Kitambulisho cha Taifa, Passport nini cha muhimu zaidi?

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,933
0002_968a7.JPG

Kitambulisho cha Taifa nini umuhimu wake kwa walio tayari na vitambulisho vingine vinavyotambuliwa kitaifa hata kimataifa?
Kuna wenye
  • Passport ambayo humvusha nje ya Tanzania
  • Kitambulisho cha mpiga kura nacho kinaonyesha uzawa wa mwenye kumiliki
  • Driving licence nisingependa kukiambatanisha na vitambulisho vya kitaifa kwa sababu hata asiye raia anaweaa kupata.
Kwangu bora nibaki tu na passport yangu ina nafasi kubwa zaidi ya kitambulisho cha Taifa. Kitambulisho cha Taifa hakitanivusha customs pale airport au Sea Port.

Je, wenzangu mnasemaje kuhusu hili?
 
Usijidanganye ndugu: siku hizi ukitaka kupanda treni ya mkoa lazima uwe na utambulisho wa kitaifa kwanza ndo upate tiketi.
 
Hati ya kusafiria ndio ID yenye enough info..hata mimi nakumbuka information nlizotoa katika kitambulisho cha uraia ni nusu ya nlizoweka kwene passport. Duniani huko hati ya kusafiria ndo kila kitu.

Lakini pia huko duniani iwe i US, UK nk wanazo pia Citizen IDs

Mfano ya George W Bush hii hapa https://encrypted-tbn2.gstatic.com/...Ayv8jvYeWHvYPJN0-uaOH126a4Rk2CIz468uvAFworv0q

kingine hiki https://encrypted-tbn3.gstatic.com/...1-k8N4nBwEIsGVfVj1wlrJ-Z8smSXWGBnoZgv72YEW05Q
 
Hati ya kusafiria ndio ID yenye enough info..hata mimi nakumbuka information nlizotoa katika kitambulisho cha uraia ni nusu ya nlizoweka kwene passport. Duniani huko hati ya kusafiria ndo kila kitu.
tatizo hapa ni ile ile theory ya "it's our time to eat'. na ndio maana hatutakaa tukaenda mbele mbali na kubadilishana migodi na ujenzi wa bomba la mafuta!
Hebu angalia hivi vitambulisho:
- TIN certificate
- Cheti cha kuzaliwa
- Kitambulisho cha mpiga kura
- Hati ya kusafiria (passport)
- Driving Licence
- Kitambulisho cha raia

Cha hajabu taarifa zote kwenye hizi documents zi sawa kwa karibia 100% na zinamilikiwa na entity moja ambayo inatumia 'STJ' - Serikali. Sasa ni kwa nini zisiwe kwenye taasisi moja!!!??

Kitambulisho cha Taifa na passport kila kimoja kina umuhimu wake:
  1. Kitabulisho cha Taifa kitakumbulisha uraia wako na shughuli zako za kila siku. Kitasaidia mamlaka mbalimbali kujua uhalali wa shughuli zako na mchango wako katika pato la Taifa. Aidha hata ukiwa nje ya nchi unaweza kukitumia kujitambulisha endapo utapata matatizo yo yote ikiwa ni pamoja na kupotelewa na passport yako. Kitambulisho cha Taifa kitakuwezesha kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii na kimaendeleo nchini bila kutiliwa shaka na mtu ye yote. Kitambulisho cha Taifa ni cha KUDUMU! Kitambulisho cha Taifa hakiwezi kutumika kama hati ya kusafiria (PASSPORT)!
  2. Hati ya kusafiria (Passport) itakuwezesha wewe kusafiri mahala po pote duniani na pia kukuwezesha wewe kuomba kutembelea, kufanya kazi au kukaa katika nchi yo yote duniani. Pamoja na kwamba passport inaonyesha uraia wako lakini matumizi yake ni ya MUDA MAALUM! Kwa maneno mengine ina UKOMO WA MATUMIZI! Aidha PASSPORT zinatolewa kulingana na hadhi ya msafiri au madhumuni ya safari. Hivyo kuna hati za kawaida ambazo hutolewa kwa kila mtu; kuna hati za kibalozi ambazo ukisafiri unaweza kuruka baadhi ya taratibu zikiwemo za ukaguzi; kuna hati za watu mashuhuri ambazo zitakuwezesha wewe kupata huduma maalum kama vile ulinzi n.k.
 
tusipo kuwa makini na suala hili ni wazi kuwa kuna watu watakosa haki ya kupiga kura mwaka 2015 kwa kigezo cha kitambulisho cha taifa
 
Sio mbaya kumiliki vyote, tusidharau
 
na wasio na driving license, voting cards (under 18) na passport (hii ni kwa wasafiri) watajitambulisha vp kama Watanzania?
 
Kitambulisho cha Taifa na passport kila kimoja kina umuhimu wake:
  1. Kitabulisho cha Taifa kitakumbulisha uraia wako na shughuli zako za kila siku. Kitasaidia mamlaka mbalimbali kujua uhalali wa shughuli zako na mchango wako katika pato la Taifa. Aidha hata ukiwa nje ya nchi unaweza kukitumia kujitambulisha endapo utapata matatizo yo yote ikiwa ni pamoja na kupotelewa na passport yako. Kitambulisho cha Taifa kitakuwezesha kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii na kimaendeleo nchini bila kutiliwa shaka na mtu ye yote. Kitambulisho cha Taifa ni cha KUDUMU! Kitambulisho cha Taifa hakiwezi kutumika kama hati ya kusafiria (PASSPORT)!

......., kwa hiyo hii picha inamdanganya rais

JK ID.jpg
Huu ni mradi mwingine wa ki :majani7:
 
Sidhani kama unajuwa unachokiongea mkuu au umekurupuka tu??check tena link zao then angalia ni vitambulisho vya aina gani hivyo ulivyoweka.

N.B UK hamna hayo mambo ya vitambulisho zaidi ya passport yao ndio inaongea kila kitu, hawana hela zakuchezea kama nchi yetu maskini TZ
 
na wasio na driving license, voting cards (under 18) na passport (hii ni kwa wasafiri) watajitambulisha vp kama Watanzania?

Kwa wasio na ID nyingine ndio wanaohitaji hivyo vitambulisho, lakini kwa aliye na Passport ni babu kubwa kuliko hilo ganda. Ganda linakuzungusha ndani ya mipaka ya nchi, na asiye nalo ataulizwa Driving license au passport.
 
Kitambulisho cha Taifa na passport kila kimoja kina umuhimu wake:
  1. Kitabulisho cha Taifa kitakumbulisha uraia wako na shughuli zako za kila siku. Kitasaidia mamlaka mbalimbali kujua uhalali wa shughuli zako na mchango wako katika pato la Taifa. Aidha hata ukiwa nje ya nchi unaweza kukitumia kujitambulisha endapo utapata matatizo yo yote ikiwa ni pamoja na kupotelewa na passport yako. Kitambulisho cha Taifa kitakuwezesha kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii na kimaendeleo nchini bila kutiliwa shaka na mtu ye yote. Kitambulisho cha Taifa ni cha KUDUMU! Kitambulisho cha Taifa hakiwezi kutumika kama hati ya kusafiria (PASSPORT)!

Sio kweli mkuu, ukiangalia picha ya kitambulisho cha Jakaya sehemu ya chini pale inaonesha Mwisho wa matumizi / expiry date. Rejea picha iliyoambatanishwa hapo juu.
 
Sidhani kama unajuwa unachokiongea mkuu au umekurupuka tu??check tena link zao then angalia ni vitambulisho vya aina gani hivyo ulivyoweka.

N.B UK hamna hayo mambo ya vitambulisho zaidi ya passport yao ndio inaongea kila kitu, hawana hela zakuchezea kama nchi yetu maskini TZ

Mbaya zaidi, eti hiki kitambulisho kina mwisho wa matumizi, halafu baada ya hap unaongezewa muda, kweli vichekesho!
 
Sio mbaya kumiliki vyote, tusidharau

Nina Passport, Driving license, birth certificate, Kitambulisho cha Mpiga picha, TIN number, sasa naongezewa kitambulisho cha Taifa, ni utitiri. Kwa anayehitaji sawa tu, lakini kwangu sioni umuhimu kwangu kwa vile Passport ina information zaidi ya hicho, papo hapo passport ni kitambulisho kinachonitambulisha uzawa, birth certificate nk.
 
Mbaya zaidi, eti hiki kitambulisho kina mwisho wa matumizi, halafu baada ya hap unaongezewa muda, kweli vichekesho!

Kitambulisho cho chote muhimu huwa na utaratibu wa muda kwisha kwa vile binadamu si jiwe, anabadilisha mahali anapoishi, anchi anayoishi kuhamia nchi nyingine, mabadiliko ya sura tokana na kukua au kuzeeka, nk. Hilo lipo po pote.
 
0002_968a7.JPG

Kitambulisho cha Taifa nini umuhimu wake kwa walio tayari na vitambulisho vingine vinavyotambuliwa kitaifa hata kimataifa?
Kuna wenye
  • Passport ambayo humvusha nje ya Tanzania
  • Kitambulisho cha mpiga kura nacho kinaonyesha uzawa wa mwenye kumiliki
  • Driving licence nisingependa kukiambatanisha na vitambulisho vya kitaifa kwa sababu hata asiye raia anaweaa kupata.
Kwangu bora nibaki tu na passport yangu ina nafasi kubwa zaidi ya kitambulisho cha Taifa. Kitambulisho cha Taifa hakitanivusha customs pale airport au Sea Port.

Je, wenzangu mnasemaje kuhusu hili?

tusha wahi kulijadili hili, unaturudisha nyuma mkubwa. kifupi ni kwamba ni matumizi mabaya ya fedha za taifa.
 
Back
Top Bottom