Kitendo cha kutaka kuhamisha familia 400 zinazozunguka eneo la kimondo cha Ndolezi Mbozi bila fidia ni cha kishenzi

Less creative

Kijiji kingeachwa na kuboreshwa ili watalii wakija wapige story na Mashuhuda jinsi kimondo kilivyo piga hiyo siku....mijitu inawaza kupiga
-Hakuna mtu yeyote aliweza ona kimondo cha mbozi kikidondoka. ilikuwa mwaka 1930 ambapo mzee halele aliyekuwa mhunzi wa chuma eneo hilo ndiye mgunduzi wa jiwe hilo.

-Niliwai tembelea eneo la kimondo na nilimuuliza msimamizi wa hicho kimondo sababu za kuto kujua umri wa kimondo hicho toka kimekuwepo ardhini pale. alisema wakati tu kimondo kimegunduliwa kwa wakati huo, udongo wote wa pembeni uliokuwa unazunguka kimondo hicho uliondolewa kimakosa pasipo kujua faida ya udongo katika kupima umri wa kimondo kuwepo pale ardhini sababu ule udongo uliogusana na kimondo unakuwa na layers mbalimbali ambazo zingetumika kutambua umri wa kimondo hicho tangu kimekuwepo pale.

-Mfano ni kimondo cha Hoba kilichopo Namibia kiligunduliwa miaka nyuma kadhaa kabla ya kimondo cha mbozi, ilikuwa mwaka 1920's lakini wameweza kujua umri wa kimondo cha Hoba uwepo wake pale ardhini, ni umri wa miaka 8,0000 iliyopita, hii inatokana na kuto kualibiwa kwa scene ya kimondo hicho.
 
Tatizo ni thamani ya hicho kimondo, material yake ni muhimu
Hakina thamani yo yote zaidi ya kuwa ni chuma ambacho kimedobdoka kutoka anga za mbali! Hivyo watu wanakishangaa kama ambavyo watu wanakwenda kushangaa tembo mbugani.
 
Wazungu walishapa pima hapo chini kuna mali ya kufa mtu iyo ardhi yote ni mali Tupu wakatafuta jiwe la ajabu ili wawatishe eti ni kimomdooo fck kabisa hawa white pple sasa wanataka kurudi kuchimba mali zao huku nyiny mamonky imkiamini hicho ni kimondo na elimi yenu ya mchongo..........
 
Wazungu walishapa pima hapo chini kuna mali ya kufa mtu iyo ardhi yote ni mali Tupu wakatafuta jiwe la ajabu ili wawatishe eti ni kimomdooo fck kabisa hawa white pple sasa wanataka kurudi kuchimba mali zao huku nyiny mamonky imkiamini hicho ni kimondo na elimi yenu ya mchongo..........
Mwehu wewe!🤓😁😂
 
Wazungu walishapa pima hapo chini kuna mali ya kufa mtu iyo ardhi yote ni mali Tupu wakatafuta jiwe la ajabu ili wawatishe eti ni kimomdooo fck kabisa hawa white pple sasa wanataka kurudi kuchimba mali zao huku nyiny mamonky imkiamini hicho ni kimondo na elimi yenu ya mchongo..........
Aisee hivi watu kama nyie mpoo?
 
Project za CCM ndio maana hazinaga matunda sababu zinafanyika kwa roho mbaya na ukatili mkubwa. Pesa za machozi ya watu huwa hazinaga matokeo mazuri.
 
Wananchi wa kijiji cha Ndolezi kilipo kimondo maarufu cha Mbozi wamekuwa wakiishi hapo kabla ya wanasayansi kuthibitisha kuwa jiwe lile ni kimondo, hivyo kulipa jiwe hilo hadhi ya pekee kulinganisha na mawe mengine yaliyopo kijijini hapo.

Baada ya uthibitisho huo wanasayansi, watalii, na watu wengine wadadisi kwa mamia wamekuwa wakitembelea eneo hilo. Hapo awali ilikuwa kutembelea eneo hilo ilikuwa bure kabisa lakini baadaye serikali ikaweka ada ya kuliangalia jiwe hilo. Jambo hilo halikuwa baya kwani kijiji na serikali vilipata fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

Tofauti na awali ambapo wanakijiji walifurahia kupokea wageni na kunufaika kiuchumi sasa jiwe lile (kimondo) limezua balaa. Wananchi wanatakiwa kuondoka eneo hilo ili serikali ijenge wigo kwa ajili ya wanyama wa porini (Zoo) ili kuongeza vivutio kwa watu wengi zaidi kutembelea eneo hilo.

Kitendo hicho hakikubalika kabisa na hasa kuwaondoa wananchi bila stahiki na fidia za mali zao. Kwa nini serikali hii inayojinasibu kuheshimu haki za binadamu inataka kuwafanyia dhuluma wananchi wake kwa sababu ya wanyama wa porini? Kwani hakuna vivutio vingine nchi hii zaidi ya wanyama? Kwa nini serikali hii inapenda kuanzisha migogoro isiyo ya msingi na wananchi wake?

Hii inaonyesha wazi kabisa kuwa serikali hii haina watu wabunifu, wamekaririshwa kuwa wanyama pekee ndiyo kivutio cha utalii. Hivi haiwezekani serikali kujenga nyumba ya makumbusho (Museum) ambayo kwanza itachukua eneo dogo lakini pia itahifadhi vitu vya kale na vya utamaduni wa jamii ya watu wa mkoa wa Songwe. Pili itawawezesha wananchi wanaoishi eneo hilo kuendelea kukaa kwa amani na kuendeleza shughuli zao za kiuchumi.

Wakati umefika kwa serikali kujisafisha kwa kuondoa watumishi wanaokosa ubunifu katika kutekeleza majukumu yao na kuajiri wanaoweza kubuni miradi ambayo itawanufaisha wananchi na serikali kupata kipato bila kuathiri maisha ya watu na mazingira yaliyopo!
Wananchi wasikubali huo ujinga
 
Watanganyika tujipange sana kuhusu uyo kizimkazi hana nia njema nasi.
Yy akistaff teke zenji.kazi kwetu!!


KAZI ni kipimo cha UTU
 
Back
Top Bottom