Mimi sitasahsu ucku wa tarehe 4/4 nikiwa nimelala na mke wangu aliyekua mjamzito wa miezi 6 aliniamsha huku akilia sana kwa maumivu ya tumbo, nilijaribu kumbembeleza ila nikaona hali inazidi kuwa mbaya ikabidi nimpeleke hospital huku akilia njia nzima, kufika hosp madokta wakampokea kumpima wakaona mtt hachezi, wakampeleka theatre, wakampa msaada akajifungua mtt wa kike amekufa, tulikaa pale hadi asbh, tokea siku ile mke wangu amekua mtu wa huzuni sana sometime analia sio yule niliyemjua, imebidi nibadili life style nawahi kurudi nyumbani ilimradi awe anachangamka kidg!