Kitendo cha Mzee Stephen Wasira Kuvunja Sabato Hadharani: Je atapewa adhabu kwa mujibu wa kanuni za Kanisa?

Unasemeje

JF-Expert Member
Apr 29, 2021
249
915
Kwa mujibu wa Kanuni za Kanisa la Waadventista Wasabato, yapo mambo 13 ambayo ikibainika bila shaka kuwa umeyafanya, adhabu yake ni KUFUTWA USHIRIKA au kupewa karipio ( inategemea na situation).

Kitendo cha KUVUNJA SABATO ni miongoni mwa mambo hayo. Kanisa la Waadventista Wasabato linaamini kuwa siku ya Sabato ni siku maalumu kwaajili ya kumwabudu Mungu, kukumbuka kuhusu kazi ya Uumbaji na Ukombozi kama inavyo elezwa katika Maandiko Matakatifu, pamoja na kutenda matendo mema ya kuokoa maisha ya watu kama vile kuwasaidia wagonjwa na wenye mahitaji.

Katika siku ya Sabato, ni marufuku kufanya kazi za kujiingizia kipato, kujihusisha na mambo ya siasa na mengine kwakuwa hayo yote unaweza kuyafanya ndani ya siku 6 za wiki.

Sasa leo, mshiriki wa Kanisa la Waadventista Wasabato ndugu Stephen Wasira Masatu ameamua kuvunja Sabato waziwazi na kwenda kujihusisha na mambo ya siasa ambayo angeweza kuyafanya siku nyingine za juma.

Je kanisa litamshughulikia kama linavyo shughulikia wazinzi?
Screenshot_20230729-224503~3.png
 
Kanisa na Wadventista Wasabato wanajua maandiko na wanajali sana kondoo kama aliwahi kukosea huko nyuma wakamuonya mara kadhaa watamfuta ushirika lakini kama ndio kaanza naamini watamkalisha chini na kumpa maneno ya kumsaidia kurudi kwenye mstari
 
Kanisa na Wadventista Wasabato wanajua maandiko na wanajali sana kondoo kama aliwahi kukosea huko nyuma wakamuonya mara kadhaa watamfuta ushirika lakini kama ndio kaanza naamini watamkalisha chini na kumpa maneno ya kumsaidia kurudi kwenye mstari
Sawa mkuu.
 
Back
Top Bottom