Machache Kuhusu Kimondo Hoba (Namibia)

TESRA

JF-Expert Member
Nov 25, 2017
329
317
-Ni miaka 80000 iliyopita. Jiwe kubwa lililokuwa na uzito wa tani 60 lilianguka na kufika katika ardhi ya Namibia pembezoni mwa milima ya Otavi, ni km 20 kutoka mji wa Groot fontein.

- Mwaka 1920, bwana Jacob Hermanus Brits (alikuwa ni Boer), alienda shamban kwake na vifaa vyake vya kazi kwa ajili ya kuandaa shamba lake lililokuwa linapatikana eneo linaitwa Hoba si mbali na milima ya Otavi. Brits alianza kazi ya kulima mda mfupi tu baada ya kufika shambani, lakini alikutana na jiwe kubwa lilokuwa limetokeza toka ardhini.

-Alianza kuchimba zaidi ili aweze kulitoa lile jiwe lakin alipokuwa akiendelea kuchimba na ukubwa wa jiwe pia uliendelea kuongezeka. Alishindwa kuendelea na kazi ile ya kuchimba ili aweze kulitoa jiwe. Alienda kutoa taarifa kwa watu wengine ili waende kuona ukubwa wa lile jiwe lililokuwa shambani kwake. ndipo ilipokuja kugundulika kilikuwa ni kimondo kikubwa kilicho kuwa na upana wa mita 3, urefu wa mita 3, kimo ni mita 1 na uzito wa tani 60.
Taarifa zingine kuhusu kimondo cha Hoba
- Kimondo kilipewa jina la Hoba kutokana na kugundulika kwake katika eneo hilo la shamba lililoitwa Hoba.

- Ni kimondo chenye uzito mkuwa zaidi duniani mpaka sasa. kinashika nafasi ya kwanza kwa uzito duniani kikiwa na tani 60.

-Kimeundwa na madini mbalimbali kama vile Iron 82.4%, Nickel 16.4% pamoja na Cobalt, Copper, Zink, Iridium, Carbon, Surphur, Germanium, Gallium na Chromium.

-Kimondo cha Hoba kinakisiwa kuwa na miaka zaidi ya billion 4 toka kuundwa kwake. lakini hapa duniani kimekuwa na miaka elf 80 toka kuanguka kwake toka angani.

-Mwaka 1955 serikali ya Namibia ilikiweka kimondo cha Hoba kwenye orodha ya vitu vya kiutalii katika nchi hiyo kutokana kualibiwa na majangili . Watu walianza kukata baadhi ya sehemu ya kimondo kwa ajili ya kuuza chuma. Mwaka 1985 kimondo cha Hoba kilijendelewa kwa mawe yaliyokuwa yamezunguka kimondo hicho kwa mtindo wa kiwanja cha mpira mpira.
Hoba-Intro (1).jpg


-----kama kutakuwa na makosa ya kisarufi very sorry------
 
Dunia ya sasa habari bila picha video clip sw na takataka TU.



KAZI ni kipimo cha UTU
 
Back
Top Bottom