kitu gani kilichokutokea 2017 ambacho hutokisahau?

kitu gani kilichokutokea 2017 ambacho hutokisahau?

Nimepata changamoto ya kutopata promotion kazini inaumiza sana.But Mungu yupo
 
Kumpoteza mamangu mzazi tarehe 12/12/2017. Umekuwa mwaka wenye majaribu sana lakini yote kwa yote namshukuru Mungu kwa wema na upendo wake usio na kikomo. Bila shaka kwa nguvu zake mwaka huu 2018 utakuwa na mibaraka zaidi. Mungu huwa hakosei na uwepo wetu katika sayari hii nzuri unategemea wema na uwezo wake. Tusichoke kumuomba na kumwabudu.
Polesana! Comrade
 
Poleni sana Mkuu na hongera kwa kubadili life style ili uwe karibu na mwenzio.

Mimi sitasahsu ucku wa tarehe 4/4 nikiwa nimelala na mke wangu aliyekua mjamzito wa miezi 6 aliniamsha huku akilia sana kwa maumivu ya tumbo, nilijaribu kumbembeleza ila nikaona hali inazidi kuwa mbaya ikabidi nimpeleke hospital huku akilia njia nzima, kufika hosp madokta wakampokea kumpima wakaona mtt hachezi, wakampeleka theatre, wakampa msaada akajifungua mtt wa kike amekufa, tulikaa pale hadi asbh, tokea siku ile mke wangu amekua mtu wa huzuni sana sometime analia sio yule niliyemjua, imebidi nibadili life style nawahi kurudi nyumbani ilimradi awe anachangamka kidg!
 
Mungu wetu ni mkuu, siku zote
Akufanyie wepesi kwenye kila jambo ufanyalo
Asante mkuu. Bila Mungu sisi si kitu. Amenibariki sana na kunitia nguvu. Naamini Anafanya hivyo hivyo kwako pia. Tuendelee kumuomba na kumtegemea [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Mmh sitasahau Mwezi wa kwanza 2017 nilipo mpoteza baba yangu kipenzi, ambae ndio mzazi pekee nilie kuwa nimebaki nae , baada ya kumpoteza mama yangu kipenzi 2001 kuwa yatima mtihani sana asikwambie mtu .
 
Back
Top Bottom