Asilimia kuubwa ya maneno ya kiswahili yanatokana na Kiarabu, hakuna lugha duniani inaitwa kibantu, kibantu ni mchanganyiko wa lugha nyingi za watu wenye asili ya kibantu. Watu wenye asili ya kibantu hupatikana kusini mwa sahara. Wale wa Afrika wengine wasio wabantu, ambao na hapa kwetu wapo wengi tu, kama vile wamasai, waIraqw, waRangi, wa Zanaki, waJaluo na kadhalika, utakuta wana asili za kiarabu kwenye lugha zao. Ikumbwe pia uArabu ni lugha na si utaifa. Kuna mataifa mengi katika Afrika yanayoongea kiarabu na wao hujiita wa Arabu, si kwa uTaifa bali kwa lugha.
Ukichukuwa Kiarabu na lugha ambazo si za kibantu lakini za kiafrika zilizongiza maneno yake kwenye kiswahili utakuta kuwa maneno ya lugha za kibantu si mengi sana katika kiswahili, hayawezi fika asilimia 40%, asilimia chache zingine zinatokana na lugha za nchi ambazo zilikuwa na muingiliano mkubwa wa kibiashara na utawala katika pwani ya afrika mashariki, kama vile Kireno, Kijerumani, Kiingereza, Kihindi, Kichina.
Duniani, kila mawasiliano yanavyozidi ndio lugha huchukuwa maneno kila muingiliano wa mataifa unapozidi, ni lugha chache sana zinazojitolesheza na maneno yake yeneyewe, na hizi ni lugha za zamani na huitwa kugha tajiri, utajiri wa kuwa na maneno mengi.
Kiswahili kimebahatika kuwa na maneno mengi ya Kiarabu (Kiarabu ni Lugha tajiri) na nadhani ni hivi ppunde tu na chenyewe kitakuwa moja ya lugha tajiri.
Kwa sasa, kuna hujuma za wazi za kukitowa kishahili kutoka uasili wa kiarabu kwa sababu tu uarabu unahusishwa na uIslaam. Kilanjia zinafanyika kubuni maneno mapaya ambayo hayana hata msamiati wala lafdhi za kiswahili, ili mradi tu, kitoke kwenye asili yake ya asili.
Baraza la kiswahili limeingiliwa na watu wasio na asili ya lugha ya kiswahili. Wenye asili ya lugha ya kiswahili ni watu wa pwani ya Afrika Mashariki na wanaoongea kiswahili kama lugha mama.
Hta neno ki- swahili lenyewe linatokana na kiarabu "sahil", pwani, "sawahil" watu wa pwani.