Kitu gani kilisababisha usijiunge na UDSM?

Kitu gani kilisababisha usijiunge na UDSM?

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
21,237
Reaction score
43,790
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni chuo bora Tanzania. Kiko mbali mno kwa ubora kulinganisha na vyuo vingine. Kikubwa zaidi ni kuwa wanaodahiliwa Mlimani ni vipanga watupu. Bila Div One & Two ni ngumu mno kuwa mwanafunzi wa UDSM. Ni ndoto ya watanzania wengi kusoma pale. Hata mimi ilikuwa ndoto yangu kusoma pale ila haikuwezekana. Nitaeleza kwanini.

Kwa upande wangu nilishindwa kujiunga na UDSM kwa sababu kwenye maombi yangu sikuambatanisha baadhi ya vitu hivyo maombi yangu kutofanyiwa kazi. Nakumbuka siku chache kabla ya Marticulation exam pale Arusha Tech ndo nilipokea majibu kuhusu makosa niliyofanya wakati wa kutuma maombi. Ikabidi nikajiunge na chuo kingine ambacho bado hawakuwa wamefika deadline ya kutuma maombi.

Je, wewe kwanini ulishindwa kusoma UDSM undergraduate?
 
Inategemea unataka kusoma nin,
Kwa watu wa Afya, UDSM huwa hatuiwazi kabisa 🤣 tunawaza Muhas na UDOM tu,

So usiwaze kila mtu mwenye akili anaenda Udsm, huko kwa wanaosomea siasa na vitu vya ajabu ajabu kama mazingira na international relations 🤣🤣
 
Swali linakuhusu wewe,lakini cha ajabu unamuelezea binti yako,Khaa Acha wachina wachukue hii nchi
While my daughter was attending JKT nilimwombea chuo. Sikupenda UDSM kutokana na life style ya pale, though her pass was good enough.

Niliomba chuo kingine
 

Attachments

  • 20250321_222742.jpg
    20250321_222742.jpg
    126.5 KB · Views: 46
Nafasi za kuingia UDSM miaka ya 70/80 zilikuwa chache sana wakati huo Muhimbili Medical School ikiwa moja ya vitengo vyake.

Maombi yangu yalikataliwa kwa msingi huo wa kuchukua watu wachache, kitu kilicho nisononesha sana kwa sababu niliweka matumaini ya kupata.

Barua ya kukataliwa niliyoipokea kutoka UDSM ndio iliyonifanya nitafute vyuo vingine nje ya nchi na nikafanikiwa!.
 
Inategemea unataka kusoma nin,
Kwa watu wa Afya, UDSM huwa hatuiwazi kabisa 🤣 tunawaza Muhas na UDOM tu,

So usiwaze kila mtu mwenye akili anaenda Udsm, huko kwa wanaosomea siasa na vitu vya ajabu ajabu kama mazingira na international relations 🤣🤣
Wenye uchungu kwa kusoma nje ya UDSM utawajua tu..!!
 
Back
Top Bottom