Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,921
- 30,265
- Thread starter
-
- #101
Huu ujanja wa kutaka kuwaongeza Wpagani katika Tanzania hauwezi kusaidia kitu kwa kuwa hawapo.
Kwa kweli ukitaka tuwe na mjadala mzuri ni lazima kwanza usome kitabu ujilete katika hali ya kujua.
Vinginevyo itakuwa tunazungushana humo kwa humo na hii haina tija.
Upon reaching Mwembe Togwa (now known as Fire) at the junction of (Ronald Cameroon Road (now United Nations Road) and Morogoro Road Mwalimu Nyerere met Mshume Kiyate.
Mwalimu Nyerere told Mshume Kiyate that he was going to Kariakoo Market to buy provisions but he did have a single sent in his pocket. Mshume Kiyate dipped his hand into his pocket and gave Mwalimu Nyerere two hundred shillings.
Bwana Saidi Mohamed, hebu angalia hiki kipande katika kitabu chako
Nadhani hapo kwenye "sent" ulimaanisha "Cent", anyway swali langu ni hili, je Mwalimu alikuwa na Senti moja mfukoni au alikuwa hana Senti hata moja?.
Na kama alikuwa hana senti hata moja mfukoni , je alikuwa anakwenda kariakoo kununua provisions zipi?
Na kama alikuwa na senti moja tu, je kwa wakati huo angeweza kununua provisions zozote kiasi cha kumfanya afunge safari kwenda kariakoo?
Nafikiri Mzee Nyerere alikua anaogopa zaidi udini kuliko dini ya Kiislamu.....nafikiri mawazo yake yalikua kwamba hichi kitabu kingeamsha waislamu kuwafanya wahisi wanahaki zaidi ya watu wengine (wakristu+dini nyengine/aethists) katika jamhuri kwani wao ndio waliochangia zaidi...hili sasa lingeleta mtafaruku na ndilo aliloogopa...vut=rugu za kidini!!
Mbogoni kitabu chake kiliruhusiwa kuingia nchini na maudhui ni hayo hayo lakini kitabu cha Hamza Njozi "Mwembechai Killings" kilipigwa marufuku ukikutwa nacho ni kosa la jinai na maudhui ni hayo hayo.
Labda nikuulize serikali inaogopa nini?
Sasa hizo nukuu za Mbogoni hazina maana yoyote ikiwa yeye ataruhusiwa kusema peke yake.
Waislam tunakijua kinachoogopewa.
Hujajibu hoja. Hoja ni madai yako kwamba EAMWS ilipigwa marufuku kwa shinikizo ya kanisa Katoliki. Hapa unaruka na kusema kitabu cha Mbogoni kiliruhusiwa kuingia lakini cha Njozi kilipigwa marufuku. Nimevisoma vyote. Kitabu cha Mbogoni ni more rational wakati kitabu cha Njozi kina ushabiki wa Kiislamu zaidi. Maudhui ni tofauti. Na kuhusu wapagani ni kweli idadi yao imekuwa inapungua kutokana na kazi zinazofanywa na shule, makanisa na misikiti. Niliposoma shule kule Musoma, miaka ya 60 nusu ya wanafunzi walikuwa wapagani, lakini leo wengi ni Wakristo au waislamu baada ya kwenda shuleni. Lakini jibu hoja kuhusu kanisa Katoliki na EAMWS.
Umekisoma hicho kitabu hata ukatoa comments hizo hapo juu? Soma halafu ueleze ni page gani na gani mwandishi amemaanisha udini.
Jee, umekisoma kitabu tajwa kwenye hii mada?
Ndiyo nimeshakisoma hicho kitabu hata ninayo nakala hapa nyumbani kama nilivyo na nakala ya kitabu cha Mbogoni na Judith Listowell. Lakini jibuni hoja. Onyesheni ni wapi kanisa Katoliki lilihusika katika kufutwa kwa EAMWS.Jee, umekisoma kitabu tajwa kwenye hii mada?
Yote hayo tisa. Mimi nimeuliza swali moja tu. Ushahidi uko wapi kwamba kanisa Katoliki lilihusika katika kupigwa marufuku kwa EAMWS? Kumbuka kitabu chako ni rekodi.Itakuwa bora kama utasoma kitabu kwanza na kisha ndiyo utoe maoni. Nimeeleza matatizo yalianza toka 1963 na hapa ukienda katika kitabu utakutana na Sheikh Hassan bin Amir akieleza njama zilivyoanza na jinsi na yeye alivyojaribu kupambananazo. Elewa kuwa huyu ndie alikuwa Mufti wa Tanganyika na Zanzibar na mchango wake kwa Nyerere na TANU hauna kifano.
Utamkuta Bilal Rehani Waikela (yu hai na Allah ampe umri mrefu. Amin) anaeleza mipango waliyopanga ndani ya EAMWS kupambana na fitna za Kanisa Katoliki dhidi ya kujengwa kwa Chuo Kikuu cha Waislam.
Utasoma maungamo ya Shaban Kayugwa (State Intelligence 1960s) aliyuhusika katika kukamilisha fitna ile. Nini aliwaeleza Waislam kabla mauti hayajamfika.
Mwisho utamkuta Bibi Titi Mohamed ndani ya Kamati Kuu ya TANU alivyotoleana maneno na Nyerere na Titi akamwambia Nyerere "Mimi namuogopa Allah simwogopi yoyote." Ugomvi wao ni kuwa Titi alikuwa anapinga kufungiwa kwa EAMWS akisema imekuwapo kabla ya TANU na ina manufaa makubwa kwa Waislam na Uislam na Nyerere akishinikiza EAMWS ivunjwe.
Mwisho utamsikiza mrehemu Hamza Azizi aliyekuwa IGP wakati ule nini alinambia mimi na wengine ili aende kwa Mola wake akiwa ana radhi ya Allah.
Utamsoma Godfrey Sawaya aliyekuwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai alivyokuwa akitisha Waislam viongozi wa EAMWS.
Ukisoma haya yote kwa ukamilifu wake utakuwa katika nafasi ya kuzungumza utakacho.
Yote hayo tisa. Mimi nimeuliza swali moja tu. Ushahidi uko wapi kwamba kanisa Katoliki lilihusika katika kupigwa marufuku kwa EAMWS? Kumbuka kitabu chako ni rekodi. Na kama rekodi imekosewa vizazi vijavyo vitayachukulia hayo makosa kama ni ukweli isipokuwa kama kuna mtu atajitokeza kuyasahihisha makosa hayo hivi sasa. Kubali kuwa ni dhana yako tu kwamba kanisa Katoliki lilihusika katika upigaji marufuku wa EAMWS na siyo fact.