Kitambulisho cha Taifa, Passport nini cha muhimu zaidi?

Kitambulisho cha Taifa, Passport nini cha muhimu zaidi?

ni sawa lakini kumbuka yafuatayo:
TIN namba hapa ni kwa wafanyabiashara tu lakini kumbuka wafanyakazi wa serikali na umma (nssf, pspf, ppf, lapf nk) wanalipa kodi bila TIN. Na kwa vile kila raia inatakiwa kulipa kodi wangerekebisha tu contents na mambo yageenda.
birth certificate taarifa zote zilizomo (jina, tarehe ya kuzaliwa, mahali ulipozaliwa nk) ndivyo vilivyomo kwenye hizo zingine pia.
driving licence anaweza kuwa nayo hata mgeni lakini ya mtz ni tofauti na ya usa, kenya, uganda nk.
nimekjuelewa lakini cha msingi hapa ni kuwa na database moja yenye nguvu na kwa vile hivyo vitambulisho vyote nilivyovitaja vinatumia contents hizo hizo inakuwa hakua haja ya serikali hiyo hiyo kumiliki database saba zenye taarifa zinazofanana huku wote wakila mapadiem ya 'kufa mtu'!

Si kwa wafanyakazi tu, mimi si mfanyakazi lakini na TIN.
Kila mwananchi ni mlipa kodi na kila raia hata wahamiaji wanaoishi kihalali wanatakiwa kuwa na TIN kwa vile ndicho kitambusho cha mlipa kodi na kumbukumbu za kila mtu kwenye database. Ukitaka kupata habari za raia ye yote ni TIN hapo kila kinogaubaga unakipata. Mahakama, polisi, kusajiliwa ukazi vijiji na mijini, nyumba, mashamba nk yote yanatakiwa umiliki yatambuliwe si kwa jina tu ila pia kwa TIN ambayo mhusika ana-finger print kwenye database ya taifa.

Tanzania tuko bado, sasa ndio tunaanza. Uliza waliozoea huko zilikoanzia watakueleza. Mkazi wa UK akipeleka namba yake pale ubalozini watafungua computer na kuona kila kitu hata taswira ya sura yake.

MMarekani akifika ubalozini kwao akiwaambia namba ya social security kina kinoga ubaga watakipatga pale.

Kabla ya kupata TIN lazima uwe na birth certificate.

Tatizo wengi wetu wanabishi kwa sababu ya kukosa uzoefu, na tunaofahamu tunajitahidi kuwa wavumilivu kwani tunajua si makosa yako, ni kitu kipya, hata watumishi wa serikali wengi wao wahafahamu vizuri. Itafika wakati mambo yatakaa vizuri na haya ninayoyaandika yatakuja kurekebishika, kwa sasa tuendelee na hii hii mradi hakuna matatizo ya pekee.
 

Nadhani tatizo hujanisoma ninachokiongelea, itafika wakati tutaelewa kwa sasa ni mambo mapya kwa wengi. Mmoja alieleta mfano wa kitambulisho cha kitaifa cha marekani kama ifuatavyo:

images


Passport nchini Marekani hutolea na mamlaka ya Homeland Security Administration. Passport Marekani zinatolea za mitindo miwili ambayo ni:
  • Long form - book (Passport)
  • Short form - ganda ( Passport) ambayo haina uzito wa kusafiria nje ya nchi isipokuwa Canada.
Hivi ndivyo vitambulisho vya kitaifa Marekani.

Kuna vitambulisho vingine ambayo hutolewa kila state kwa wakazi wake na vina taratibu karibu zinazofanana lakini vina uzito kitaifa.
  • Driving license
  • Non Drivers for Identificaton only
Vitambulisho hivyo nitolewa na idara ya Motor vehicle.
Hivyo ni vitambulisho ambavyo unavitumia po pote na katika state yo yote nchini Marekani. Kuna vitambulisho kwa baadhi ya miji hutolea na county (wilaya) au jiji ambavyo havitambuliwi kitaifa bala sehemu vinakotolewa tu.
Taratibu za kupata vitambulisho hivyo ni:

  • TIN (Social Security number ambayo inatambuliwa kama Tax Identification Number)
  • Birth Cetificate
  • Proof ya bill kuonyesha makazi yako.

Jambo la msingi unaona hakuna utitiri wa mamlaka nyingi za utoaji vitambulisho, kwani hali ilivyo Tanzania ni rahisi kuleta igongano katika utendaji. Waandaji wa vitambulisho vya taifa lazima wapata data kutoka Revenue ambao ndio watoaji wa TIN na Driving Licence hali kadhalika business license.
Mamlaka ya utoaji vitambulisho Tanzania:
  • Driving Licence (Police - Revenue)
  • TIN (Revenue)
  • Passport - Mamlaka nyingine
  • Kitambulisho cha Taifa - Mamlaka nyingine
  • Usajiri wa uzazi (Birth Certificate) na usajili wa vifo - Mamlaka nyingine
  • Kitambulisho cha Mpiga kura - Mamlaka nyingine.
Ni utiriri wa mamlaka ambapo baadhi ya shughuli huingiliana na pengine kusababisha misuguano.


Kama nilivyoainisha hapo juu, kwa nini mamlaka ya Passport isifanye shughuli hiyo kwa vile Passport ni kitambulisho mojawapo cha kitaifa, hivyo basi ganda tunalopata lingekuwa ndio

  • Identification short form
na​

  • Passport ni Identification long form.

Kinachofanyika ni kile kile ambacho watoaji wa Passport wanafanya, tofauti ni kwamba tu wanatoa vitabu na hawa wanatoa ganda.

Jambo la msingi hujanielewa, sipingi watu kupata kitambulicho cha taifa, lakini ninachoongelea kwa walio na Passport binafsi sioni umuhimu wake wakati kuna vitambulisho vingine wanavyohodhi kama driving license. Passport ni kitambulisho cha kitaifa pia, asiye raia hawezi kupata passport.
mkuu hapo nakubalina na wewe, ninachokataa ni wewe kupinga japo sasa hivi umegeuka, ninachokumbuka ulisema bora nibaki na pasport yanhu. anyway mapendekezo yako ni mazuri lakini je yatawafikiaje wahusika. naamini kuhusi kitambulisho cha mpiga kura kitakufa baada ya hiki cha utaifa kwani hakitakua na maana tena..
 
mkuu hapo nakubalina na wewe, ninachokataa ni wewe kupinga japo sasa hivi umegeuka, ninachokumbuka ulisema bora nibaki na pasport yanhu. anyway mapendekezo yako ni mazuri lakini je yatawafikiaje wahusika. naamini kuhusi kitambulisho cha mpiga kura kitakufa baada ya hiki cha utaifa kwani hakitakua na maana tena..

Mbinu moja wapo ya kufikisha ujumbe ni kujaribu kuibua pengine hali ya kutokukubali ili kuchokoza mawazo ya watu, na kwa njia hii tunajifunza mengi. Katika mada hii nimeweza kuona viwango tofautitofauti, na si wote wenye uelewa wa kiwango chako kwa vile wengine tatizo hilo hawalioni bali mradi wana vitambulisho vya taifa. Si wote wanaojua kuwa kitambulisho cha Taifa ni kile kile kama kitabu cha passport ndio maana kuna information zote muhimu kama ilivyo passport. Si wote wanaojua umuhimu wa TIN kwa kila mwananchi ili taifa liwe na database za kila raia. Ndio maana wewe na mimi tunatakiwa kutokata tamaa kuwaelimisha wengine kwa vile mambo haya bado kwetu ni mageni.
 
kwa upande wangu mimi naona ni matumizi mabovu ya fedha za umma, hakizidishi chochote wala hakipunguzi chochote. Hakuna statistics za kweli zinaonyesha kama zitasaidia kupunguza uhalifu au kurahisisha masula ya utendaji. Kitambulisho kimekuwa pushed na western goverments kwa misingi ya kuweka reckords za wananchi ili kuwa na njia ya kuwasaidia katika war against terrorism, lakini kwa nchi masikini basi cost yake inazidi umuhimu wake, ziko nchi zisizo na ID za raia wake na zimeendelea zaidizikiwa na ufanisi zaidi kuliko zenye vitambulisho.

Ufaransa ni moja ya nchi yenye mfumo wa ID cards, na sababu kubwa inayoingilika akilini ni uzuiaji wa uhamiaji haramu, jambo la kwanza unaposimamishwa na askari wa kifaransa ni papers zako za kuishi, lakini jirani zao UK serikali ya Blair ilipotaka kuintroduce ID cards wananchi na wabunge wao waligoma kwa sababu ya cost zake pamoja na ukweli kwamba haitozuia uhalifu, nafikiri kama nchi nyengine zilionendelea ziazofanya badala ya kuweka ID cards wangehakikisha huduma za utoaji wa passport ikawa ni haki ya kila mwanachi kuanzia mtoto mchanga mpaka vizee, bila ya bughudha na mashaka, ingelikuwa na faida kwanza kama ni kitambulisho cha utaifa wako pili kama ni document muhimu ya halali inayotambulika duniani nzima kwa shughuli za usafiri.

Tiuge yenye faida, kwa hili cost out weighs merits.
 
Back
Top Bottom