!

  Chuki mbaya mpaka kufikia kumuumiza mtu iwe physically au pschologically.Ila kama unamchukia tu mtu basi heey go ahead and ridhisha moyo wako!

  Kulaani/kuita watoto majina ya ajabu ajabu mpaka wakafikia kukua na hizo character mbaya ulizowatupia!!

  Kuua kwa kukusudia!

  Kumprovoce mtu hata akafanya kitu ambacho mwanzoni hakuwahi kukifikiria/hakuwahi kudhani kiko ndani ya uwezo wake kama kuua.

  Kumdharau mtu yeyote yule ambae bila yeye usingekua hapo ulipo.Mzazi/ndugu/rafiki/jirani/mwalimu n.k

  Dah ntaendelea baadae.....
   
 14. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #14
  Aug 11, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ahsante sana Asha kwa ufafanuzi wako mzuri saaana!!

  Sasa kwa nini tusivunje magereza ili wote tubanane uswahilini??? Kwa sababu wao (wanaoishi keko na segerea) na sisi hatuna tofauti au??
   
 15. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #15
  Aug 11, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  Quran + bibble.
   
 16. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #16
  Aug 11, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Vinapatikana wapi? Viko accessible na applicable kwa kila mtu?
   
 17. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #17
  Aug 11, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Tunarudi pale pale kua kila jamii ina tamaduni zake... na hio ya wahalifu ni moja ya tamaduni ambazo ipo katika kila jamii ya hapa dunini thou end result ya kua judged ni tofauti.... Hivo jamii yetu uhifadhi wahalifu huko (thou sio woote ni wahalifu..) Issue nzima ya kudefine dhambi iko katika issues za mila/customes na the like... Mfano... yule mama/baba anaetaka kukeketa binti yake hufanya that out of love sio kwa kumkomoa... BUT majority ya jamii inakua against because nao wana interest ya huyo huyo binti out of love pia.... Issue kama hio ndo tatizo saana...
   
 18. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #18
  Aug 11, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Duhhhhhhhhhhh.....Lizzy...Umeniamsha usingizini mdogo wangu!!

  My take...
  1. Ukimuibia RA ni poa tu....unafanyiwa bonge la party!!
  2. Kama wewe na mwenzi wako wote mnabanjua ile amri ya God kwa kwenda mbele ni poa tu...
  3. Mengine ukifanya kwa kiasi na kusababisha moderate damage ni ruksa...

  Tuendeleee...Akili inaanza kurudi sasa!!
   
 19. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #19
  Aug 11, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Sawa tu dada,

  Ila kama wanajamii wote ni wahalifu...kwa nini wengine waishi keko na kufungiwa kama kuku wa mayai wakati wengine wanatesa uraiani???
   
 20. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #20
  Aug 11, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Welcome Back!!! lol... Hio statement imenifurahisha...lol
   
Loading...